Wednesday, May 18, 2005

Sakata la CITY water

Nakuambia mambo yameiva. Hawa jamaa wa city water nani kakuambia watakubali kirahisi? Wamesema wataenda mahakamani. Nakuhakikishia hii mambo itakuwa kama yale ya TTCL. Si mnakumbuka ilianza hivi hivi kama utani. Jamaa wakagoma kutoa pesa zilizobaki. Songombingo za kisheria zikaanza. Jamaa wakavimba mahakama zote mpaka ughaibuni wakaibuka washindi. Sasa hivi wanajimwaga bado. Nasikia wataongezewa tena mkataba. Nakuapia wadanganyika tutakoma kipindi hiki. Unajua kuna watu ukiwaambia kuna wazungu matapeli watakumaliza. Watakuambia hapana, mzungu hawezi kuwa tapeli, atakuwaje tapeli wakati wao ndio magwiji na wapiga debe wa utawala bora? Hapo ndio tunapodanganywa. Tusipojihadhari tutapigwa bao lingine.

5Comments:

At 3:08 PM, Blogger mwandani said...

Utapeli hauna rangi, makampuni ya bima makubwa yamegushi hata yakaishia kuanguka, marekani, ungereza, hata huku matawi ya chini HIH nao wanakwenda jela. Mwizi mwenye tai hafi amesimama, atakufa na wewe.
Dawa ni kujitegemea. Wakati wa kubadili fikra ni huu!

 
At 10:43 PM, Anonymous Anonymous said...

kwani ngozi zao zikiwa nyeupe ndio wanakuwa hawana tamaa ya mali? Wana tamaa hasa na wanaiba kisawasawa

 
At 7:44 AM, Blogger Bakanja said...

Ni kweli kabisa,shida kubwa ni kwamba sisi waafrika tumefundishwa kutojiamini.Hakuna kinachoshindikana katika kuendesha mashirika mbalimbali ila tunafikiri siku zote kuwa ngozi nyeusi haiwezi ila ngozi nyingine.Ni kweli?Mbona Mengi anaweza?Kwa nini tunashindwa kuwapa watu kama hawa nafasi ya kututhibitishia kuwa tunaweza?Haya sasa,yanawatokea puani wanaserikali ya ccm.

 
At 10:48 AM, Blogger Martha Mtangoo said...

Huyo Sitti na Huyo Wotta tulianza kuwashtukia kabla hawajaanza hata kutambaa lakini kama ilivyo kawaida babu akawatetea kuwa hao wakikua ndio watakuwa watulivu kupita kiasi, nadhani babu alisahau kuwa lisemwalo lipi na kama halipo laja na kama linakuja lipo kwenye kona linachungulia ngoja tuwaone akina Netto na Grupo ambao babu kasema wakishirikia na huyo mwenzao Solusheni wanakua vizuri. ngoja tuwasubiri tuone.

 
At 6:40 PM, Blogger Reggy's said...

site wota watajiju: lakini tusiwalaumu wenyewe peke yao. Yuko wapi aliwaleta?
Alitumia vigezo gani kuwapima na kuutangazia ulimwengu kuwa wanafaa sana na leo anabadilika na kusema hawafai?
Kwa nini anaunda kampuni nyingine ya DAWASCO badala ya kuiboresha DAWASA ili iendelee kufanya kazi hiyo.
Kwa nini Dawasa ilikuwa haipewi pesa za kutosha lakini walipopata mkopo wa sh bilioni 162 wakaiita site wota badala ya kuiwezesha Dawasa? hayo si ndiyo ya TANESCO, ilipokuwa na wazalendo walikuwa wanalipwa si zaidi ya sh laki 8 kwa mwezi, lakini wale wasauzi wa Net Group Solutions wanalipwa mamilioni, kwa nini wasingelipwa wazawa wakafanya kazi hiyo?

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI