Thursday, June 30, 2005

Kiswahili lugha yetu

Kuna makala mbili za Padre Karugendo zilizopo kwenye blogu ya Ndesanjo kuhusu Kiswahili. Moja ya jambo aliloonya ni kwamba kama Tanzania italala na kufikiri kwamba ni bingwa wa kiswahili, basi kuna siku utasikia wakenya, waganda, wakongo waafrika ya kusini wakiwa ndio waalimu wakubwa wa kiswahili na wakawa wanatengeneza fedha kupitia lugha ambayo Tanzania inaweza kabisa kujisifu ndio gwiji wake. Mambo kama haya yameshatokea duniani si mageni. Wareno katika historia walikuwa wa mwanzo kabisa kufanya tafiti na kugundua mambo mengi lakini wakalala wakaanza kunywa mvinyo wakapitwa na nchi nyingine za ulaya. Sasa hivi Ureno ni kati ya nchi masikini barani ulaya. Mfano mwingine ni wa Malasia na Ghana katika kilimo cha Mawese, nchi hizi mbili zote zilipata uhuru mwaka 1957, Ghana ilikuwa mzalishaji mkuu wa mawese ambayo ni malighafi muhimu sana, Wamalei walikuwa wanakwenda Ghana kujifunza kilimo hicho, waghana walikuwa wakienda Malasia kuwafundisha namna ya uzalishaji wa zao hilo. Angalia leo tofauti iliyopo kati ya Malasia na Ghana. Malasia sasa hivi ni mzalishaji mkuu wa Mawese duniani, wakitumia taaluma ya kisasa. Ghana sasa wanajifunza toka Malasia. Mifano ni mingi. Tunajifunza?

3Comments:

At 12:23 PM, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Tena umenikumbusha ni leo katika radio moja hapa TZ walikuwa na mada moja kuhusu kiswahili...lakini nakumbuka waliongelea kuhusu utandawazi na kiswahili.Kwa kifupi sisi ndio tunaonekana kama "wamama" wa kiswahili Afrika lakini wenzetu wakenya wanakitangaza sana kiswahili kuliko sisi... tumekalia "Umarekani" mwingi! Whatts up! nyingi

 
At 2:08 PM, Blogger Reggy's said...

Nimefurahi kusikia kuwa una kawaida ya kutembelea blogu yangu, pia nimesikitika kuwa huwa unakwama kunitumia maoni. Nitajitahi kurekebisha kasoro hiyo, sikujua kama inakwamisha wengi. Bye

 
At 8:52 PM, Anonymous Anonymous said...

Wengi wa wafasiri wa Kiswahili nje ya nchi ni Wakenya. 'Software' maarufu kwa wafasiri wa lugha (TRADOS) ina bendera ya Kenya. Kazi kwetu.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI