Saturday, October 29, 2005

Uganda imeendelea sana, haiitaji msaada wa IMF

Kuna habari inayoifagilia kweli nchi ya Uganda ilivyopiga hatua ya kimaendeleo. Sijuhi. Kama vigezo walivyotumia ni sahihi basi Uganda iko mbali. Lakini kama ni suala la kucheza na takwimu tuu, basi kila nchi inaweza kuonekana imeendelea au haijaendelea. Naziogopa sana takwimu japo nacheza nazo kila ukicha. Kwa upande mwingine licha ya maendeleo haya, bajeti ya uganda inafadhiliwa kwa asilimia kama 50 hivi na wahisani wa nje. Innocent tuambie. Mtaani Uganda mambo yakoje? Soma habari hiyo hapa

1Comments:

At 11:49 AM, Blogger Innocent said...

Hapa kuna unafiki mkubwa sana wa hawa mabwana wa Britton Woods.Ukisoma habari hapa ni malalamiko juu ya rushwa na hata Museveni wamemchoka sasa.
Ila tukumbuke Museveni anajua unatakiwa ufanye nini ili ukubaliwe na hawa wezi wakuu wa dunia.Mfano ni rais pekee aliyemuunga mkono Bush kule Iraq na kutangaza yuko tayari kutuma askari.
Ukiangalia mtaani watu masikini hapa wako kama kule Tz tu siwezi kutofautisha ila nafikiri kuna kelele kubwa ya rushwa sana.
Kwa siasa hizi za kupakana mafuta,
Tumekwisha.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI