Thursday, October 27, 2005

Ethan akiri ugwiji wa Ndesanjo

Ethan Amekubali kwamba Ndesanjo Si mchezo jinsi alivyoweza kuhabarisha wasomaji wake kilichokuwa kinaendelea katika mkutano wa Pop Tech huko Camden. Kilichomuacha hoi ni jinsi Macha alivyoweza kuandika karibu kila kitu kilichokuwa kikiendelea tena akitafsiri kwa kiswahili. Lazima na mimi nikupongeze kwa hili ndugu yangu. Ongeza bidii. Lisha jamii habari Mangi. Ukifungua blogu ya Ethan utakumbana na hiyo habari. Tumpe Ndesanjo hongera zake kwa hili. Ukibonyeza HAPA utasoma kwa undani alichosema Ethan

4Comments:

At 4:36 PM, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Mimi namkubali kwa asilimia 100 kwa habari zake ana lake.Kuna wanachuo wenzangu wamekuwa wakiniuliza sana kuhusu huyu mtu(Ndesanjo) kwanza alionekana kama vile ni mtu aliyekuwa akipinga kila kilichokuwa kikifanywa nmaserikali yetu.Wengi wamekuwa wakisoma habari zake kupitia Mwanachi Jumapili.Lakini wamekuja kuona kuwa kumbe ni kama alikuwa akiwafumbua macho watanzania,wamekuwa wakiniambia "leo rasta kasema nini?" niliwaambia na wao wanaweza kumsoma zaidi kupitia blogu sasa ndio hapo hii teknolojia ya blogu ilipoaanza kusomwa na wanachuo wengi na kupata mawazo mapya na kufunguka fikra.
Lazima nimpe pongezi sana bwana Ndesa

 
At 12:28 PM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Hongera Ndesanjo!

 
At 4:28 PM, Blogger boniphace said...

Huyu Ndesanjo yaani acha tu, kasi aliyonayo ni mpya sana zaidi ya falsafa ya yule mgombea wa CC. Tena anaandika kwa ari na nguvu angavu siku zote. Sijui kwa nini wagombea wa Bongo hawakumuona na kumpa dili la Kampeni au waliogopa malipo yake si unajua anakaa mtoni huyu!

 
At 11:37 AM, Blogger mloyi said...

Anapenda kila mtu ajue kama yeye!
Anataka kuongea na kila mtu, anasoma kila kitu hata kama hakubaliani nacho na ata bandika kwenye blogu yake.
anafanya kazi nzuri sana.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI