Monday, October 10, 2005

Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Tarehe 14/10/2005, itakuwa imetimia miaka sita tangu Mwalimu Nyerere atangulie mbele ya haki. Katika kumuenzi na kumkukumbuka mzee wetu huyu, Chuo Kikuu cha Cape Town kwa ushirikiano na Jumuiya ya Wanafunzi wa Afrika mashariki wanaosoma Chuo hiki wamendaa mhadhara Maalum wa kumbukumbu kutafakari mchango wake kama kiongozi, mwanafalsafa, mwanazuoni na mpigania uhuru na haki za wanyonge katika bara la afrika na duniani kote. Mgeni Rasmi katika tukio hili atakuwa Prof. Haroub Othman wa chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam. Katika tukio hilo tunatarajia tutakuwa na wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali hapa Afrika ya Kusini na wawakilishi toka balozi mbalimbali. Huu ni mhadhara wa kwanza kuandaliwa na chuo hiki na ni nia yetu kufanya tukio hili liwe la kila mwaka. Nitazidi kuwafahamisha zaidi juu ya tukio hili.

9Comments:

At 5:24 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Tupe zaidi juu ya hili, hasa nasaha za Haroub na wengine. Pia kama kuna kiungo cha webu.

 
At 10:36 AM, Blogger Indya Nkya said...

Nitabandika pia makala nilizoandika kuhusu tukio hili na mawazo yangu kuhusu fikra za mwalimu

 
At 1:42 PM, Anonymous Anonymous said...

Sijui itakuwa vipi?. wataongelea mapungufu yake?. nimekuandikia kabla sijaona hii nakala.
Nilisoma kitabu kimoja watu wa SWAPO waliongelea 'Tanga consultation conference',nimesahau ulikuwa mwaka gani, mkutano huu walikaa usiku kucha, asubuhi wakatoa tamko wanahamamisha makao makuu yao toka DSM kwenda Lusaka sababu lusaka ni karibu sana na 'frontline' hivyo wanasonga mbele!. Lakini wengine wakasema 'ukweli' eti sababu Nyerere alikabidhi wafuasi wawili wa SWAPO kwa utawala wa pretoria, wa Botha yule mbu, akijua kuwa watanyongwa, hivyo kumuadhibu na yeye ni kuhama dsm.
Jaribu kufuatilia hili.
Mloyi.

 
At 1:20 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Kila la kheri kwa tamasha kama hili.Hivi lakini leo hii tuna viongozi kama kina Nyerere na wenzake kweli?Nyerere alikuwa ana mapungufu yake kama binadamu wote.Tunachotakiwa ni kuweka kwenye mzani tuone kati ya mapungufu na nia njema nini kilizidi mwenzake.

 
At 9:36 AM, Blogger Indya Nkya said...

Hili la SWAPO nimesema kwa vile kina Sam Nujoma wapo hai wataweza kuulizwa tusifuate hisia. Mimi nikienda Namibia nitafanya niwezelo niweze kuongea na SAM

 
At 9:45 PM, Blogger boniphace said...

Kituko hicho kweli Mungu aache kuwatafuta maskini amfate George Bush ikulu Marekani?

 
At 2:41 PM, Blogger Rama Msangi said...

Ni kweli Nyerere kama Nyerere alikuwa na mapungufu yake lakini kwa mtizamo wangu binafsi, kila alilokuwa akilifanya alikuwa akilifanya kwa dhamira njema. Unajua mtu anaweza kuwa anawaza jambo zuri lakini akalitekeleza kwa ubaya, afadhali ya huyu kuliko yule anayewaza baya akijifanya anatekeleza zuri

Nasubiri kwa hamu kujua maongezi yako na Sam yatatoa muafaka gani kuhusu hoja iliyoko hapo juu

 
At 8:00 PM, Blogger Indya Nkya said...

Mhadhara umefanyika. Umekwenda vizuri sana. Prof. Amemwelezea vizuri san Mwalimu. mahudhurio yalikuwa mazuri sana. Balozi wa Rwanda ametuma ujumbe mzito ambao umesomwa kwenye mhadhara huu. Nitaweka paper yote ya Prof. baadaye

 
At 9:26 AM, Anonymous Anonymous said...

Ninaomba kuwaulizeni na tena ninaomba jibu la kina. Ikiwa kama Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa na sifa zote hizi kwa nini hakuandika (autobiography) au hakuandikiwa (biography) shajari ya maisha yake?

Nasubiri majibu yenu,
F MtiMkubwa Tungaraza.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI