Thursday, July 21, 2005

Nimekutana na Ethan Zuckerman

Leo jioni nimekutana na Ethan Zuckerman Tumejadili mambo kadhaa likiwepo jambo muhimu la wanablogu wa Tanzania. Jambo moja analosema ni kwamba watanzania wengi wenye kublogu ni waandishi na wamejikita sana kwenye mijadala ya kisiasa. Si kwamba ni vibaya. Jingine ni kwamba watu wengine mitaani hawako kwenye hii taaluma ya kutumia blogu. Hili la pili lina maelezo- miundombinu hafifu; si rahisi kwa watu wengi kutumia blogu kutoa mawazo yao kwa vile teknolojia bado ni ya hali ya chini. Jingine la msingi ni kwamba je ni watu wangapi wanaosoma mawazo yetu tunayoandika kwenye blogu? Kama wasomaji ni wachache ni namna gani basi tunahakikisha kwamba mawazo yetu yanafikia jamii kupitia magazeti na vyombo vingine? Hili ni jambo la kufikiria kabisa wanablogu wote watanzania. Mambo tunayoandika kwenye blogu yanawafikia wanajamii? Kwa mfano wanasiasa kweli wanasoma blogu? Kama hawasomi tutawafikishiaje ujumbe? Kaniuliza pia jambo lingine ambalo sikuwa na jibu lake. Hili waandishi mnaweza kulijibu. Ni kweli kwamba mnayoaandika kwenye blogu hamyaandiki kwenye vyombo vya habari mnavyofanyia kazi? Kwa kuwa siandiki magazetini sikuwa na jibu. Labda msaidie hapo.
Kesho atatoa mhadhara hapa chuoni nitahudhuria na kutoa mchango wangu kuhusu blogu za kiswahili.

3Comments:

At 2:00 PM, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Kama blogu zetu zinasomwa kwa hili kwa kweli teknolojia yetu bado iko chini sana hasa huko vijijini sidhani... lakini hapa mijini tunasomwa sana hasa vijana kwa sababu wanakuwa kama vile ndio wameamka zamani ulikuta mtu anaogopa kusema ukweli wa kiongozi

 
At 2:10 PM, Anonymous http://eap.uonbi.ac.ke/ said...

Jambo la uandishi ni nzuri, inatakiwa kujua nyancha zote.

 
At 2:12 PM, Anonymous Mary said...

Hizi ni enzi hatari, yatupasa kuchunguza na kuchambua mambo kimakini.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI