Friday, July 22, 2005

Mambo ya blogu

Leo Ethan alitoa shule kuhusu "Community Blogging". Lilikuwa somo la nguvu sana. Washiriki walikuwa na furaha na wengi wamehamasika kuanzisha blogu zao na kuanzisha jamii yao ya mtandao wa blogu. Mimi nilizungumzia kidogo kuhusu blogu za Kiswahili; tunaandika nini, ni nani wanaandika nakadhalika. Wengi walifurahia jinsi ambavyo watanzania wanachipukia katika ulimwengu huu wa blogu na jinsi ambavyo wengi wetu tunavyojadili mambo yahusiyo nchi yetu, na ulimwengu kwa jumla kinyume na baadhi ya wanablogu wa nchi nyingine ambao huzungumzia mambo yao binafsi, familia na rafiki zao. Changamoto kubwa waliyotupa ni je ni nani anasoma tunayoaandika? Tutahakikishaje kwamba mawazo yetu yanasomwa na watu wengi zaidi? Hili ni jambo la msingi na inabidi wanablogu wote tubunge bongo kuhakikisha tunasomwa na watu wengi zaidi hasa wale ambao hawana "internet". Tujadiliane kwa hili kurahisha ufikishaji wa ujumbe kwa jamii. Lazima nikiri kwamba Ethan ni mtu muungwana, mpenda mijadala na mhamasishaji mzuri anayeweza kukufanya ukawa na blogu hata kama ulikuwa huna mpango wa kuwa nayo. Anaijua Tanzania kiasi pia, ameniambia ameshakuwa Dar mara kadhaa na ametembelea Zanzibar na Mikumi. Tuongeze bidii sauti zetu zitasikika.

4Comments:

At 3:08 PM, Blogger mwandani said...

Changamoto kwelikweli. katika chombo hiki wengi huandika kwa haraka. Tukita tusomwe na wengine kwenye vyombo vya kuchapa kama magazeti, changamoto inazidi kwani inapasa kueleza kwa makini. Tutulize akili.

 
At 4:16 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Aisee asante kwa taarifa hii. Nimerudi. Tutawasiliana zaidi kuhusu masuala uliyogusia hapa na pia kuhusu swali ulilouliza kama wanablogu wanafanya uandishi wa habari. ngoja kwanza nisome mambo maana niko nyuma. Ila mbele kwa mbele...

 
At 2:00 PM, Anonymous Mary said...

Asante kwa taarifa hii nzuri, yatupasa tujue kiundani.

 
At 2:03 PM, Anonymous Anonymous said...

Hii taarifa yapendeza kweli kweli.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI