Monday, May 16, 2005

Hivi Angola inauza wapi mafuta yake?

Afrika kweli kiboko. Mimi najiuliza ni wapi Angola inauza mafuta yake? Hii ni nchi ya SADC lakini sijuhi kama kuna nchi inayonunua mafuta toka Angola. Wengi wanaagiza uarabuni. Jumuiya kama SADC inafanya nini sijuhi kupunguza hali hii ya utegemezi wa kununua bidhaa zinazopatikana kwenye moja ya nchi za jumuiya toka nchi za mbali. Na usione ajabu Angola ikawa inaagiza mafuta toka nje kama inavyofanya Nigeria. Inauza Mafuta ghafi halafu inanunua yaliyosafishwa. Kweli safari ya Afrika bado ni ndefu!!

1Comments:

At 2:23 PM, Anonymous Anonymous said...

Mimi nakwambia tangu Malkia Nzinga Mbande aondoke mambo yamekuwa yakienda mzaba mzaba tu.


Da Mija.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI