Thursday, August 04, 2005

Uajua hili?

Mnamo mwaka wa 1960, Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikuwa na hali nzuri kwa zaidi ya asilimia 50 ikilinganishwa na Taiwan, lakini kufikia mwaka 2000, kibao kilikuwa kimegeuka kabisa kwa Taiwan kuwa tajiri mara 17 ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Tukiweka tarakimu ili ieleweke kirahisi ni kwamba; mwaka 1960 kipato cha wastani kwa mwananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kilikuwa Dola za Marekani 2,180 wakati cha Taiwan kilikuwa Dola 1430, mwaka wa 2000 kipato cha kila Mtaiwani kilipanda na kufikia dola 18,700 wakati cha Mwanaafrika ya kati kilishuka na kufikia dola 1,120. Hali si tofauti sana ukilinganisha kwa mfano Malaysia na Ghana ambazo zote zilianza kwa kipato kinacholingana mwaka 1960 na zote zikiwa zinategemea sana kilimo, kadhalika unaweza ukalinganisha Nigeria na Indonesia zote zikiwa wazalishaji wa mafuta. Nitajaribu kuandika kwa lugha rahisi sbabu za maajabu haya. Kwa vyovyote unaweza kwa sasa ukachukulia tuu kwamba Afrika tuna kile ambacho tunatumia kujifariji na kuhalalisha uzembe "bahati mbaya" wakati wenzetu wana kile ambacho huitwa "bahati nzuri." Au tuite mkosi kwa Afrika? Sijuhi. Ngoja nitafute muda nichambue sababu ambazo zimekuwa zikitolewa kwa pengo hili.

7Comments:

At 2:47 AM, Anonymous Anonymous said...

Tumelaaniwa nini Nkya? Labda laana ya Nuhu hiyo!

 
At 2:47 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Lazima laana walahi.

 
At 1:56 PM, Blogger Indya Nkya said...

Lazima tutafute chanzo cha hii laana vinginevyo tumekwisha

 
At 6:02 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Kweli Nkya. Napenda upanue zaidi mchanganuo huu.

 
At 10:37 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Nasoma kitabu cha Fareed Zakaria kinaitwa the Future of Freedom. Kuna mahala anazungumzia uhusiano wa maendeleo na utamaduni. Anamnukuu jamaa mmoja aliyesema kuwa ukitaka kuendelea ni vyema uwe na utamaduni wa kiyahudi, kichina, na kihindi. Je ni kweli utamaduni una nafasi kubwa katika kufanya jamii iendelee?

 
At 3:13 PM, Blogger kivale said...

Inawezekana ni mila na desturi zetu ndizo zinazochangia kutokuwepo na maendeleo

 
At 11:39 AM, Anonymous Anonymous said...

Nitachambua kwa undani suala hili, pamoja na utamaduni ukiwemo

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI