Friday, September 23, 2005

Ya Zimbabwe kutokea Africa ya Kusini

Licha ya staili ya Bob Mugabe kukamata mashamba ya Wazungu na kuyagawa kwa wazalendo kulaaniwa vikali na baadhi ya nchi, Afrika ya Kusini inataka kujifunza mbinu toka kwa Bob. Soma habari hiyo hapa

3Comments:

At 4:28 PM, Blogger mwandani said...

Baada ya Bob kuchukua ardhi, wanamchora picha kama Saddam, sasa kipenzi chao na dira ya maendeleo Afrika akianza, sijui watamchora kama nani. Ardhi ndio mzizi wa vurumai lote...

 
At 8:35 PM, Blogger Dennis Mponji said...

Hii itakuwa hatari maana ninavyojua mimi hapa South Africa watu weusi huwa hawalimi sasa wakitwaa ardhi toka kwa watu weupe si ajabu hii nchi ikaanguka vibaya sana kiuchumi.

 
At 12:38 PM, Blogger Indya Nkya said...

Itabidi wabadilike. Nadhani hata wazimbabwe ndivyo walivyo. Wamezoea kuajiriwa kwenye mashamba ya wazungu na kupata mishahara. Hiki ndicho kirusi kinachotakiwa kupigwa vita. Kirusi cha kutoweza kujiajiri mwenyewe lakini wakati huo huo unalilia ardhi. Baadhi ya weusi Zimbabwe walipewa ardhi na mikopo ya kuanzisha kilimo, badala ya kununua trekta na pembejeo wakanunua BMW na BENZ.Wakati mzungu ananunua trekta na kuvaa boots kuelekea shambani, mweusi anakwenda mji hadi mji, hoteli hadi hoteli kuonyesha ubabe wa benzi mpya!

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI