Wednesday, August 17, 2005

Taifa Moja Nchi Mbili


Niliposoma takwimu za umiliki mali na mapato kati ya weupe na weusi Afrika ya Kusini nilishindwa kuamini. Katika takwimu hizo mwandishi alisema kwamba, kama ukiigawa Afrika ya Kusini kama nchi mbili tofauti; moja ikiwa ya wazungu ambao ni asilimia 14 na nyingine ikiwa ya weusi asilimia iliyobaki na ukitumia kigezo cha shirika la maendeleo la umoja wa mataifa –UNDP cha maendeleo ya watu (Human Development Index) ambapo nchi hupangwa kuanzia ya juu kabisa mpaka ya mwisho basi sura itakuwa hivi:
Taifa la wazungu asilimia 14 wanaomiliki asilimia 88 ya mali binafsi (Private Property) litashika namba ya 24 likiwa hatua moja chini ya Uhispania
Taifa la weusi ambao zaidi ya nusu wanaishi kwa kipato cha dola moja kwa siku, na asilimia 40 ya watoto wakiwa wamedumaa kwa utapiamlo litashika namba ya 123 likiwa juu ya Congo hatua moja. Hii inaonyesha ni jinsi gani pengo la walio nacho na wasio nacho lilivyo kubwa.
Nilianza kwa kusema sikuamini hizo takwimu kwa sababu ya picha ya mwanzo niliyokuwa nayo ya sehemu za katikati ya miji ambapo kuna barabara nzuri, nyumba nzuri, mahoteli makubwa, magari ya kifahari na vinginevyo. Sasa nimeamini. Nilishiriki katika utafiti wa maeneo mbalimbali ya Cape Town siku za karibuni tukiwa tunatafiti shule za Msingi. Acha utani. Maeneo wanayoishi weusi ndani ya hili jiji zuri yanatisha. Vijumba vingi ni vya mbao na mabati kote. Msongamano wa ajabu. Shule zao utaziona ziko hoi kabisa. Ukilinganisha na hizo za wazungu utazimia. Za wazungu zimesheneza acha utani. Kila kitu kipo darasani. Wanafunzi utaona tofauti zao za kuelewa mambo kabisa. Si kwamba weusi ni wajinga ila mazingira yanawafanya wasiweze kuwa kama wenzao. Tembea uone. Hapa ni mjini bado sijaenda huko vijijini nijionee.
Gazeti moja hapa siku za karibuni limetoa takwimu za kusikitisha. Inasemekana kwamba kwa sasa wanafunzi 3.6 milioni hawana viti vya kukalia na wengine milioni 4.2 hawana madawati yanayofaa kuandikia (hakuna mweupe hapa). Lakini ukiona maisha ya mijini huwezi kuamini kabisa. Kwa mtaji huu si kwamba kuna watu tofauti tuu katika nchi hii, bali pia hizi ni dunia mbili tofauti kabisa.

3Comments:

At 5:22 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mfumo wa uchumi na kijamii ambao umeunda nchi mbili ndani ya taifa moja ndio ambao sisi tunaung'ang'ania tukiamini kuwa ndio jibu la matatizo yetu. Sio hilo tu, bali hata hao jamaa asilimia 14 tumeamua kuwapa nchi yetu wafanye watakalo.

 
At 6:08 PM, Blogger Indya Nkya said...

Kwa kasi yetu tutakuwa na taifa moja lenye nchi tatu: weupe wanaopewa kila kitu asilimia 2 pengine wanaomiliki asilimia 70 halafu weusi wezi wanaoshiriki kwenye mnada wa nchi asilimia 1 watakamiliki asilimia 27 na asilimia 97 ya walala hoi wengine weusi watakaomiliki asilimia 3

 
At 7:32 PM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

ni kweli unachosema kaka kuwa kuna utofauti katika maisha ya afrika ya kusini na tanzania. hata hivyo ukichunguza kwa undani, sababu kubwa ilikuwa ni ubaguzi wa rangi. sasa basi wote tukiwa tumekabiliwa na changamoto la kufuta unmasikini utakuta Tanzania hatujui tuko wapi, na tunatakiwa tufanye nini. mfano, hata ukipitia ripoti za UNICEF au WHO Tanzania iko kwenye list ya hali mbaya kabisa kilishe! south afika haiko kwenye upande huo japokuwa kuna masikini! mfano mwingine ni kwa wenzetu huku kusini, mathalani msomi au mtu anayetoa huduma kwa jamii kihalali hafanywi kama wale madaktari wetu wa tanzania (muhimbili). yaani chini ya ulimwengu wa afrika kusini unakula jasho lako na si vinginevyo! tanzania anayevuja jasho hali asiyevuja jasho anakula!! mtu ni mzee anapewa pension ya rand 1000 kwa mwezi! yaani ninachosema hapa ni kuwa hawa jamaa wamekubali kulikuwa na tofauti na wanaganga ujao! kizuri wanaelezwa ukweli! kitu ambacho HATA KUKICHA NINACHUKIA VIONGOZI WETU PALE BONGO hawatendi wanavyohubiri! au kwa lugha rahisi wanatenda kinyume na wanachohubiri! hivyo utakuta mtu analazimishwa kuishi tofauti na impasavyo! hakuna kwenda mbele sana sana kurudi nyuma! afrika kusini asilimia 60 % wako mjini! na iko wazi kuwa tatizo ni kupata kazi ukipata kimeeleweka! tanzania hata ukipata kazi bado ni kasheshe! sijui kama nimnaeleweka kirahisi. ni kwamba siku zote huwezi epuka kuwepo tajiri na anayemtumikia tajiri, lakini kama wote wanapata mahitaji yao ya msingi (kwa haki kama raia - hakuna taabu!). kitu ingine ni kuwa mfano mazingira ya siasa ya kwao na sie ni tafauti! hukuti mtu anamwogopa mbeki, na mbeki huwa na heshima sana akikutana na watu,kwa sababu watu hawachelewi kukubadilikia ukichemsha! katika tanzania toke na ukweli kwamba nchi yetu ni kanisa hatuwezi wala kudhubutu kumwambia katibu kata hapo umekosea!

aksante ,

mark

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI