Kimya wenzangu!
Jamani nimekuwa kimya kwa muda sasa. Nilikuwa nakusanya nguvu baada ya igizo la tarehe 14. Wale waliotarajia mabadiliko makubwa nadhani wamekata tamaa. Wengine wanasema bunge limerudia kuwa la chama kimoja. Lakini Frantz Fanon anasema tuendelee kuelimisha wananchi mpaka wajue wao ndio wenye nguvu ya kuleta mabadiliko na hakuna mtu yeyote mmoja anayeweza kuleta mabadiliko ya maana isipokuwa wao wenyewe. Kwa wale wanaokubaliana na kalenda Gregory basi kheri ya mwaka mpya.
9Comments:
Karibu tena Nkya,
Kimya chako kilianza kututisha.Tuendeleee kufanya kinatochotakiwa kufanywa.
Nadhani ile ilikuwa tamthilia. Maana inaendelea.
Leo mwongozaji wa tamthilia ametuingiza kwenye hatua nyingine. Wazee ambao tulidhani mchango wao umetutosha, wamerudi tena. Na wanaigiza katika sehemu nyeti kabisa!
Tusubiri kuona kinachoendelea...
Heri ya mwaka mpya kaka.
Karibu sana Nkya. Igizo lile linaendelea. Huna tiketi ya kuingia ukumbini?
Wenzangu, kazi tunayo. Wazee sijuhi mpaka lini? Uchifu huu!!!
Umenunuliwa nini na hawa jamaa wa ari mpya?? Ngoja tutaunda tume ya kuchunguza huu ukimya!
Frantz Fanon anatupa fundisho kubwa. Tukienzi mafundisho yake tutafika mbali sana. Tuendelee kuwafundisha kwa Njia Mpya mpaka wajitambue.
Nkya,
ninawasiliana ana Efu Bi Ai ili tuanze kukutafuta.
Frantz Fanon anatupa fundisho kubwa.
Cheers,
best survey sites
Wazee sijuhi mpaka lini? Uchifu huu..
Cheers,
what is debt consolidation
Post a Comment
<< Home