Tuesday, November 15, 2005

Uhuru si urithi

Nimekutana na nukuu hii:

"No people are really free until they become the instrument of their own liberation. Freedom is not a legacy that is bequeathed from one generation to another. Each generation must take and maintain its freedom with its own hands." By John Henrik Clarke

Kila kizazi inabidi kipambane kujipatia uhuru wake.

9Comments:

At 4:05 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Nukuu nzito kweli hii Nkya. Nitaiweka kwenye mjadala fulani ninaouandika. Alilosema ni kweli. Fanon alisema kuwa kila kizazi kina wajibu wake...kinaweza kuamua kutimiza wajibu huo au kutupilia mbali.

 
At 4:39 PM, Blogger boniphace said...

Hili linabainisha wazi kuwa hao wafame waliopitwa na wakati wanatakiwa kungolewa kwa sururu na sio uoga tena. Safari ya ukombozi inatakiwa kuanza na kizazi kilichokimbia giza

 
At 8:52 PM, Blogger Indya Nkya said...

Ni kweli kabisa. Hatuwezi kungoja. Hiyo nukuu inatuambia kwamba kama kizazi kilichopita kilipigania uhuru kumuondoa mwingireza halafu wakaanza wao kuwa wakoloni wapya lakini weusi inabidi tuwan'goe sasa.

 
At 9:18 AM, Blogger mloyi said...

Inapinga mambo mengi tunayoamini huku. 1961 tulipata uhuru wa zamani, sasa tunahitaji uhuru mpya. Tutumie kauli ya mpiganaji clarke kuanzisha vuguvugu.

 
At 1:29 PM, Blogger Indya Nkya said...

Nitakutumia makala moja bwana Mloyi inayosema kwamba tulikuwa huru tangu 1967-1985 tuu

 
At 2:55 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Nkya, nami naomba makala hiyo ya uhuru tuliokuwa nao hadi 1985.

 
At 6:54 PM, Blogger Indya Nkya said...

Nitaiweka isomwe hadharani

 
At 7:38 PM, Blogger Innocent Kasyate said...

Oh, nilikuwa sijui kwamba uhuru ulikwisha mwaka 1985.Hebu tupashe mheshimiwa manake mimi nilifikiri hatujawahi kupata uhuru kabisa.
Una ushahidi wowote kuonesha tulikuwa huru kabla ya 1985?
Nasubiri makala yako.

 
At 12:29 PM, Blogger Fikrathabiti said...

Sasa jamani kibaraza cha NKYA chazua mambo mazito mazito na yasiyopaswa kupuuzwa hata chembe.

Mimi nafikiri uhuru wa kweli tunaouhitaji kwasasa mbali na wa bendera ni uhuru wa kifikra ambao nadhani brother innocent anauzungumzia.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI