Thursday, October 13, 2005

Chavez kawashitukia wamisionari

Rais wa Venenzuela Hugo Chavez ambaye ni adui mkubwa wa Marekani ameshtukia wahubiri toka Marekani na ameamua atawatimua sasa. Chavez ambaye Marekani inashinikiza kuondolewa kwake madarakani anahisi wahubiri hao ni wale wale wapiga propaganda za adui wake. Soma hapa ujionee mwenyewe.

5Comments:

At 11:59 AM, Anonymous Anonymous said...

Matt Asay joining as regular contributor to Open Resource
In an attempt to bring a bit of intellect to this blog, Matt Asay will be joining me here as a regular contributor in the very near future.
Find out how to buy and sell anything, like things related to private road construction on interest free credit and pay back whenever you want! Exchange FREE ads on any topic, like private road construction!

 
At 12:48 PM, Blogger mwandani said...

Huyu ni ngangari. Soma mahojiano yake alipokuwa New York wakati wa mkutano wa umoja wa mataifa. Ndani ya nchi ya wanaomtesa.Fuata kiungo hichi ufurahi.

http://abcnews.go.com/Nightline/print?id=1134098

 
At 2:12 PM, Blogger Innocent said...

Kweli huyu bwana ni ngangari lakini sijui kama atafanikiwa.Si unajua tena hakuna umoja duniani.Angalia Mugabe mambo yamekwenda kombo na sasa kachanganyikiwa kabisa.
Ila nataka tuanzishe mjadala juu ya hawa mabwana wawili: Mugabe na Chavez, je ni wanamapinduzi wa kweli wanaotakiwa ktk dunia ya leo?

 
At 2:19 PM, Blogger msangimdogo said...

Kwanza pole kwa hilo tatizo la hivyo viunganishi ambavyo Bw. rsmiruko alishalizungumzia kwake. Kuhusu huyu bwana, mimi naona ni kama enzi za akina Mkwawa na kina mangi wote. Waliwashtukia jamaa lakini wapi bwana, huwa wanamwaga kirusi cha kutokuungana mkono kwenye maafa ili iwe rahisi wao kuingia. Akazane lakini huenda akashinda

 
At 6:57 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mwandani asante kwa kiungo hicho cha mahojiano ya Chavez.
Nkya,
wamisionari...hawa si ndio walikuja hadaa afrika ili wakoloni wapate urahisi? Kwanza hii tabia ya kutaka kubadili kila mtu duniani ili awe na imani hizi mbili "kuu" za kuja huwa inanitia kichefuchefu. Nani kawaambia hawa wamisionari kuwa makabila wanayohubiria huko Venezuela vijijini hayana imani ya kweli? Sijui kwanini Chavez hakuwapa masaa 24.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI