Tuesday, October 04, 2005

Ugunduzi mpya huwa mgumu kukubalika

Jana nilielezea washindi wa tuzo ya Nobeli katika Utibabu walivyogundua kwamba vidonda vya tumbo kwa asilimia kubwa husababishwa na bakteria na matibabu yake ni rahisi yaani kutumia "antibiotics" tuu. Hawa jamaa walianza utafiti wao miaka 20 iliyopita. Walivyotangaza mara ya kwanza walichekwa sana na kuonekana ni watu wanaotaka kuleta mzaa katika sayansi. Leo ukweli umedhihirika lakini baada ya gharama kubwa ya maisha ya watu pamoja na dawa za kutibu vidonda hivyo zinazouzwa na kampuni za mabepari. Hili si tukio la kwanza; miaka mingi iliyopita ugonjwa unaoitwa "Scurvy" ulikuwa ukiwasumbua sana watu. Akajitokeza mwanasayansi mmoja akasema watu wasihangaike; tatizo la ugonjwa huo ni ukosefu wa vitamini C. Alichekwa vibaya sana. lakini baadaye ikadhihirika kwamba ugunduzi wake ni ukweli mtupu. Sasa hivi kuna mtaalam mmoja anayeitwa Dr. Mathias Rath; anapambana na mambo mawili makubwa. Kwanza anasema magonjwa ya moyo husababishwa na upungufu wa vitamini C. Anauliza kwa nini wanyama hawapati magonjwa ya moyo lakini sisi binadamu tunayapata? Jibu ni kwamba miili ya wanyama inazalisha vitamini C ambayo ni muhimu katika kuzuia matatizo ya moyo wakati miili ya binadamu haina uwezo huo. Kwa maneno mengine tunahitaji vitamini C za kutosha toka kwenye vyanzo vingine. Jambo la pili analopambana nalo ni matumizi ya vitamini na virutubisho katika kupambana na UKIMWI. Katika mapambano haya anakumbana na upinzani wa kutisha. Upinzani uliogeukia majukwaani badala ya maabara. kampuni za dawa hazitaki kusikia dawa mbadala kabisa. Wanataka kuendelea kuuza dawa zao.
Nimalizie kwa kutoa nukuu hii: "New Truths go through three stages. First they are ridiculed, second they are violently opposed and then finally, they are accepted as being self-evident". Arthur Schopenhauer

3Comments:

At 10:30 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Kaka,
Ujumbe wa maana sana huu.Nimewahi kusema kwamba mwili wa binadamu una kila aina ya kinga ukitumiwa na kutumikiwa vizuri.Ni muhimu watu wakajua kwamba dawa ni biashara kama zilivyo siasa za siku hizi.

 
At 5:16 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Napenda sana ulivyoshikia bango suala la utata wa ukweli juu ya ukimwi. Lakini pia umeongeza tofali jingine kwa mfano huu wa vidonda vya tumbo na "scurvy." Na nukuu kuhusu hatua tatu ambazo kweli hupitia. Siri moja imefichuka majuzi kuhusu makampuni ya madawa. Kumbe eti kila mwisho wa mwaka madakitari hupewa fedha na tiketi za kwenda mapumzikoni na kampuni za madawa. "Zawadi" hizi hupewa wale madakitari ambao wamewandikia wagonjwa dawa za makampuni haya kwa wingi. Sasa Nkya unadhani kama mtu unajua kuwa ukiwaandikia wagonjwa dawa nyingi utapewa "zawadi" unadhani utakachofanya ni nini? Kila anayekujia unamtundika dawa hata kama hahitaji! Kingine ni kuwa kampuni za madawa ndio huchangia fedha vyuo vikuu vya utabibu kwahiyo wanafunzi wa utabibu wanakuwa wanafundishwa jinsi ya "kuuza" dawa za makampuni hayo. Bepari achana naye kabisa.

Hivi scurvy ni beriberi??

 
At 10:43 AM, Blogger Indya Nkya said...

Sina uhakika na scurvy kama ndiyo Beriberi. Nitachimba. Umenipa changamoto kuhusu kuandikia wagonjwa dawa na kupata tiketi ya mapumziko. Nitaandika makala kabisa. Niliwahi kugusia hili kwenye makala yangu moja. Hii uliyosema kwa kiingereza inaitwa Supply- induced demand. Yaani daktari anakuandikia dawa ambazo si muhimu kwa vile wewe huna elimu yoyote kuhusu ugonjwa wako. Nitaiandikia makala kabisa ili ieleweke.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI