Saturday, June 25, 2005

Majadiliano ya Doha

Jumapili ya tarehe 12/6/2005, kulikuwa na majadiliano mazuri yaliyoendeshwa na mwandishi maarufu wa BBC Tim Sebastian huko Doha Qatar. Majadiliano yenyewe yalihusu kama Wanawake wa nchi za kiarabu wawe na usawa kamili. Kulikuwa na pande mbili zilizokuwa zikijadili pamoja na wachangiaji wengine wengi, upande mmoja ukiwa na waunga hoja mkono ukiwakilishwa na mwanamama mmoja ambaye ni mbunge wa kwanza mwanamke nchini Jordan na Bwana mwingine ambaye ni mtangazaji toka Kuwait. Wachangiaji wa upande huu walielekea kuifahamu barabara jamii ya kiarabu. Walionyesha jinsi watu wengi wanavyochanganya mila za asili za uhafidhina za kiarabu na Uislamu. Nilichojifunza toka kwao ni kwamba wanawawake wanavyochukuliwa katika nchi nyingi za kiarabu si ndivyo uislamu unavyotaka bali ni mila za kale za kiarabu.

Upande wa wa pili wa hoja uliwakilishwa pia na mwanamama na bwana mwingine ambao wote wamekulia nchi za magharibi. Hawa pamoja na kuonekana kutoilewa vema jamii kutokana na kuishi nje walionya kuhusu nchi za kiarabu kuiga demokrasia ya magharibi kichwa kichwa. Lingine lililojitokeza ni uelewa kuhusu usawa kwa wanawake. Watu wengine bado wanafikiria usawa ni hali ya mwanamke kubadilika na kuwa kama mwanaume. Ukizungumzia usawa wanasema basi wanawake wakiwa sawa na wanaume ule uanawake wao utapotea, wanafikiri usawa ni mwanamke sasa kuwa mwanaume. Kinachozungumziwa ni nafasi. Mwanamke apatiwe nafasi kama anazopatiwa mwanaume na tuone kama hataweza. Ni lazima tujue kuna tofauti za maumbile ambalo ni suala la kibiolojia tusiloweza kushindana nalo. Mjadala uliitimishwa kwa kura waliounga mkono hoja walipata asilimia 86 na waliopinga walipata asilimia 14.

Hoja ya kutoiga kila kitu toka magharibi ilinifurahisha mno kwa sababu hata kwetu sisi weusi na watanzania kipekee ni mabingwa wa kuiga mara nyingi mambo ya hovyo zaidi kuliko ya msingi. Wakati mmoja Ndesanjo aliandika makala ambapo aliuliza kwa nini kwa mfano tusiige mambo mazuri toka kwa wazungu kwa mfano kuheshimu muda na kutunza mazingira kuliko kuiga mambo ya hovyo kabisa? Huko tuendako kwa kasi hii ya kuiga ni lazima ukiwa na watoto wa jinsia yoyote ile utenge pesa za kusuka nywele na kununua hereni kwa wanao.

2Comments:

At 10:27 AM, Blogger mwandani said...

Safi sana kaka.

 
At 8:55 AM, Anonymous oscar munishi said...

kaka nimesoma na nimeeelewa sana kazi yakonina maswali macache sana je mambo ya ovyo maana yake ni nini?na ni wakati gani jambo fulani litaitwa la ovyo,
kaka swala la usawa bado sana linatakiwa clarification ya kutosha na lisiwe likawa linadidimiza hali ya kielim tanzania ukitaka kujua waulize wanafunzi wa uhandisi wa chuo kikuu cha dar es salaam utajua kaka, je usawa wenyewe tunauongelea katika nyanja gani, je kuna usawa darasani?je tunatakiwa kuongelea gender equality au gender equity darasani?
natumai utatafakari na kunieleesha mie mwenye upeo mdogo
ahsante sana

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI