Wednesday, July 13, 2005

Unmfahamu George Galloway?

Huyu ni mwakilishi katika "House of Commons" Uingereza, anawakilisha eneo ambalo watu wake wengi walikufa katika milipuko iliyogharimu maisha ya waingereza wasiopungua 50 karibuni. Huyu bwana ameamua kusema ukweli. Anasema haya ni matokeo ya chuki ambayo imeongezeka dhidi ya Uingereza na Marekani kutokana na sera zao mbovu hasa huko Iraq, Afrighanistan, Mambo yanayotokea Guantanamo bay, yaliyotokea katika gereza la Abu Ghraib huko Iraq na mengineyo. Pamoja na kulaani hiki kitendo cha kulipuliwa waingereza kwa nguvu zote, bado anahoji mantiki ya kutoona wale wanaouwawa Iraq kila siku kama binadamu wengine. Anasema kuna watu wanaofikiri kwamba damu ya Wairaq waliouwawa Falujah wakati mji unateketezwa na wanajeshi wa ushirika ikiwemo Uingereza haina thamani kama waingereza waliouwa kwenye mashambulizi hayo. Tafadhali soma mawazo yake kama yalivyonukuliwa katika taarifa rasmi ya bunge (Hansard) Hapa

2Comments:

At 8:48 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Galloway nilimsikia akiongea. Ana kipaji cha kuongea hasa. Ila hoja anayoizungumzia hapo kuhusu binadamu wengine kuonekana kuwa ni bora zaidi ya wengine ni nzito sana. Nimeshangaa vyombo vya uongo (habari) viliiweka kapuni. Kwanza wala sishangai maana najua kwanini.

 
At 7:47 PM, Anonymous Anonymous said...

Hii ni tabia sugu ya vyombo vya magharibi kutia kapuni mambo au majadiliano yanayowasuta wazi wazi.Hawataki kusikia hayo.Lazima wana blogu wasaidiane kusambaza ujumbe kama huu.Ni muhimu wakaambiwa kwamba tunajua nini kinatokea na siku moja na ninyi mtajua.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI