Saturday, May 14, 2005

Vita dhidi ya dawa za kurefusha maisha

Kuna malumbano makali Afrika ya Kusini baada ya kundi la wanaharakati wanaounga mkono matumizi ya dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa UKIMWI kupeleka kesi mahakamani kutaka Daktari wa Kijerumami Matthias Rath aache kupinga matumizi ya dawa hizo. Daktari huyu amekuwa mpinzani mkubwa wa ARV's kwa madai kwamba zina madhara makubwa sana kiafya. Badala yake anapendekeza lishe bora pamoja na matumizi ya vitamini muhimu kwa waathirika. Kesi ilipotajwa jana kulikuwa na makundi mawili, moja likimuunga mkono daktari huyu na lingine likimpinga. Nusura zipigwe nakuambia. Dr. Rath anasema kwamba madawa haya si chochote bali ni kuendeleza biashara ya makampuni makubwa ya dawa duniani. Unaweza kutembelea tovuti yake kwa kubonyeza hapa

2Comments:

At 5:36 PM, Blogger mwandani said...

hii habari ya ukimwi inanichanganya. Watu wanaanguka na umeme, sikatai. kila mmoja pengine hivi sasa anamjua ndugu au rafiki aliyeondoka na ukimwi.
Kama swala ngono mboni ughaibuni ngono inaendelea bila makunyanzi, lakini takwimu za ukimwi zinaongezeka kwa uchaache tu, na watu wakijikwaa wanapata sana sana gono.
nimemsoma huyo daktari na makala nyengine nyengine,ndio nashangaa, vitamini zinaongeza maisha kuliko sumu za viwandani...
Basi mwenye siko la kufa haidhuru akajaribu njia nyingine zaidi ya za hao wenye viwanda vya madawa

 
At 1:34 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Hii habari nzuri sana. Tafadhali endelea kutupasha yanayojiri. Ninafuatilia kwa undani hasa baada ya kufuatilia zile habari nyingine za ukimwi ulizowahi kunipatia viungo zamani.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI