Saturday, November 05, 2005

Kwa nini?

Umeshawahi kujiuliza kwa nini Amani Karume awe rais wa Zanzibar? Kwa nini Ndugu yake ni balozi? Kwa nini Hussein Mwinyi ni Naibu Waziri wa Afya? Kwa nini Watoto wawili wa Nyerere ni wabunge wa kuteuliwa? Kwa nini? Nimeulizwa. Mimi nikasema kwa vile ni wanasisiemu wazuri. Nikaulizwa je ni wao tuu ambao ni wanasisiemu wazuri? Je ni kwa vile baba zao walikuwa Rais kwa vipindi tofauti? Sijuhi.

8Comments:

At 3:55 PM, Blogger mloyi said...

Kwanini, labda ni kwa kuwaenzi baba zao. Baba zao ni nani? Labda ni maarufu kuliko Mkwawa na Mirambo. Chaburuma na Mangi, hata Rumanyika.
Siasa sasa. Kesho raisi ni mtoto wa mkapa baada ya mttoto wa kawawa.

 
At 4:37 PM, Anonymous Anonymous said...

KWANINI??

 
At 8:39 PM, Anonymous Anonymous said...

Mimi nadhani ni kwa sababu tuu ni watanzania kama wengine. Nyingine ni hisia tuu!!

 
At 3:21 PM, Blogger mwandani said...

george bush=george W bush

Zulfiqar Ali Bhutto=Benazir Bhutto

Indira Gandhi=rajiv=Sonia...

Oginga odinga=raila odinga

jomo kenyatta=uhuru kenyatta

Jfk=keneddy=kennedy=kennedy

Lee Kwan yew= Lee...

govan Mbeki=Tabo Mbeki

Hosni Mubarak=Mubarak mtoto

Hefez Al Assad= Assad mtoto

Ndi mambo yalivyo... kwa nini?

 
At 3:34 PM, Anonymous Anonymous said...

Labda ukweli ni uleule wa kurithi kazi ya baba. Kama baba alikuwa fundi seremala mtoto anaweza kurithi, mkulima mtoto anaweza kurithi nakadhalika. Lakini siasa bwana ni urithi mzuri. Nadhani watoto nao wanaandaliwa na wazazi wao kuongoza. Kama hawaandaliwi basi wanaangalia na kugundua utamu uliopo ukishakuwa kiongozi. Siasa hasa za Afrika ni nzuri sana. Haziumizi kichwa kabisa lakini wakati huo huo unapata raha si za kawaida. Kwa nini watoto wasirithi kazi rahisi na yenye marupurupu kibao!!

 
At 3:53 PM, Anonymous Anonymous said...

Grolia Aroyo = ?

Chandrika Bandanaranaike Kumaratunga = ?

Baby Doc = ?

Joseph Kabila = ?

Bashar Al Assad = ?

Faure Gnassingbé = ?

Megawati Sukarnoputri = ?

Wapo wengi wanaorithi hatamu za uongozi utafikiri ni hatamu za kichifu, kitemi, kisultani au kifalme. Bwana Mwandani, kawataja wachache nami nawaongezea wengineo. Na wewe ukiwa nao waongezee halafu tutawajumlisha, tutawatoa, na kuwagawanya ili tupate kuijua kanuni(formula) yao.

Masalaam, ni miye maridhiya,

F MtiMkubwa Tungaraza.

 
At 8:55 PM, Blogger Indya Nkya said...

Seretse Khama= Ian Khama (Botswana)

 
At 12:51 PM, Blogger Fikrathabiti said...

Mimi nadhani ni mbinu chafu ya kufukia yale maovu waliyofanya wakati wa utawala wao.Hivi MLOYI unaweza kumrudi na kumuadhibu baba yako mzazi kweli?????
ABED KARUME+AMANI KARUME=Siri kuu ya uozo uliotawala madaraka yao.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI