Wednesday, June 08, 2005

Elimu ya Dini Tanzania

Hivi ule ufundishaji wa dini katika shule za sekondari umebadilishwa? Wakati tukiwa sekondari kulikuwa na utaratibu mbovu unaofundisha ukristo, uislamu, uprotestanti ukatoliki katika shule. Walikuwa wakija Mapadre, Wachungaji, masheik kufundisha dini. Wakija mnatenganishwa. Waislamu darasa lao, waprotestanti la kwao wakatoliki la kwao. Nilichukia mno utaratibu huu kwani ulikuwa haufundishi elimu ya dini bali dini. Matokeo yake mtu anafundishwa dini nyumbani, kanisani na misikitini na shuleni. Shule ingetakiwa itoe elimu ya dini. Tofauti ni kwamba shuleni watu wanatakiwa wafundishwe kufikiri, kuzielewa dini zote kuanzia za asili na za kuja na wasifundishwe na viongozi wa dini wahafidhina bali wafundishwe na watu wenye upeo mkubwa wa theolojia. Hii inawapa wanafunzi uwezo wa kuzielewa dini kwa undani na kuzijadili bila jazba hata baada ya kuhitimu shuleni. Mwenye uhakika kama mfumo huu umebadilishwa naomba aniambie kama bado tupige debe ubadilishwe.

1Comments:

At 5:09 AM, Anonymous Anonymous said...

Msumari umegonga penyewe. Hoja nzito sana hii. Sana, mno. Tofauti ya kufundisha dini na kufundisha elimu ya dini...hapo ndio tumepotea njia.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI