Monday, October 17, 2005

Maajabu haya!!

Jamaa wa Kanisa la Ephata wameamua kwenda Israel kuombea uchaguzi mkuu na pia mahusiano mazuri kati ya Israel na Tanzania. Wakati huo huo Huyo kiongozi wao anawambia watanzania wengine waombee uchaguzi. Hivi, kwa nini wasingeombea wote nyumbani mpaka waende Israel? Kama anaona Israel ni mahali patakatifu ambapo sala zao zitakubalika zaidi, kwa nini sasa awaambie watanzania wengine wanaosalia nje ya Israel waendelee kuomba? Ndesanjo atalieleza vizuri hili. Halafu anataka uhusiano na Israel uwe mzuri, sababu zilizofanya uwe mbaya ni zipi? Je sababu hizo sasa si za msingi tena? Israel inaheshimu haki za Wapalestina? Soma habari hiyo hapa.

2Comments:

At 10:13 AM, Anonymous Anonymous said...

Hi :)

Your blog is great! I will make sure to bookmark it and visit regularly. Keep up the good work!

Please visit my site if you get some time: home based businesses

 
At 2:59 PM, Blogger mwandani said...

kanisa la ephata linaamini nini. Ningeelewa zaidi kama ningejua itikadi zao. naamini Mungu anaweza kuombwa popote. Mantiki rahisi - kama yeye ni Muumba basi dunia nzima takatifu.Kwanini aumbe uchafu? Sioni kwa nini afanye upendeleo.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI