Wednesday, February 15, 2006

NEPAD ubeberu mpya

Kuna mjadala sasa kwamba hili dude linaloitwa NEPAD ni aina mpya ya ubeberu ambapo Afrika ya Kusini inatumia kupeleka mitaji katika nchi nyingine za Afrika. Kuna bwana mmoja kaandika kitabu juu ya hili. Lakini hata kusingekuwa na hicho kitabu hili ni jambo la wazi kabisa. Ukiangalia changamoto wanazokabiliana nazo hawa jamaa wa Afrika ya kusini utagundua kwamba ni ukweli mtupu. Baada ya ule mfumo wa kibaguzi kwisha mwaka 1994 ilibidi watafute nafasi ya kuwakuza kiuchumi weusi. Njia rahisi ilikuwa ni kuwatafutia weupe nchi za kupeleka mitaji yao ili nafasi ibaki nchini mwao kuwasaidia weusi. Nchi nyingi za kiafrika zimeingia kwenye makubaliaono hayo bila kuona janja ya hawa jamaa. Tatizo ni kwamba biashara inakuwa ya upande mmoja. Nchi nyingi sana hazina mtaji wa kuwekeza Afrika ya kusini. Kwa hivyo tutawasidia kupunguza matatizo yao huku hizo sera zikiwa hazisaidii sana nchi zingine. Wanapotoka kwenda nje hawana mpango wowote wa kuendeleza nchi wanazowekeza. lao ni kupata faida na kuondoka. Ubeberu huu mpya sijuhi utatufikisha wapi.

2Comments:

At 7:49 AM, Anonymous Anonymous said...

Kaka Nkya sio matani. Nashangaa watu wanafurahia wawekezaji kwamba watawakomboa na kuleta maendeleo. mimi niko Ughaibuni bwana ila nikipata hela najenga kwetu na sijengi huku niliko. na najua hao jamaa ndio hivyo hivyoo. Nchi itakombolewa na wananchi wake na sio wageni toka nje. Fikiria Wewe kama Baba ndani ya nyumba uanze kufikiria kwamba bwana fulani ataokoa maisha ya wanao na wewe unamuacha tuu ukidhani atawaokoa kama ambavyo wewe unefanya sio ukweli, Ni wewe mwenyewe ndio utawaokoa) hata kama huyo mtu ambaye unampa familia ana rangi gani au umbo gani. Still ni wewe mwenyewe ndio utaweza kujikomboaa na usitegemee nje.

 
At 9:01 AM, Blogger Indya Nkya said...

Kaka huo ndio ukweli. Hawa jamaa wameweza kuwadanganya waafrika wenzao na kuanzisha hilo dude kusaidia kupunguza Pressure kwao. Halafu nchi nyingi zinaingia kichwa kichwa. Nchi haiwezi kujengwa na watu toka nje kama ilivyo familia. Ukiona mtu anajifanya kujenga kwako ujue kuna kitu atapata na ni kikubwa kuliko kile anachojifanya kusaidia.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI