Monday, March 09, 2009

Wikipedia- Kiswahili

_Watanzania wote wanakaribishwa kuchangia habari za mahali
wanapoishi au wanapotoka katika wikipedia ya Kiswahili! (sw.wikipedia.com) Ijulikane ya
kwamba wikipedia ni mradi mkubwa wa elimu unaojengwa na wachangiaji
wanaojitolea bila malipo yoyote. Kila mtu anakaribishwa kuchangia!

Kwa sasa tumeanzisha makala fupi za kila kata kwenye mikoa ya Arusha,
Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Kigoma, Lindi, Mara, Mwanza,
Mbeya, Manyara, Morogoro, Mtwara, Pwani na Tanga.

Angalia ukienda anwani hii: sw.wikipedia.org/wiki/Mkoa_wa_Arusha.

Chini kuna sanduku inayoonyesha mikoa yote. Ukiingia katika mkoa fulani unapata majina ya
wilaya. Kila safari ukibonyeza kwenye neno lenye rangi ya buluu
unapelekwa kwenye makala mpya. Ukifika kwenye wilaya utaona sanduku
lenye majina ya kata za eneo hili. Makala mengi yana habari fupi tu kama
"ABC ni kata ya wilaya DEF katika Mkoa wa XYZ. Idadi ya wakazi wake
ilihesabiwa kuwa xxxxx katika sensa ya 2002". Kila mtu yuko huru
kubonyeza kwenye sehemu ya "hariri" juu ya makala na kuongeza habari.
Baada ya kuongeza habari unabonyeza sehemu ya "Hifadhi ukurasa" iliyoko
chini.

Si vigumu na hapa unaweza kuingiza habari juu ya watu, historia,
utamaduni na taasisi zilizopo katika eneo la kata hii.

Karibuni sana tutawaarifu wakati mikoa mingine itakuwa tayari!

Monday, February 09, 2009

HAKUNA APANDAYE JUU YA MTI KUTAFUTA SAMAKI!!

kooooorti!!!watu wote wanasimama kuashiria mheshiwa hakimu kashatia maguu ndani ya mjengo...prosija za mahakama zinaendelea na baada ya muda mreefu tangu 2006 hatimaye leo kile kitendawili cha KATI YA ULIMI NA MENO NANI MPANGAJI NDANI YA KINYWA kinaanza kujibiwa...najua unashauku ya kutaka kujua nazungumzia nini...Ni yule jamaa alikuwa mtu mzito ndani ya Geshi la polisi...A.Zombe...akiwa na washikadau wenzake kwa kesi ya kuua wafanyabiashara wa madini..Nimekuwa nikifuatilia kesi hii na hapa mwishoni mwakili wa Zombe wanadai mteja wao hana kesi y kujibu eti kwa sababu ushahi ulotolewa unaonyesha hakuwepo eneo la tukio..kweli kila mtu na kazi yake...ukiwa wakili lazma ukubali kuwa na uwezo wa kujipiga ganzi...Haya...Ushahidi unaonyesha kuwa order zote zilitoka kwa zombe...hapa ni kwamba hata kama hakuwepo ktk eneo bado anakesi ya kujibu..MATUMIZI MABAYA YA OFISI...na hapo ndipo napotaka kutundika mawazo yangu...kilaiini kama kuweka shati kwenye msumari...Ninaposema hakuna mtu mzima mwenye akili timamu amabye anaweza kupanda hadi juu ya mti na kisha akiulizwa anatafuta nini!?aseme" NATAFUTA SAMAKI"namaanisha kwamba Zombe na wenzake walijua dhahiri walichokuwa wanafanya..na hivyo umefika wakati wa wao kuambiwa"KWENYE MTI HUWA KUNA MATUNDA"...ili jamii yetu iweze kuwa na imani na vyombo vyake vya sheria tunategemea kuona Zombe na wenzake wakipata matunda ya kazi yao..Kwani kama Zombe ndiye mwenye nyumba basi Mahakama imtoe na kicheko..lakini kama yeye na wenzake na wapangaji ndani ya kinywa(SHERIA)basi mwenye kupewa notice apewe!!!vinginevyo itakuwa sawa na kile kitendawili cha KATI YA NGUO NA MWILI NANI ANAYEMBANA MWENZAKE???!!

Tuesday, June 12, 2007

Askofu agawa kondomu

Alhamisi ya tarehe 7 Juni 2007, BBC ilirusha kipindi cha Hard Talk ambapo mwandishi maarufu Steven Suckur alifanya mahojiano na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Rusternburg Nchini Afrika ya Kusini. Askofu huyo, Kevin Dowling alikiri kugawa kondomu kwa watu ili wajikinge na maambukizi ya UKIMWI. Alisema kwamba yeye kama askofu ameshuhudia mengi, anaona watu wakifa ambapo pengine wangestahili kupona. Alisema katika moja ya kliniki sehemu hizo, asilimia 50 ya wanawake wanaohudhuria kliniki ya wajawazito wameambukizwa virusi vya UKIMWI. Wengi wa wanaothirika ni wahamiaji masikini kutoka katika majimbo yenye hali mbaya sana kimaisha hase jimbo la Eastern Cape. Baadhi ya wahamiaji hao huja kutafuta namna ya kujikwamua kimaisha katika maeneo hayo ambapo kuna mgodi wa madini, lakini wengi hasa wanawake hujikuta wakijihusisha na ngono kama njia ya kujikimu baada ya kukuta hakuna cha kufanya.

Alipoulizwa kama haoni huku ni kupingana na Vatican, Askofu huyo ambaye pia alikuwa mmoja wa wapambanaji wa mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini humo alisema ni kweli mtazamo wa kanisa si huo lakini yeye anaangalia hali halisi na mazingira aliyomo. Anasema akiwatembelea watu katika maeneo hayo wanaoishi kwenye vibanda vibovu kabisa anawakuta wengi wakiwa katika hali mbaya sana jambo linalomfanya ahisi kwamba wangeweza kupona kama wangejikinga. Hilo linamsukuma kuwagawia kondomu watu wengi ili kuponya maisha yao na madhara yanayoambatana na UKIMWI. Anaendelea kusema kuwa watu anaowahudumia si wakatoliki tu bali ni kutoka katika dini na madhehebu mbalimbali na kwamba anachofanya ni kujaribu kuwasaidia watu kutua mizigo na si kuwatwisha kama neno la bwana linavyonena!

Askofu agawa kondomu

Alhamisi ya tarehe 7 Juni 2007, BBC ilirusha kipindi cha Hard Talk ambapo mwandishi maarufu Steven Suckur alifanya mahojiano na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Rusternburg Nchini Afrika ya Kusini. Askofu huyo, Kevin Dowlin alikiri kugawa kondomu kwa watu ili wajikinge na maambukizi ya UKIMWI. Alisema kwamba yeye kama askofu ameshuhudia mengi, anaona watu wakifa ambapo pengine wangestahili kupona. Alisema katika moja ya kliniki sehemu hizo, asilimia 50 ya wanawake wanaohudhuria kliniki ya wajawazito wameambukizwa virusi vya UKIMWI. Wengi wa wanaothirika ni wahamiaji masikini kutoka katika majimbo yenye hali mbaya sana kimaisha hase jimbo la Eastern Cape. Baadhi ya wahamiaji hao huja kutafuta namna ya kujikwamua kimaisha katika maeneo hayo ambapo kuna mgodi wa madini, lakini wengi hasa wanawake hujikuta wakijihusisha na ngono kama njia ya kujikimu baada ya kukuta hakuna cha kufanya.

Alipoulizwa kama haoni huku ni kupingana na Vatican, Askofu huyo ambaye pia alikuwa mmoja wa wapambanaji wa mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini humo alisema ni kweli mtazamo wa kanisa si huo lakini yeye anaangalia hali halisi na mazingira aliyomo. Anasema akiwatembelea watu katika maeneo hayo wanaoishi kwenye vibanda vibovu kabisa anawakuta wengi wakiwa katika hali mbaya sana jambo linalomfanya ahisi kwamba wangeweza kupona kama wangejikinga. Hilo linamsukuma kuwagawia kondomu watu wengi ili kuponya maisha yao na madhara yanayoambatana na UKIMWI. Anaendelea kusema kuwa watu anaowahudumia si wakatoliki tu bali ni kutoka katika dini na madhehebu mbalimbali na kwamba anachofanya ni kujaribu kuwasaidia watu kutua mizigo na si kuwatwisha kama neno la bwana linavyonena!

Wednesday, June 06, 2007

Paper ya padre Karugendo

Padre Karugendo hivi karibuni alitoa mada kuhusu kujikinga na UKIMWI katika usharika wa Chuo Kikuu DSM. Naiweka hapa ili uisome.
KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Waheshimiwa mabibi na mabwana. Bwana asifiwe!
Tuombe:
Tumwombe Mungu Mwenyezi muweza wa yote,
Muumba wa Mbingu na Dunia,
Mwenye wingi wa upendo, huruma na hekima,
Mwenye kujali na kusamehe,
Anayetujalia Uhai,uhuru na utashi,
Anayetufunulia kila kitu mpaka kututumia
Mwanaye wa pekee kuja kutukomboa;
Atushushie roho wake Mtakatifu,
Aje kutuongoza katika maongezi yetu ya leo.
Kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu. Amen!

Ninawashukuru sana kunikaribisha katika Usharika wenu wa Chuo Kikuu, ili tuweze kushirikiana katika kujadili na kuelimishana juu ya ugonjwa hatari wa UKIMWI.

Katika maongezi yangu nitaongozwa na masomo matatu:

“Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na atapata malisho. Mwizi huja kwa sababu ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uzima- uzima kamili” ( Yohana 10:9).

2. “Kama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo pia alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhai” (Yohana 5: 26).

3. “Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma” (Yohana 17:21)

UKIMWI, ni somo pana sana na linagusa nyanja zote katika maisha yetu. Hivyo kuna mambo mengi ya kujadili juu ya ugonjwa huu. Mengi yamejadiliwa na bado mijadala inaendelea na ndiyo maana tuko hapa siku ya leo. Imani yangu ni kwamba kwa vile hapa ni sehemu ya wasomi. Mijadala kama Ukimwi ni nini, Virusi vya Ukimwi ni nini, Ukimwi ulianzia wapi, Ukimwi unaambukiza kwa njia zipi, njia za kujikinga,dawa za kurefusha maisha na utata mwingi unaozunguka ugonjwa huu si mipya. Na kwa vile kuna wachangiaji wengine, basi niwaombe niongelee kipengele kimoja: Kujikinga na Maambukizi ya UKIMWI. Nikiwa na lengo la kusisitiza wajibu wetu wakristu wa kulinda na kuutunza uhai. Kama anavyosema Bwana wetu Yesu kristu: “Mimi nimekuja mpate kuwa na uzima- uzima kamili.”

UKIMWI, unaambukiza kwa njia mbali mbali. Nafikiri na hili si geni kwenu. Nawaomba niongelee njia moja tu inayosambaza ugonjwa huu kwa asilimia kubwa: Ngono.

Sintaingia kwenye upande wa Ushoga na Usagaji. Nitajikita kwenye kujamiana katika hali ya kawaida inayokubalika katika jamii na katika kanisa.

Wataalamu wa jambo hili la kujingina na maambukizi ya Ukimwi (Ngono), wanapendekeza njia kama tatu. Padri Joinet, ambaye amekuwa mstari wa mbele,katika swala hili la kujikingia na maambukizo ya Ukimwi, anaoegelea mashua tatu. Yeye anauchukulia UKIMWI, kama mafuriko – na kwamba watu wanatafuta namna ya kuokoa maisha yao kwa kuyakimbia mafuriko. Mashua hizi tatu ni:
Uaminifu
Kujinyima
Kondomu.

Yeye anasema kwa vile mtu ana uhuru na utashi, na kwa vile kuna njia tatu za kujikinga – hakuna haja ya kupoteza maisha. Mashua zote ni salama, hivyo kila mtu anaweza kujiponya kwa kuchagua mashua mojawapo. Na anasema mambo kama yakikwendea vibaya kwenye mashua moja, basi mtu unaweza kuamua kuhamia kwenye mashua nyingine. Anasema ni uzembe na kutojali mtu kufa kwa mafuriko wakati mashua zipo. Ni zaidi ya miaka 15, Fr. Joinet, akihubiri juu ya mashua tatu, lakini maambukizi ya virusi vya UKIMWI bado yanashika kasi ya kutisha. Maana yake ni kwamba, kuna baadhi ya watu wanaamua kufa kwa mafuriko kuliko kuingia kwenye mashua mojawapo!

Wengine kama Mheshimiwa Askofu Gamanywa, wanaongelea kitu kilekile, lakini kwa mtanzamo mwingine na kwa kukwepa Kondomu;
Subiri
Tosheka naye
Acha kabisa.

Njia hizi nazo ni salama kabisa. Lakini la kushangaza, ni kwamba maambukizi ya UKIMWI, yanapanda badala ya kushuka. Maeneo mengine yanashuka kidogo – lakini kwa wastani hapa Tanzania maabukizi ya virusi vya UKIWMI bado yako juu.

Kwa sabablu zilizojuu ya uwezo wangu, ninawaomba niongelee njia mbili tu:
Uaminifu
Kondomu.

Maana hizi nyingine:
Kujinyima
Acha kabisa.

Ni za watu wachache sana ambao ninafikiri hawaishi katika dunia yetu hii. Hizi ni za wateule wachache. Nafikiri sisi tunatafuta njia za kuwakinga watu wengi, jamii nzima. Hivyo hizi za wateule wachache hazitusaidii sana.

Uaminifu.

Kile ambacho Padri Joinet, anakiita Mashua ya Uaminifu, ndicho Askofu Gamanywa na viongozi wengine wa dini wanakiita Tosheka naye. Maana yake ni kwamba mtu awe na mpenzi mmoja. Mme mmoja, mke mmoja! Kwa kuzuia maambukizi ya UKIMWI, hii ni njia nzuri kuliko zote!

Jambo hili si jipya katika kanisa. Ndoa ya kikristu ni ya mme mmoja, mmke mmoja. Hiyo ndiyo maana ya tosheka naye. Kwenda kinyume ni kuvunja uaminifu.

Sote tumekwisha shuhudia ndoa za Kikristu zinazofunjika, tumeshuhudia wakristu wenye wanawake zaidi ya wawili, tumeshuhudia nyumba ndogo, tumeshuhudia watoto wanaozaliwa nje ya ndoa nk. Nisingependa kuingia sana katika jambo hili. Kitu ninachopenda kujadiliana na nyinyi ni je:
Kuna Uaminifu katika ndoa za Kikristu?
Uaminifu ni kitu kinachowezekana katika ndoa na katika mapenzi?
Maana kama Uaminifu ni njia nzuri ya kujikinga maabukizi ya Ukimwi, ni bora tukahakikisha kama kweli njia hii ni salama, vinginevyo tunajiingiza katika hatari.Mfano:

Mimi ni Padri wa Kanisa Katoliki. Sisi wakatoliki tuna kitu kinachoitwa Sakramenti ya kitubio. Waumini wanatubu dhambi zao kwa Padri. Sina lengo na kutaja dhambi za watu. Ninautumia huu kama mfano wa kutusaidia. Kwa kipindi cha miaka 18, niliyoungamisha, sikukutana na familia hata moja yenye Uaminifu katika ndoa. Sikukutana na mtu hata mmoja, mwenye uaminifu katika mapenzi:

Kwa maana kwamba kila mtu mwenye ndoa niliyemuungamisha, alitaja dhambi ya kuzini na kutembea nje ya ndoa!

Kwa maana kwamba kila mtu mwenye mpenzi niliyemuungamisha, alitaja dhambi ya kukosa uaminifu kwa mpenzi wake.

Nimeishi Ulaya, nimeungamisha, hali ilikuwa hivyo hivyo. Nimeishi Mbeya, nimeugamisha, hali ilikuwa hivyo hivyo. Nimeishi Karagwe, nimeungamisha, hali ilikuwa hivyo hivyo. Ninataja sehemu mbali mbali ili isije ikachukuliwa kwamba tabia ya kutokuwa na uaminifu katika ndoa na mapenzi ni ya sehemu Fulani.

Nimekaa kwenye parokia moja ya Bushagaro Karagwe, kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi. Kipindi chote hicho nimeshuhudia watu wakifa kwa UKIMWI. Watu niliowafahamu, niliowaungamisha, watu tuliokuwa tukisali pamoja. Kwa kipindi chote hicho nimeshuhudia watu walio kwenye ndoa na wenye wapenzi wakiungama dhambi ya kuzini. Na kipindi hicho UKIMWI, ulikuwa unapamba moto.

Mapadri haturuhusiwi kutaja au kutumia maungamo kwa namna yoyote ile. Hata kama unajua kwamba aliyeungama ametembea na mtu mwenye virusi, wakati amemwacha mke wake nyumbani, unakaa kimya. Badala ya kutetea Uhai, unabariki kifo!

Je, katika hali kama hii tunaweza kusema kwamba uaminifu ni njia ya kukinga maambukizi ya Ukimwi? Labda tatizo la kutokuwa na uaminifu katika ndoa ni la wakatoliki peke yao? Inawezekana kwenu nyinyi Walutheri ni tofauti? Nafikiri nitakuwa nimechokaza majadiliano.

Mwaka 2002, niliamua kukataa kubariki vifo na kuanza kutetea uhai kwa nguvu zangu zote.Nilivunja ukimya na kuwashawishi waumini kuuvunja ukimya ili tushirikiane kwa pamoja kupambana na maambukizi ya UKIMWI. Niliunga mkono matumizi ya kondomu. Katika mkutano wa “National Multisectoral Aids Conference” nilitoa mada na kuwaomba waheshimiwa Maaskofu kuvunja ukimya. Maana kama kuna watu wenye ushuhuda kwamba uaminifu katika ndoa ni kitu kigumu ni mapadri wa kanisa Katoliki. Niliwaomba maaskofu kama hawapendi kuunga mkono matumizi ya kondomu, basi wanyamaze. Au waendeshe kampeni ya chini kwa chini. Maana maaskofu wana ushawishi mkubwa, wakisema kondomu ni dhambi, watu wanafuata hata bila ya kufikiri kwanza.Jambo hili liliniingiza matatani na uongozi wa Kanisa katoliki hadi leo hii.

Ukweli ndo huo, kwamba hadi leo hii Mapadri tunaendelea kuchochea maambukizi ya Ukimwi. Watu wanaungama kuzini, tunawabariki na kuwasafisha. Wanarudi kuzini – wakirudi tunawabariki na kuwasafisha. Ni mzuguko usiokuwa na mwisho. Tunabariki vifo, badala ya kubariki uhai! Na kwa nguvu zote tunaendelea kuhubiri kwamba njia pekee ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni uaminifu na Tosheka naye. Nitakuwa nimechochea majadiliano zaidi?

KONDOMU.


Wataalamu wanasema Kondomu, ikitumiwa vizuri ina uwezo wa kuzuia maambukizi kwa asilimia 98. Kuna mabishano mengi juu ya Kondomu. Wengine wanasema virusi vinapita. Wengine wanatoa ushahidi wa watu waliotumia Kondomu, wakapata maambukizi. Wengine wanasema kwamba Kondomu,ni biashara. Yako mabishano mengi. Nisingependa kujiingiza sana kwenye mabishano hayo. Labda moja tu kwa wale wanaosema kwamba Kondomu inachochea uzinzi. Ninakataa kukubaliana na watu hawa:

Kondomu ni silaha. Na kawaida mtu kuwa na silaha, si kigezo cha kuitumia hiyo silaha vibaya. Benki zetu masaa yote zinalindwa na mapolisi wenye bunduki zenye risasi. Ni mara ngapi mapolisi hawa wanafyatua risasi ovyo? Zinatumika pale yanapotokea majambazi.Yapo mambo mengi yanayochochea uzinzi:
Pombe,
Madawa ya kulevya.
Mavazi yasiyokuwa ya heshima,
Picha za ngono katika Internet,
Umaskini,
Ujinga nk.

Hadi leo hii jamii yetu haijafanikiwa kuwa na mfumo mzuri wa kupambana na hayo niliyoyataja. Baadhi ya waandishi wameandika makala, riwaya, michezo ya kuiigiza na mashairi kuonyesha kwamba niliyoyataja hapo juu yanachochea uzinzi. Mkipata nafasi mnaweza kujisomea vitabu kama:
Kisiki Kikavu- Dkt.Aldin Mutembei.
Ua la Faraja- William Mkufya
Mpe Maneno Yake- Freddy Macha.

Kwanini kanisa linapiga vita matumizi ya Kondomu?

Kwenye karne ya tatu kanisa lilishambuliwa na falsafa ya Kigriki. Falsafa ya akina Aristotle na Plato. Hawa walianzisha mfumo wa kufikiri uliokuwa unatenga vitu vyote katika makundi mawili:
Matter
Spirit.

Matter, ni vitu vyote vinavyokufa kama mwili. Na spirit ni vitu vyote vinavyodumu kama roho. Kwa maoni yao vitu vinavyokufa (Matter) vilikuwa vitu vichafu, dhambi nk. Lakini vile vinavyodumu (Spirit) vilikuwa vitakatifu.

Falsafa hii iliuchukulia mwili na matendo yote ya mwili kama ngono kuwa ni machafu, ni dhambi. Mtu aliyetaka kuishi maisha ya kitakatifu, ilibidi aachane na matendo ya mwili.

Hata kwa watu wenye ndoa, ngono iliruhusiwa pale ilipokuwa inalenga kutunga mimba. Ili kushika utakatifu, watu walishauriwa kufanya tendo hilo bila kulifurahia.

Watu kama Pliny, walifikia hatua ya kuisifia tembo, maana ilikuwa ikiingia kwenye joto mara moja baada ya miaka miwili. Origen, aliamua kujihasi ili asifanye ngono na Plotinus, aliishi maisha yake yote akiona aibu kuwa na mwili.

Lakini mtu aliyeingiza chuki ya furaha ya tendo la ngono katika kanisa ni Mtakatifu Augustine (430). Huyu aliunganisha dhambi ya asili na furaha ya tendo la ngono. Alisisitiza kwamba ni lazima mbegu za uzazi zidondoke kwenye sehemu yake na ziwe zinalenga kutunga mimba. Mafundiso haya yaliwageuza wanawake kama vyombo vya uzazi – yaliwanyima haki ya kufurahia tendo la ngono na kuwa na haki sawa katika jamii. Mafundisho ya kanisa juu ya ndoa hadi leo hii yanafuata mafunfisho ya Mtakatifu Augustine.

Mwandishi Uta Ranke- Heinemann, wa Ujerumani katika kitabu chake cha Eunuchs For The Kingdom of Heaven, anatwambia kwamba Mtakatifu Thomas Aquinas, alifikiri kwamba kumwaga mbegu za kiuume kwenye nafasi tofauti ni dhambi kubwa kuliko mtu kufanya ngono na mama yake mzazi!

Msingi huu ndio unalifanya kanisa kupinga matumizi ya Kondomu, maana ukitumia kondomu, mbegu zinamwagika kwenye mpira na zinakuwa hazilengi kutunga mimba.

Enzi tulizomo hakuna mtu ambaye bado anaamini kwamba kila tendo la ngono ni lazima lilenge kutunga mimba. Hata Kanisa lo limepiga hatua na kuongeza kwamba mbali na kutunga mimba, tendo la ndoa ni muhimu katika kuimarisha na kuchochea mapenzi katika ndoa. Ila kwa vile kanisa linapinga uzazi wa mpango, linaendelea kupinga matumizi ya Kondomu.

Hoja na chamgamoto iliyombele yetu na mbele ya kanisa, ni kwamba hatuongelei juu ya kudondosha mbegu kwenye mpira au kufanya uzazi wa mpango. Tunaongelea juu ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya UKIMWI. Ugonjwa ambao umepoteza mamilioni ya watu. Hivyo tunaongea juu ya kuulinda uhai.

HITIMISHO:

Kwa kuhitimisha, ningeomba kusema hivi: Ukiniuliza swali la haraka juu ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwenye kongamano au semina. Jibu langu litakuwa kwamba kinga ya kwanza ni Uaminifu, na kinga ya pili ambayo inaaminika zaidi ni Kondomu. Lakini ukiniuliza swali hilo hilo tukiwa tumekaa na kujadiliana kama tunavyofanya leo, kwenye jumuiya ya waumini, jibu langu litakuwa tofauti.

Nitakujibu hivi: Kinga pekee ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI, ni kubadilisha mfumo wa jumuiya zetu za kikristu, ni kubadilisha mfumo wa familia zetu ni mtu binafsi kubadilisha mfumo wake wa maisha.

Njia pekee ya kukinga maambukizi ya virusi vya Ukimwi, magonjwa mengine ya hatari na kukinga majanga mengine kama umasikini, ujinga, vita na upweke, ni kujenga jumuiya zinazoishi Utatu: Mungu Baba, Mungu Mwana Na Mungu Roho Mtakatifu. Ni kujenga familia zinazoishi utatu. Ni kila mtu kuishi maisha ya Utatu.

Kinga pekee ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI, ni kujenga jumuiya zinazojaliana, zinazojuliana hali, zinazochungana, zinazolindana na zinazowajibishana.

Jumuiya za Kikristu tulizonazo sasa hivi, familia za kikristu tulizonazo sasa hivi, ambazo zinatishiwa na ugonjwa wa Ukimwi na hatari nyinginezo, ni zile ambazo kila mtu yuko kivyake.Hakuna anayemchunga mwenzake, hakuna anayemlinda mwenzake na hakuna anayemwajibisha mwenzake. Kila mtu amejifungia katika nafsi yake:

Hakuna uwazi katika familia,
Hakuna kufunuliana katika familia,
Hakuna kushirikishana katika familia,
Hakuna kuchukuliana katika familia,
Hakuna kulindana na kuchungana katika familia.

Hivyo hivyo hakuna uwazi katika jumuiya zetu,
Hakuna kufunuliana katika jumuiya zetu,
Hakuna kushirikishana katika jumuiya zetu,
Hakuna kuchukuliana katika jumuiya zetu,
Hakuna kulindana na kuchungana katika jumuiya zetu.

Kila mtu anaufunga moyo wake na kubaki na siri nyingi ndani ya nafsi yake. Hata na mambo ya kawaida kama vile kupenda yanafanywa siri. Mambo kama tamaa, uchu, furaha,uzuni nk, yanabaki siri ndani ya moyo wa mtu. Kuna waandishi wengi, mfano kama Elieshi Lema (Parched Earth) wameandika juu ya ya tabia hii ya mtu kujifunga ndani ya nafsi yake. Mkipata nafasi mnaweza kujisomea vitabu hivyo kikiwemo cha “Parched Earth”. Mtu anayeufunga moyo wake hawezi kufanikiwa kutengeneza familia ya kuishi Utatu. Na kama hakuna familia za kutengeneza utatu, ni vigumu kuwa na Jumuiya zenye kuishi utatu.

Bila kuwa na Jumuiya zenye kuishi utatu, ni lazima tuandamwe na majanga mengi. Si Ukimwi peke yake. Leo tunaongelea UKIMWI, lakini kesho na keshokutwa yatakuja majanga mengine katika jamii yetu. Ni lazima tuwe na mfumo imara na wa kudumu kuweza kuyakabili majanga yanayoweza kutukumba kimwili na kiroho.


Bwana wetu Yesu anasema hivi:

“Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma” ( Yohana 17: 21.

Maneno haya ya Yesu, yanaeleweka vizuri ukiyaunganisha na yale ya Yohana 5: 19-20.

“Kweli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya baba, Mwana hukifanya vile vle. Baba ampenda Mwana, na humwonyesha kila kitu anachokifanya yeye mwenyewe,tena atamwonyesha mambo makuu kuliko haya, nanyi mtastaajabu”.

Yesu, alikuwa akielezea uhusiano wake na Mungu Baba. Jinsi yalivyo maisha ya uwazi. Hakuna siri kati yao. Analolijua Mungu Baba, analijua Mungu Mwana, na analijua Mungu roho mtakatifu. Hii ndiyo maana ya Mwana kuwa ndani ya Baba na Baba kuwa ndani ya Mwana na wote wawili kuwa ndani ya Roho Mtakatifu. Wanaishi maisha ya utatu, katika uwazi na kufunuliana. Uwazi huu unawafanya waungane na kuwa kitu kimoja.Yesu, anatuombea na sisi kuishi maisha ya Utatu. Kuishi maisha ya uwazi. Tuwe ndani ya Yesu, nay eye awe ndani yetu na sote tuwe ndani ya Baba. Tuwe na familia zenye kuishi utatu. Baba ndani ya familia amjue mama, na mama amjue Baba. Baba ajifunue kwa mama, na mama ajifunue kwa Baba. Hata kama baba anavutiwa na mwanamke mwingine, au mama anavutiwa na mwanaume mwingine, wafunuliane! Kwa njia hii wanaweza kulindana, kuchungana, kuchukuliana na kusaidiana. Ni katika uwazi na kufunuliana familia inaweza kuungana na kuwa kitu kimoja.

Baba na mama wakichukuliana, wakafunuliana, wakalindana na kuchungana, wanajenga mfumo wa kuwalinda na kuwachunga watoto wao. Watoto watakua katika uwazi na kutembea katika mwanga. Watafundishwa maadili mema bila ya matatizo na kuwa sehemu ya familia inayoishi utatu.

Familia zilizoungana na kuwa kitu kimoja, zinatengeneza jumuiya iliyoungana na kuwa kitu kimoja. Jumuiya ikiungana na kuwa kitu kimoja, ni lazima pawepo kufunuliana, kujaliana, kulindana, kuchungana na kusaidiana.

Jumuiya inayoishi Utatu, ndiyo inayoweza kupambana na majanga makubwa kama UKIMWI. Kwa ufafanuzi zaidi juu ya Jumuiya inayoishi Utatu mnaweza kujisomea kitabu cha Marehemu Askofu Christopher Mwoleka: “The Church as a Family”

Yote niliyoyasema yanawezekana pale tu ambapo kila mmoja wetu, kila mwanausharika na kila mtanzania, atasali sala kama ile ya Bwana Sufi Bayazid:

“Nilipokuwa kijana mwanamapinduzi, sala yangu pekee kwa Mungu ilikuwa: ‘Mungu, nipatie nguvu na uwezo wa kuubadilisha ulimwengu’

“Nilipofikisha umri wa mtu mzima na kugundua kwamba sijafanikiwa kuibadilisha roho hata moja, nilibadilisha sala: ‘Mungu, nipatie nguvu na uwezo wa kuwabadilisha watu wanaonizunguka, familia yangu na marafiki zangu’

“Sasa ninapozeeka, bila kufanikiwa kuubadilisha ulimwengu sala yangu imekuwa: ‘Mungu, nipatie nguvu na uwezo wa kujibadilisha mimi mwenyewe’

“Kumbe ningesali hivi tangia mwanzo, nisingepoteza muda wangu bure” (The Song of the Bird – uk 153 – tafsiri ni yangu).

Kama anavyosema Sufi Bayazid, tusiweke nguvu nyingi katika kutaka kuyabadilisha maisha ya wengine, kabla ya kubadilisha maisha yetu sisi wenyewe. Hivyo basi kinga pekee ya kusambaa kwa virusi vya Ukimwi, ni kila mmoja wetu kubadilisha maisha yake mwenyewe. Ni kila mmoja wetu kujinyoshea kidole. Kwa njia hii tunaweza kuulinda na kuutetea uhai!

Kristu yu hai, jana, leo, kesho na hata Milele.

Asante sana kunisikiliza.

Na,
Padri Privatus Karugendo
e-mail:pkarugendo@yahoo.com
Marejeo:

Agano jipya – injili ya Yohana.
Kisiki Kikavu- Dkt Aldin Mutembei
Ua la Faraja- W-Mkufya
The Song of the Bird – Anthony de Mello
AIDS-Petit Echo- Fr.Bernard Joinet.
Eunuchs For The Kingdom of Heaven,1991.- Uta Ranke-Heinemann
HIV/AIDS Challenges for Professionals- Fr.Privatus Karugendo, 2002
The Church as a Family- Late Bishop Christopher Mwoleka.
Mpe Maneno Yake- Freddy Macha.
Parched Earth – Elieshi Lema.

Natia jembe Mpini

Nimekuwa kimya muda mrefu na niliondoka bila kuaga. Sasa narejea, nasema natia jembe mpini nirudie kazi yangu. Naendlea na kublog sasa. Samahani kwa kupotea bila taarifa

Saturday, July 29, 2006

Makala ya Karugendo Kumuaga Chachage

Padre Karugendo kaandika makala kuhusu prof. Chachage. Yeye anasema anamlaumu sana Chachage. Ni muhimu uisome ujue anamlaumu kwa nini. Naibandika hapa

Wednesday, July 19, 2006

Tenzi za Kumuaga Prof. Chachage

Prof Shivji na Jenerali Ulimwengu waliandika tenzi za kumuaga Prof. Chachage. Unaweza kusoma wa Shivji kwa kubonyeza hapa na wa Ulimwengu kwa kubonyeza hapa

Monday, July 17, 2006

Buriani Prof. Chachage

Mengi yameshaandikwa na kusemwa kuhusu Marehemu Prof. Chachage aliyetutoka hivi karibuni. Mwanazuoni huyu ambaye hakuendekeza kabisa uvivu wa kufikiri ametutoka katika kipindi ambacho kwa vyovyote watu walikuwa wakitaraji mengi toka kwake. Lakini hata hivyo katuachia mengi ya kusoma. Siku za nyuma niliuliza ni wangapi walikuwa wamesoma Makuhadi wa Soko Huria. Kitabu alichoandika Prof. Chachage mwaka 2002. Ukikisoma pamoja na vitabu vyake vingine kama Sudi ya Yohana na Almasi ya Bandia ndipo utamwelewa msimamo wake na uwezo wake wa kufikiri. Jenerali Ulimwengu na Issa Shivji wameandika tenzi kwa ajili ya kumbukumbu ya Chachage. Nitaziweka hapa ili wengi wazisome.

Tuesday, May 16, 2006

Mkataba wa IPTL na sheria ya Takrima imetufunza nini?

Kwa wiki kadhaa sasa tumekuwa tukijadili na kufurahia sana kufutwa kwa sheria ya Takrima na Ile ya kumzuia mgombea binafsi. Lakini kuna uwezekano wa hawa jamaa wakarudi mahakama ya rufaa kukatia rufaa rushwa. Pia tumeisoma taarifa jinsi tulivyoingizwa pabaya na Wamalasia na Watanzania wenye uroho wa pesa kwenye mkataba wa IPTL. Inabidi katika mviringo wetu wa Blogu pamoja na kwenye magazeti tuanze kujadili kwa kina kabisa baadhi ya wahusika ili jamii iwajue. Kwa mfano; Andrew Chenge, aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Serikali ametajwa kama mhusika mkubwa sana kwenye IPTL. Alihusika kwa mambo mawili; kwanza kama mwanasheria mkuu wa Serikali ofisi yake inahusika na kutoa ushauri kwa serikali kwa mambo yote ya kisheria; lakini la pili ni kwamba alikuwa kikwazo katika kutoa pingamizi la kukamatwa kwa Rwegamarila ashitakiwe kwa rushwa kwa kudai hakuna ushaidi.
Hakuna ubishi kwamba Chenge na ofisi yake ni mhusika na Mhandisi wa Sheria ya Takrima. Alikuwa anaitetea kweli. Wakati mwingine alikuwa akiwatukana wabunge waliokuwa wakihoji hiyo sheria. Ni kweli kwamba sheria hiyo imemsaidia kuingia tena bungeni sasa. Jamani mtu huyu tena kapewa wizara ya Afrika mashariki. Hii ni wizara ambayo inahitaji umakini mno. Tunaongelea ushirikiano na baadaye shirikisho. Katika kipindi cha Mpito kutakuwa na makumi ya mikataba. Chenge anaweza kuisimamia?
Chenge na ofisi yake pia wanahusika na mikataba yote mibovu ambayo sasa Serikali inakiri kwamba itarekjelewa upya. Sasa sijuhi kama atatuvusha katika jahazi hili la ushirikiano wa Afrika Mashariki. Ni lazima mambo haya yavaliwe njuga.

Sunday, May 14, 2006

Kina Galileo wasingehoji tungekuwa wapi?

Ndani ya blogu hii kuna habari ya Askofu kuzaa mtoto na kujificha. Hoja hiyo imejadiliwa sana. Baadhi ya watoa maoni wanaonyesha ni jinsi gani wanavyotaka mawazo mgando yaendelee. Hasa yale yahusuyo imani. Hivi kama kina Galileo wa Galileo hawakuhoji baadhi ya mambo bado leo tungeambiwa dunia ni mstatili na jua linazunguka toka mashariki kwenda magharibi? Kama hawakubali adhabu ya kifo kwaa kuhoji leo tungekuwa wapi? Nimeamua kuweka hapa chini maoni ya mmoja wa wachangiajia ambaye hataki watu wahoji uhalali wa papa anayeongoza watu zaidi ya bilioni moja kuchaguliwa na wazee wanaume wasiozidi mia moja. soma sehemu ya maoni hayo hapa chini.
"Nakumbuka uliwahi kuandika katika gazeti la Rai ukihoji uhalali wa uchaguzi wa Baba Mtakatifu anaye chaguliwa na Makardinali na kuongoza kanisa zima! Wewe ni Padri mkatoriki unaye hoji uhalari wa Baba Mtakatifu?! Zaidi umehoji ukweli wa mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu utumiaji wa Kondomu. Kama "Padri" wa kwanza mkatoriki umeunga mkono matumizi ya Kondomu, kama kinga dhidi ya Gonjwa hatari la Ukimwi.Haya yote yamekupatia sifa katika ulimwengu unaopinga msimamo wa Kanisa katoliki katika masulala mbalimbali yanayo husu maadili"
Mambo sasa yameanza kubadilika. Huko Uchina wamebariki maaskofu katoliki bila mkono wa Vatican. Wametolewa macho lakini wachina wameendelea. Huko Marekani wamemkabidhi uaskofu mtu aliyeoa. Sasa hapo ndipo utaona watu wameanza kuhoji na kutekeleza mambo ambayo awali yalikuwa mwiko kuyahoji. Miaka ya sitini Mwanaharakati Malcom X, katika moja ya hotuba zake alisifia sana Uchina kwa kuwa nchi ambayo ilikuwa ikifanya maamuzai yake mengi bila kuwasikiliza mabwana wa magharibi na mavyombo yao yanayoitwa UN, Benki ya Dunia, IMF nakadhalika. Alibashiri kwamba China ingeendelea sana. Sote tunaona yanayotokea China. Sasa wameanza kuchoka na kutawaliwa na Vatican. Baada ya kukubali dini za kigeni kwa mbinde sana sasa wameanza kujichukulia maamuzi yao wenyewe. Wacha watu wahoji. Kama watu wasingehoji basi tungekuwa mbali sana.

Friday, April 21, 2006

Ripoti ya Transparency International kuhusu IPTL na Tanesco

Nimepata kupitia barua pepe yangu taarifa iliyotolewa na transparency international kuhusu lile dude la Tegeta linalogharimu serikali shilingi bilioni tatu kila mwezi (hapa ni wakati ambapo halijawashwa) Likianza kutoa umeme tuu unalipa bilioni tatu za kila mwezi na kulipia umeme watakaokuuzia. unaweza kuisoma hapa

Thursday, April 13, 2006

Urasimu Mpaka lini?

Kuna Mtanzania mmoja anayeishi nchini Marekani ameandika maoni kwenye blogu yangu jinsi urasimu ulivyo kwenye pasipoti mpya. Nachapisha maoni yake hapa chini. Je na wengine mmepata matatizo kama haya? Lazima nikiri kwamba mimi binafsi sikupata tatizo lolote lakini sipo Marekani. Nipo Kusini.

Urasimu mpaka marekani!! Mimi ni mgeni kwenye blog yetu hii na ni mtanzania ninayeishi marekani.Kuna jambo moja linalosumbua vichwa sana hasa kwa tuliopo huku,jambo hili ni urasimu ulikithiri kwenye ubalozi wetu wa huku.Ni swala la passport mpya ambazo tumelipishwa fedha nyingi kwa kufanya process ya kubadilisha,kuna state tumelipa karibu dollar 95(laki na upuuzi kwa fedha zetu za madafu).Toka mwezi wa sita/saba 2005 kwa malengo ya kutumiwa kwenye address zetu by sept/octoba 2005.Cha kushangaza sana ni kuwa huyu ndugu wa marehemu Sokoine alitumia nafasi hii kujitengenezea fedha kisha kuingia mitini.Kama tulilipa ghalama zote ili passport zetu zitumwe kwenye makazi yetu,inakuaje tena tunatakiwa tuzifuate washington?Waliojaribu kwenda DC walitakiwa kutoa hongo ili kupata passport zao.This is bullshit wewe bwana sokoine,tambua kuwa fedha zile watu hawakuziokota bali ni kuzifanyia kazi.Keep in your freak-ass mind,next time unakuja Kansas,tegemea kukabiliana na bakora za maana.Acha kuharibu jina la marehemu wewe,na kama ulihitaji fedha ungesema mapema tukatafuta njia ya kukusaidia.

Tuesday, April 04, 2006

Askofu akumbushwa Mwanae

Mwenye kumwandikia baruapepe hii Askofu Severini ameniambia niiweke kwenye blogu ili watu wengine wasome kwamba "Baba Askofu" ana mtoto huko Arusha.

Date:
Wed, 15 Feb 2006 02:00:45 -0800 (PST)
From:
"Antiparth Martin"
Subject:
Mkunde!
To:
niwemugizi@iwayafrica.com
CC:
nunzio@cats-net.com, nyumba@cats-net.com, tec@cats-net.com
HTML Attachment [ Download File Save to Yahoo! Briefcase ]

Mtumishi wa Mungu, Askofu Severine Niwemugizi, Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.
Tumsifu Yesu Kristu.

Mtumishi wa Mungu,
Pole sana kwa kazi nyingi ya kuchunga kondoo. Bwana akubariki na kukuzidishia moyo mkuu. Ninakuandikia ujumbe huu kukumbusha jambo moja:

Unakumbuka siku chache kabla ya kuchaguliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge, ulizaa mtoto na Consolata Kyala, dada yake na Padri..... wa Jimbo Kuu la Dar-es-salaam. Padri huyo alikutunzia siri, na sisi tukanyamaza! Mtoto wako Mkunde, anaendelea kukua na sasa anasoma shule Maji ya Chai Arusha.

Ili Consolata Kyala, akae kimya, ulimjengea nyumba kule Maji ya Chai Arusha. Sasa hivi anaishi kwenye nyumba hiyo na mme wake Antiparth Martin. Hapo hapo anaendesha biashara ya Bar ijulikanayo kwa jina la Holiday Inn.

Tumesikia tetesi kwamba hivi karibuni utateuliewa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora. Tunafikiri ni jambo la muhimu na la lazima, viongozi wa Kanisa kufahamu kwamba wewe una mtoto. Ofisi ya Askofu Mkuu ni kubwa na yenye kudai maadili ya Kanisa Katoliki.

Viongozi wa kanisa wanaweza kupuuzia jambo hili. Nawe pia unaweza kupuuzia jambo hili. Kwa vile siku hizi sayansi imepiga hatua, tutasisitiza ipimwe DNA yako na ya mtoto Mkunde. Tunataka watanzania wajue ukweli huu na ulimwengu ujue ukweli huu.

Ni matumwaini yetu kwamba utaupokea ujumbe huu na kuwajibika ipasavyo.
Tunakutakia moyo mkuu.

Kwa niaba ya waumini wenye upendo na kanisa katoliki wa Maji Chai-Arusha.
Ni, wako katika Upendo wa Kristu.
Antiparth Martin.

Tuesday, March 14, 2006

Mawaziri wetu

Niliposoma habari kwamba mawaziri wanalala Hotelini kwenye Blogu ya Da Mija nilitoa maoni kwamba sikushangaa kwa hilo. Sababu ya kusema hivyo ni kwamba nilitarajia. Kwa nini nisingetarajia kwa sababu nyumba zote ziliuzwa? Wakati nashangaa hilo nakutana na habari kwamba mmoja wa naibu waziri ambaye alikuwa akifanya kazi nchini Botswana kama mwalimu kwenye chuo kimoja cha kilimo na kujifanya anaumwa sana kumbe wlikwenda kwenye kampeni. Alikuwa akilipwa mshahara huku akiwa anapiga kampeni. Nimeikuta hii habari kwenye barua pepe yangu labda wengine mmeisoma lakini niiweke muione. Hii ni kashfa ya hali ya juu sana. Kingine ni kwamba huyu jamaa kuna watu wanahoji shahada yake ya PHD kaipata wapi? Kwenye maelezo yake binafsi katika tovuti ya bunge anadai Free State University. Kuna watu wamejaribu kuitafuta hii University ilipo lakini haijaonekana. Soma habari hii hapa chini:


Tanzanian minister on Botswana's payroll?
by Sarah Mophonkolo
2/14/2006 7:39:04 AM (GMT +2)
A Tanzania deputy minister may still be drawing a salary from Botswana
government almost eight months after he returned to his native country.
Authorities were this week sent in to a frenzy at the shock revelation
that Dr. David Mathayo David (37) who was employed as a lecturer in
agriculture at the Serowe College of Education, was in fact paid to
fund
his political campaigns last year. !

College Principal Caiphus Dema said they did not know that David was
involved in politics. "What we know is that he went on a three week
sick
leave last year in June. He said he wanted to be close to his family.
When the leave was over he applied for an extension a number of times
saying he was still very sick," Dema said.
A reliable source has alleged that David is still on government!
payroll. "He is still getting paid as he is still considered an
employee
of the college," she said. Nevertheless, Dema said he doubted that
David
was still getting paid. "He said he was considering resigning as he was
too sick to work," Dema said. He said when he did not return, they went
to his house sometime last year to reclaim the school furniture. "It
did
not appear as if he had left any of his belongings," Dema s! aid.

David became a Member of Parliament for Same Magharibi (West)
constituency under the ruling party, Chama Cha Mapinduzi ticket after
the October parliamentary elections. He was subsequently appointed
Deputy Minister of Industry, Trade and Marketing December 28 last year.
Approached for comment, the Teacher Service Management (TSM) referred
us to the Department of Teacher Training and Development. The Deputy
Director, Tebogo Mongatane, requested a questionnaire last week saying
she feared being misquoted. She had promised to answer the
questionnaire
as soon as it was sent. Nevertheless, a follow-up on Friday afternoon
found she had 'other important obligations.'

On Monday afternoon she sent a res! ponse advising us to "direct
these
questions to TSM, who are employer and are responsible for all
employment matters affecting teachers." Efforts to reach David for
comment proved futile.
_______________________________________________________

Comments za watu wa karibu na mweshimiwa:
Hii habari inatia woga kidogo. Ukiisoma inaonyesha Naibu Waziri sio
mkweli.

Alimdanganya mwajiri wake kuwa anaumwa kumbe yuko kwenye harakati zake
za kisiasa. Hapa kidogo panatia shaka kama hatamdanganya Mheshimiwa
Rais
kwenye wadhifa wake mpya alionao mradi mambo yamwendee.

Huyu jamaa kuna sehemu nyingine wanamjadili pia, wanasema elimu yake
iliyoonyeshwa kwenye website ya bunge sio kweli. Naanza kuamini kuwa
hata kwenye sifa zake ametia chumvi kama style yake ndio hii. Nanukuu
"Mh. Mathayo David Mathayo (naibu waziri wa biashara na viwanda),
alisoma SUA degree ya wanyama (Ba! chelor Vet. Medicine) kati ya
1992-1997 na tulikuwa tunakaa naye Hall moja pale na nilimwacha pale,
na
baaada ya hapo alifanya kazi kidogo Botswana na akarudi nyumbani
kujiunga na! NEC ya CCM (kutokea kundi la vijana), sasa cha kushangaza
hivi sasa ana PhD ambayo haijulikani kaipatia wapi na lini, mwanzo
nilifikiri wanamwita Dr . kutokana na field yake wanyama kumbe
nilipopitia CVs za wabunge, nimegundua naye kapata PhD from Free State
University(kwa kifupi hii university haipo ni feki-jaribuni ku-google
wenyewe). Tena kwa kifupi hana hata Masters degree jamani, sishangai
kupewa wizara nyeti bali kinachoikumba Kenya kipo njiani kuja Tanzania,
hii ndiyo ! labda kasi ya kundi la vijana katika kujiingiza kwenye
siasa
kwa mbwembwe za kwamba waonekane wasomi haswa"
___________________________________________________________
mmmmh!, mambo ya bongo hayo!

Monday, March 06, 2006

Kuadi wa soko huria atoswa

Waziri Mkuu wa Libya bwana Shukri Ghanem ametemwa kazi yake japokuwa alikuwa akipata umaarufu mkubwa toka sekta binafsi. Kamati inayoshughulika na sera za Serikali inasemekena kutopenda mageuzi makubwa aliyotaka kuyafanya ya kuuza kila kitu. Soma habari hiyo hapa

Thursday, February 16, 2006

Afrika haitaji msaada wa Chakula

BBC iliendesha mdahalo mzuri sana kati ya Nicholas Crawford toka WFP na Tajudeen Abdul-Rahem Wa Justice Afrika kuhusu chakula barani Afrika. Jamaa wa Justice Afrika anadai kwamba hakuna haja ya Afrika kupewa msaada wa chakula na anajaribu kuelezea kiini cha tatizo la njaa barani Afrika na jinsi misaada inavyolemaza bara hili. Mzungu wa WFP anatetea umuhimu wa msaada wa chakula. Kwa kweli nakusihi usome mdahalo huo hapa. Ni mdahalo mzuri mno.

Kuua Mwenzi wako ni upendo?

Nchi ya Botswana imekumbwa na ongezeko la mauaji yanayotokana na wanaume kuwaua wapenzi wao. Mwaka 2005 peke yake inasemekana kulitokea vifo sabini. Wenyewe siku hizi wanaita "Passion Killings". Botswana ni nchi ndogo- si kwa ukubwa wa eneo bali kwa idadi ya watu. Ina watu wapatao milioni moja na laki sita tuu. Halafu maambukizi ya Ukimwi ni ya kutisha. Takwimu zinaonyesha kwamba ni asilimia 40 ya watu wazima walioambukizwa. hapohapo kuna ongezeko kubwa la vifo kutokana na ajali nyingi shauri ya uendeshaji mbovu hasa kutokana na kunywa pombe kupindukia. Sasa haya mauaji ya kina dada tena inaongezea idadi ya vyanzo vikuu vya vifo yaani UKIMWI na Ajali. Ni hatari. Wanaume hawa mara nyingi wakishaua nao hujiua kwa vile wanajua watakuja kuhukumiwa adhabu ya kifo. Soma habari hiyo hapa

Wednesday, February 15, 2006

Naanza safari ya kuhama

Nimeanza kuhamia kwenye wordpress. Siku tatu zilizopita nilikuwa nashindwa kabisa kuingia kwenye blogger.com ili niweze kuandika mambo kwenye blogu. Pamoja na hayo nimepokea ushauri wa Ndesanjo kuwa wordpress inaendana na mabadiliko mapya yanayotokea kila mara. Unaweza kunisoma kwa kubonyeza hapa. Nitaendelea kuweka viungo vya blogu na mambo mengine taratibu.

Maisha yetu baada ya Miaka 50

Kwa wale wasomaji wa makala za Padre Karugendo, naweka makala yake moja ambayo aliiandika kama changamoto kwa waliofikisha umri wa miaka 50 mwaka huu. Yeye ni mmojawapo wa hao waliofikisha umri huo. Unaweza kuisoma kwa kubonyeza hapa

NEPAD ubeberu mpya

Kuna mjadala sasa kwamba hili dude linaloitwa NEPAD ni aina mpya ya ubeberu ambapo Afrika ya Kusini inatumia kupeleka mitaji katika nchi nyingine za Afrika. Kuna bwana mmoja kaandika kitabu juu ya hili. Lakini hata kusingekuwa na hicho kitabu hili ni jambo la wazi kabisa. Ukiangalia changamoto wanazokabiliana nazo hawa jamaa wa Afrika ya kusini utagundua kwamba ni ukweli mtupu. Baada ya ule mfumo wa kibaguzi kwisha mwaka 1994 ilibidi watafute nafasi ya kuwakuza kiuchumi weusi. Njia rahisi ilikuwa ni kuwatafutia weupe nchi za kupeleka mitaji yao ili nafasi ibaki nchini mwao kuwasaidia weusi. Nchi nyingi za kiafrika zimeingia kwenye makubaliaono hayo bila kuona janja ya hawa jamaa. Tatizo ni kwamba biashara inakuwa ya upande mmoja. Nchi nyingi sana hazina mtaji wa kuwekeza Afrika ya kusini. Kwa hivyo tutawasidia kupunguza matatizo yao huku hizo sera zikiwa hazisaidii sana nchi zingine. Wanapotoka kwenda nje hawana mpango wowote wa kuendeleza nchi wanazowekeza. lao ni kupata faida na kuondoka. Ubeberu huu mpya sijuhi utatufikisha wapi.

Gregory yuko wapi?

Nilikutana na binti mmoja ambaye tulikuwa wote Jeshi la Kujenga Taifa (Ndesanjo huliita la kubomoa taifa) akaniuliza: Hivi Gregory yuko wapi siku hizi? Nikamuuliza Gregory gani? Akanishangaa akasema kumbe urafiki wenu uliishia jeshini? Nikamuuliza jina lake la pili ni nani? Akaniambia Macha. Ohh!! Nikamwambia nimemkumbuka sasa. Nikamwambia kwamba Macha alirudisha jina lake la Gregory kwa Mchungaji wake kama mmoja wa wahusika katika kitabu cha Pambazuko Gizani alivyotaka kurudisha jina lake la Paulo kwa Padre. Binti wa watu hoi. Nakumbuka Macha alipokuwa kwenye jitihada za kurudisha jina lake alikuwa akinishambulia kila siku nirudishe la kwangu pia ikiwa ni ishara ya ukombozi mpya. Kabla ya kurudisha jina lake Ndesanjo alikuwa akiitwa Gregory!!!

Ilikuwa lazima Yesu afe?

Rafiki yangu mmoja ameniacha hoi aliponiuliza kwamba; hivi Mungu alikosa njia nyingine ya kumkomboa mwanadamu mpaka amtume Mwanae wa pekee afe kwa ajili ya dhambi zetu? Kulikuwa na ulazima wa damu kumwagika? Huyu jamaa yangu yeye si mfuasi wa dini za kuja kwa hivyo nikaona kwamba pengine anauliza mambo hayo kwa ajili hiyo. Baadaye nikaingia kwenye mjadala mwingine na jamaa mmoja mfuasi mzuri wa madhehebu ya kikristo. katika maongezi yake akasema angekuwa rais wa dunia angewaua watu wa jinsia moja wanaotaka kuooana. Jamaa akambana hivi wakristo mnaua? Nikapata jibu langu la awali la kwa nini Yesu afe? Jamaa alisema ndio maana Mungu alimtuma Yesu aje afe kutoa ishara kwamba hakuna ukombozi pasipo kumwaga damu!!

Thursday, February 09, 2006

umeshasoma Makuhadi wa soko Huria?

Kama hujakisoma basi umekosa mengi. Nilikisoma mara ya mwanzo mwaka 2003 nikakirudia 2004 nimemaliza kukirudia tena mwaka huu. Chachage si mchezo. Ameandika. Ni riwaya yenye matukio yanayoendana na hali halisi ya Tanzania. Ukikisoma huwezi kushangaa kwa nini Chinua Achebe alikimbia nchi baada ya kitabu chake cha A man of the people. Alimaliza kitabu chake kwa kuonyesha kwamba jeshi limepindua nchi. Na ikapinduliwa baada ya muda mfupi. Wengi walidhani alihusika. Lakini wapi mwenyewe anasema ni kule kuisoma jamii na kuielewa. Chachage ndivyo alivyoielewa jamii ya Tanzania. Amegusa kila eneo; usanii wa wabunge; rushwa mahakamani; waandishi wa habari kuingizwa mtegoni; na mengineyo. Kitabu kina historia nzuri sana. Kuna michapo ambayo hutajutia wala kitabu hakitakuwa kirefu kukisoma. Mchapo wa mzungu kala fenesi kwa mfano au wa padre huko Musoma ambaye aliamua kumpa mtoto shilingi mia na mama shilingi 20! Soma tafadhali. Utakutana na jinsi Salama mke wa Mjuba alivyoamua kumpa mwanae jina la Mchungaji anayeombea vita huko Marekani baada ya kuokoka. Kitabu kimekamilika. Ujuhadi unavyofanywa na watu wenye nyadhifa. Elimu waliyo nayo waze wetu nakadhalika ni mambo ambayo yamesheheni ndani ya kitabu Hicho. Soma Makuhadi wa Soko Huria ufaidi.

Wednesday, February 01, 2006

Mambo mengine! sijuhi tuanzie wapi

Mimi huwa ni kipofu wa dini. Inakuwa ngumu sana kwangu kumuuliza mtu dini yake au hata kuhisi kutokana na jina kwa sababu nimesoma na watu wenye majina ya kizungu ambayowengi huita ya kikristo lakini baadaye nikaambiwa ni waislamu wengine wenye majina ya kiarabu ambayo huitwa ya kiislamu baadaye naambiwa ni wakristo. Sasa huwa sichukulii jina kama kigezo kabisa. Sasa baada ya mawaziri kutajwa hapo Januari wengi wetu tulianza kujadili sifa zao. Lakini kuna jamaa wengine wameniacha hoi sana. Wanasema; wewe huoni Wizara nyeti zote kawapa waislamu? Angalia Fedha, Mambo ya nje akataja na Wizara nyingine lakini sikutilia maanani. Nikamuliza? Hivi Wizara kuwa nyeti maana yake ni nini? Au kwa mfano Kikwete alipokuwa Waziri wa mambo ya nchi za nje kwa miaka kumi ambayo ni moja ya wizara nyeti kutokana na hao wanaodai hivyo waislamu walifaidi nini? Nilishangaa nikagundua kwamba kuna safari ndefu. Baadhi ya takwimu zinaonyesha kwamba Tanzania ina asilimia 35 ya ambao si waislamu wala wakristo. Hawa watapewa wizara ipi? Na hizo takwimu za wakristo na waislamu pwngine zinafuata majina na nyingine ni za zamani. Kwa mfano kuna maelfu ya watanzani wenye majina ya kikrito na kiislamu(kama yapo) ambao hawako kwenye hizo dini au walishajiondokea na kujichukulia ustaarabu wao. Tukiendelea na huu uhayawani tutafika mahali kila dhehebu litake kuwa na waziri. Na kuna madhehebu karibu 400 ya kikristo tuu Tanzania. Sijuhi itakuwaje. Lakini hao ambao hawako kwenye hizi dini mbili nani atawawakilisha? Ndesanjo kaongelea kiapo kwa kutumia vitabu; kitukufu na kitakatifu. Suala linarudi niliyowahi kusema huko nyuma: elimu ya dini

Thursday, January 19, 2006

Tumepoteza maelfu ya miaka ya elimu

Hivi lile Sakata la kufukuzwa kwa madaktari limeishia wapi? Kama wote walifukuzwa basi ni kwamba taifa limepata hasara ya maelfu ya miaka iliyowekezwa kwenye elimu. Tunaambiwa kwamba, kila mwaka mmoja wa elimu mtu anaopata unaongeza ufanisi katika utendaji kazi ambao hutoa mchango katika ukuaji uchumi na kuongeza maslahi ya anayepata elimu hiyo. Kwa kifupi ni kwamba rasilimali watu ni mtaji mkubwa mno katika ukuaji wa uchumi. Kwa nchi yenye watu wachache wenye elimu ya chuo kikuu kama Tanzania, kufukuza madaktari 200 waliosoma kwa wastani wa miaka 19 kila mmoja ni hasara kweli. Ngoja niweke tarakimu rahisi kabisa. Chukua miaka 7 ya shule ya msingi, halafu ongeza 6 ya sekondari, kisha ongeza mitano ya shahada ya kwanza ya udaktari na mwisho ongeza mwaka 1 wa mafunzo ya vitendo (Internship) inakupa jumla 19 kwa kila mmoja. Sasa ukizidisha miaka 19 kwa watu 200 unapata miaka 3,800 (Elfu tatu na mianane). Kwa hivyo miaka yote hii imepotea. Wakiamua kwenda kufanya kazi nchi nyingine, nchi hizo zitafaidi sana hiyo miaka 3,800 ya elimu. Kwamba walikuwa na haki ya kugoma au la ni mjadala mwingine. Leo nimejadili idadi ya miaka ya elimu itakayopotea kwa kufukuza madaktari 200.

Vyama Viendeshwe na wanachama

Ule uchaguzi wa mwaka jana umetoa funzo gani kwa vyama vinavyoitwa vya upinzani?( Sipendi hili neno upinzani; tuviiteje? Shindani?). Kwanza kabisa ingebidi wajifunze kwamba ruzuku haiwasaidii bali inawamaliza. Unajua ruzuku ndio inayofanya kila chama kitake kuweka mgombe wake ili angalau kipate mbunge na hatimaye ruzuku? Sisemi kwamba kuna vyama ambavyo vinaweka wagombea kwa sababu nyingine nje ya ruzuku. Ukiangalia kiundani kabisa ruzuku haifaidishi upinzani bali chama twawala. Katika ruzuku ya shilingi bilioni nane kwa mwaka CCM itaondoka na zaidi ya bilioni saba halafu kitakachobaki jamaa watagawana. Turudi kwenye hali halisi; ukitoa CCM ni chama gani kingine kinaweza kujigamba kwamba ruzuku inasaidia katika kampeni au katika kuimarisha chama? Ni asilimia ngapi kwa mfano ya fedha za kukodi helkopta ya CHADEMA ilitokana na ruzuku?

Ukweli ni kwamba kwanza kabisa chama ni kikundi cha watu wenye mwelekeo unaofanana au wanakubaliana kiitikadi. Kama ni kikundi basi inabidi kiendeshwe na hao wanachama. Hakuna haja ya kila mtanzania kuendelea kuendesha vyama ambavyo ni vya watanzania wachache sana. Hivi ni asilimia ngapi ya watanzania ni wanachama wa vyama vya siasa? Hili tulivalie njuga ili hii ruzuku ifutwe. Sioni kama eti ruzuku inasaidia kukuza vyama na hatimaye demokrasia. Kwanza hili suala la kufikiria demokrasia ni vyama vingi sijuhi limetoka wapi. Hata kama pesa hizi kinadharia zina lengo la kuimarisha vyama basi kinachoimarika ni kimoja tuu. Hata kama vingeimarika vyote, viimarishwe na wanachama wenyewe. Wanaopenda vyama wavichangie.

Hivi vyama vya upinzani ingebidi vianze kuchimba masuala ya msingi ambayo yanafanya CCM kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha. Kwa mfano mali ambazo CCM ilirithi wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanza. Angalia viwanja vya mpira kibao bado ni vya CCM, majengo mengi ambayo yalijengwa kwa kodi za wananchi bado ni ya CCM. Kwa nini mali hizo ziendelee kubaki za CCM? Tume ya Nyalali ilipendekeza kwamba mali hizo zirudishwe Serikalini lakini mpaka leo hakuna kilichorudishwa. Halafu jamaa wa upinzani wanakaa kukimbilia ruzuku ambayo kila mwaka itaendelea kuongezeka kw CCM huku ikipungua kwao, huku Chama hiki twawala kikiendelea kufaidika na mapato ambayo ni mali ya kila mtanzania. Pamoja na mambo mengine ya katiba na tume huru ya uchaguzi mimi nimeongele mambo mawili yanayohusu pesa.

Hili la ruzuku wanablogu wote tulivalie njuga. Vyama viendeshwe na wanachama hizo hela za ruzuku zikabiliane na kipindupindu au shughuli nyingine za kimaendeleo.

Natamani Kipindupindu kifike Ikulu

Kuna mwanamuziki mmoja mtanzania, kati ya wale wanaoitwa wa kizazi kipya anatamani mambo ya kuchekesha sana katika moja ya nyimbo zake. Kwa mfano anatamani mlima Kilimanjaro uamie sijuhi wapi na bahari pia ihame. Mimi leo nakuwa kama yeye. Natamani Kipindupindu kilipuke Mikocheni, Osterbay, Masaki halafu kipige hodi Ikulu pia. Kila siku kinavamia Buguruni, Manzese na sehemu zingine za walalahoi. Hivi kweli tumeshindwa kabisa kudhibiti kipindupindu? Labda kikifika ikulu kitapatiwa ufumbuzi. Rais mpya kaanza kazi kwa kukaribishwa na mlipuko wa kipindupindu kama ilivyo kawaida ya kila mwaka. Sijuhi kama atakivalia njuga kwa Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu mpya au kitaendelea kumaliza watu kwa Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya? Kama waziri wa Afya ataendeleza mapambano ya magonjwa kwa warsha, semina na makongamano na kuchapisha fulana na kofia basi hakuna kitakachotokea. Safari hii Waziri wa Afya ni Profesa. Sijuhi kama atasadia lolote kwa sababu huko nyuma alishawahi kuwepo Profesa akaboronga pia. Mimi sijuhi aibu hii ya kipindupindu itaisha lini.

Nawajibika kuomba Radhi

Kwa kweli nimepotea bila kutoa maelezo kwanza. Naomba radhi kwa hilo Ndesanjo kataka kuunda tume pamoja na kutaka kuwasiliana na FBI nitafutwe. Nimerudi. Naanza na nukuu hii ya Frantz Fanon. Kwamba wananchi ndio nguvu ya kubadili mambo. Niliwahi kuizungumzia bila kuiweka nukuu yenyewe: “To educate the masses politically does not mean, cannot mean making a political speech. What it means is to try, relentlessly and passionately, to teach the masses that everything depends on them; that if we stagnate, it is their responsibility and that if we go forward it is due to them too, that there is no famous man or woman who will take responsibility for everything and the magic hands are finally only the hands of the people”. Frantz Fanon
Nimeiweka ili kusisitiza kwamba tuna wajibu wa kuelimisha na kwamba sisi pia ni wananchi ambao tunaweza kuleta mabadiliko.

Tuesday, January 03, 2006

Kimya wenzangu!

Jamani nimekuwa kimya kwa muda sasa. Nilikuwa nakusanya nguvu baada ya igizo la tarehe 14. Wale waliotarajia mabadiliko makubwa nadhani wamekata tamaa. Wengine wanasema bunge limerudia kuwa la chama kimoja. Lakini Frantz Fanon anasema tuendelee kuelimisha wananchi mpaka wajue wao ndio wenye nguvu ya kuleta mabadiliko na hakuna mtu yeyote mmoja anayeweza kuleta mabadiliko ya maana isipokuwa wao wenyewe. Kwa wale wanaokubaliana na kalenda Gregory basi kheri ya mwaka mpya.

KITABU CHA WAGENI