Tuesday, September 13, 2005

Kimya

Jamani nimekuwa kimya kwa muda mrefu sasa. Nilibanwa na shughuli kibao. Nilikwenda pia Nyumbani kuwaona ndugu jamaa na marafiki. Nyumbani sasa ni kampeni mtindo mmoja, watu kujieleza kwa wananchi, mlungula kutembezwa pale inapobidi, kila mgombea kumtoa mwenzake kasoro na mambo mengine ya namna hiyo. Barabara za Dar zimezidi kuwa finyu, magari ni mengi kuliko uwezo wa barabara. Barabara ya Shekilango iliyojengwa miaka michache iliyopita inatisha. Imebomoka yote. Sinza yote sasa inafanana. Zile barabara za vichochoroni hazina tofauti na barabara kuu ya Shekilango. Cha kusikitisha ni kwamba uwezo wa hii barabara ya Shekilango ni kupitisha magari yasiyozidi tani kumi kama sikosei. Wapi? yanapita mpaka ya tani 30. Ukiongezea na ukweli kwamba hakuna mifereji ya kupitisha maji basi mvua inavyonyesha inazoa kila kitu. Barabara hoi.

1Comments:

At 12:29 PM, Blogger mwandani said...

hapo tu ndio nnapokoma mimi. Nasikia uchumi wetu umepanda kwa asilimia tano mwaka jana. Mapesa yameahidiwa na akina IMF. Pengine hazina watatoa mgao tujenge mifereji na barabara viuno na migongo visiumie na mashimo.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI