Friday, October 07, 2005

Kichaka alitumwa na Mungu

Msemaji wa George Kichaka anakana kwamba rais wake aliwahi kusema kwamba alitumwa na Mungu kuivamia Iraq na Afrighanistan kama inavyodaiwa na mwakilishi wa mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati toka Palestina Bwana Nabil Shaath. Kukana ndio kawaida ya wasemaji wote wa serikali duniani. Cha kukumbuka ni kwamba vita hizi zote huombewa kwanza na wahubiri maarufu kama vile Bill Graham. Huyu ndiye Mungu wa Kichaka anayetaka kwenda kuua wairaq. Soma habari hiyo hapa

5Comments:

At 12:06 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Sio kitu cha ajabu kuona kwamba mwanasiasa fedhuli kama Bush anakana matamko yake mwenyewe.Kinachosikitisha ni kwamba alimshirikisha mwenyezi mungu kuhusu ukatili na unyama unaofanywa na taifa la Marekani duniani kote.Lakini tukae mkao wa kula,yana mwisho haya.Hivi jamani nitapata wapi kitabu cha Kuli cha Adam Shafi?

 
At 5:06 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Lakini kwakuwa, kwa mujibu wa fedha za marekani, taifa la marekani ni taifa la "in god we trust" basi lazima kiongozi wake atakuwa anaongozwa na mungu. Ila nitakachoongeza hapo ni maneno yale yaliyosemwa na mshairi KRS-One. Alisema kuwa hamwamini yule mungu wa kwenye "god blesses america." Nami nakubaliana naye.

 
At 10:38 AM, Blogger Indya Nkya said...

Sina ubishi na huyo bwana nadhani mungu ni tofauti kabisa.

 
At 9:41 PM, Blogger boniphace said...

Haya tumeyajadili jana katika darasa la Polirtical Economy. Nafurahi kusoma leo, Bush na wenzake wanaoongozwa na mtazamo wa Liberal Conservatives wanaoamini kuwa kuna watu wanaopewa nguvu na Mungu na Mungu anachagua kuzungumza nao. Haya mawazo ya kishenzi sidhani yatawatoka lini. Tangu lini Mungu aache kuzungumza na maskini amtafute George Bush!

 
At 10:13 AM, Anonymous Anonymous said...

Tumuamini Kichaka. Alitumwa. Alipokuja akatuambia mungu ni mmoja, na huyo mungu ni wao, na wa kwetu hakuwahi kuwepo, tukamwamini. Sasa leo huyo huyo kaleta habari kuwa mungu kamtuma, tunakana eti hajatumwa na mungu. Hapana jamani twendeni pooole pooole. Alishamtuma mwanzo, amemtuma sasa na atazidi kumtuma. Kwani alishawahi kumtuma akatuuza utumwani, akatutawala, akapiga Vietnam, na mengineyo. Kichaka anamfahamu huyo mungu kulikoni yeyote wetu. Tuamke kumekucha...

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI