Friday, April 21, 2006

Ripoti ya Transparency International kuhusu IPTL na Tanesco

Nimepata kupitia barua pepe yangu taarifa iliyotolewa na transparency international kuhusu lile dude la Tegeta linalogharimu serikali shilingi bilioni tatu kila mwezi (hapa ni wakati ambapo halijawashwa) Likianza kutoa umeme tuu unalipa bilioni tatu za kila mwezi na kulipia umeme watakaokuuzia. unaweza kuisoma hapa

11Comments:

At 7:28 PM, Blogger boniphace said...

Asante Nkya, nitakuja baadaye kulisoma ripoti hilo na kuangalia niandike nini kutokana nalo. Thanks sana kwa kujali na kututhamini sisi wenzako ili tupate taarifa kama hizi nyeti

 
At 7:34 PM, Blogger Indya Nkya said...

Comrade Makene, najaribu kutimiza wajibu wa kutaarifiana kuhusu matukio mbalimbali ya nchi yetu ili tupete mwelekeo wa namna ya kukabiliana na changamoto zinazotukabili.

 
At 11:42 AM, Blogger Christian Bwaya said...

Indya,
Natamani nikuone uso laivu. Weka picha yako basi? Staili ya bila picha inakuwa kama anonimasi bwana!

Taarifa yako imenifungua fahamu zaidi kuhusu namna nchi yetu inavyoondeshwa. Ngoja nikapunguze jazba nije nichangie nikiwa katika hali ya kawaida.

 
At 4:52 PM, Blogger mwandani said...

Niliisoma hii taarifa. Maswali yanaongezeka, majibu yanapungua kila nikifikiri.

 
At 1:33 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Idya nilikuwa sijapata fursa ya kuisoma hii report na leo baada ya kufanya hivyo (it took me an hour)naomba upokee tano zangu. Kama ulivyosema hapo juu kuwa unatimiza kazi ya kupashana habari, hii safi sana. Inafanana sasa na kuporomoka kwa kampuni nishat ya Enron hapa marekani. Uozo huu ulikuwamo hata Enron na hivi sasa Jeff Skilling (CEO wake) anahangaishana na mahakama. Na hawa watu hawana ujinga watamtia hatiani tu.

Inapokuja katika Tanzania tunaona kuwa suala la ten percent limetawala hapa. Au nipunguze upole wa lugha: rushwa kubwakubwa. Kinachosikitisha hapa, tofauti na Enron ambako kila kitu ni cha Marekani, sisi tunazungushwa vichwa kama pia na makabaila wa nje kwa msaada wa 'political heavyweits' kama ilivyoandikwa katika hii report.

Nchi tunaiuza wenyewe tena kibaya zaidi kwa bei poa pasi na kutanabahi watoto wetu watatuelewa vipi mbele ya Mungu (nafikiri hata Shetani atatushangaa).Chifu Mangungo alidanganywa na wakina Carl Peters kwa kuwa hakusoma. Lakini leo wakina Chifu Mangungo wa sasa wamesoma vema tu. Inatia uchungu.

Angalia sasa napata muunganiko huenda Banary Luhanga alishindana na serikali kutokana na vuguvugu hili. Kama sio hili tu basi yawezekana lilichangia vya kutosha tu. Kuna mithali ya Kiswahili isemayo "Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno". Ona sasa Baruhan (Hivi na Banary au Baruhani) Luhanga leo anaongoza 'Tanesco' ya nchi moja ya kusini mwa Africa badala ya sie wenye naye kumtumia ipasavyo. Ona sasa leo umeme bado ni kimbembe. Ona sasa IPTL bado ipo na inaendelea kunyonya kile kidogo kilichomo mifukoni mwa watanzania fukara.

Sasa basi wewe na mimi na huyu mwingine kesho tutakuwa tunaishikilia Tanzania katika nafasi anuai. Tunajifunza nini hapa ili tusijeipotosha nchi yetu na kulaaniwa na watoto wetu. Kwani watot hawawezi kuwalani wazazi, walau hata kwa kugoma kupalilia kaburi?

Alamsik Binuur

 
At 4:13 PM, Blogger Indya Nkya said...

Ripoti hii ni sehemu ya kitabu nadhani kinaitwa Urgly Malaysians. Inaelezea ni jinsi gani Wamalay wanavyotumia rushwa kuimaliza Afrika ya kina Mngungo wa leo kama anavyosema Mwaipopo. Kuna nukuumoja ya Mwalimu Nyerere kwenye hiyo taarifa kwamba; "kama ushirikiano wa nchi za kusini ndio huu basi heri ukoloni urudi". Ni hatari utaona jinsi ambavyo mambo yalikuwa si kawaida. Naomba muisambaze zaidi ili isomwe.

 
At 1:31 PM, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Nilikuwa natafuta sana ripoti kama hizi.Nitaikopi a'fu nitaisoma vizuri bila ya kukimbizana na muda wa "kafee"

Ahsante sana Indya!

 
At 5:07 PM, Blogger Habari Hub said...

Indya,

Kwa hakika jazba zinanipanda kadri ninavyoisoma hii ripoti nataka niwasiliane na huyu Cooksey ili niweze kuifanyia kazi hii ripoti iweze kuwafikia watanzania wengi zaidi.

Hongera Nkya ripoti hii imenifunulia zaidi machafu yanayofanyika katika serikali yetu. Yaani mtu eti anajidai kukataa rushwa ya dola 20,000 halafu baadaye anakula rushwa ya 100,000 nchi yetu imeuzwa kwa bei poa. Kwa hakika tusiposimama tukaitetea watoto wetu watayapiga viboko makaburi yetu.

 
At 8:31 PM, Anonymous Anonymous said...

Nkya,
Sasa unaongea. Umefanya jambo la "mbolea" sana kuanika ripoti hii. Uzuri wa blogu ni kuwa hata baada ya miaka kumi mtu akiwa anatafiti haya mambo anaweza kuja hapa akaipata. Naipitia kisha ndio nisema.
Asante kwa kutupa taarifa hii.

 
At 6:55 PM, Blogger MICHUZI BLOG said...

nkya hata mie umenikuna. nikishapitia nitatoa maoni yangu binafsi.

 
At 1:17 PM, Blogger lolyta said...

I want to encourage you to definitely continue your great
job, have a nice evening!

selaput dara buatan
selaput dara keperawanan
selaput keperawanan
Jual Selaput Dara
selaput dara palsu
selaput dara

MACAM - MACAM ALAT BANTU SEX PRIA DEWASA

JUAL BONEKA SEKS FULL BODI TERBARU


JUAL VAGINA PANTAT BERTATO GETAR SILIKON


JUAL TENGA ALAT BANTU SEX


JUAL ALAT BANTU ONANI FLESHLIGHT


JUAL VAGINA PINGGUL FULL SILIKON


JUAL VAGINA BULU GETAR

MACAM - MACAM ALAT BANTU SEX WANITA DEWASA.


JUAL VIBRATOR FANTASY BLISS MURAH


JUAL ALAT BANTU WANITA VIBRATOR THORN DRAGON


JUAL SEX TOYS HAPPY SOME


JUAL PENGGELI PUTING PAYUDARA


PENGGELI VAGINA TERBARU MIC


JUAL C-STRING ALAT SEX WANITA



PENGOBATAN DAN OBAT KESEHATAN HERBAL ALAMI


SEMENAX OBAT HERBAL PENYUBUR SPERMA


OBAT PERANGSANG UNUTUK PRIA ATAU WANITA


OPIUM SPRAY

JUAL PERANGSANG RED SPIDER CAIR



OBAT DAN ALAT PEMBESAR PENIS

VMENPLUS HERBAL

VIMAX PEMBESAR PENIS DEWASA

MAXMAN CAPSULE

PRO EXTENDER

VMENPLUS
VMENPLUS HERBAL
PEMBESAR PENIS ALAMI
OBAT EJAKULASI DINI
OBAT VMENPLUS

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI