Thursday, June 02, 2005

Kimya kingi

Nimekuwa kimya kwa muda mrefu sasa. Nilibanwa sana na bado nimebanwa. Nilikuwa nasubiri kwa hamu matokeo ya kura ya maoni kuhusu katiba ya umoja wa ulaya yaliyofanyika ufaransa na uholanzi. Matokeo yake nadhani mmeyasikia watu wamekataa. Niliandika makala kuhusu jumuiya ya afrika mashariki siku nyingi lakini sikuitundika kwa vile nilikuwa nangojea kura hizi. Nitaitundika baada ya kuweka machache kuhusu matokeo ya kura ya ufaransa na uholanzi.

1Comments:

At 6:31 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Ule muungano wa afrika mashariki ni wa viongozi au wananchi? Watawala wanapokutana na suti zao na kuweka saini mkataba wa kuungana ina maana kuwa Obo, Otieno, na Masatu wameungana? Kuna somo kubwa sana tunapata toka umoja wa ulaya. Nadhani uchambuzi wako utatoa mwanga.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI