Wednesday, October 26, 2005

Sawa si sawasawa tena

Fide aliuliza binadamu wote ni sawasawa? Macha sasa nadhani huitaji mjadala tena. Kuna huyu mtu anayeitwa Magufuli -Waziri wa Ujenzi. Anasifika sana kwamba anachapa kazi. Lakini mgongoni mwa huo uchapa kazi ana mambo ya kusikitisha mno. Soma hapa uone moja ya mambo yake mengi ya ajabu.

2Comments:

At 12:28 PM, Anonymous Anonymous said...

Habari za leo? Nimekatiza tena kwenye kiwanja chako na kukutana na hili suala ambalo jana (Jumatano 26.10.2005)tulilijadili sana na swahiba wangu mpendwa Dennis Mavuto Londo (dennislondo@yahoo.com). Baada ya majadiliano nilimuacha Bwana Mavuto aendelee na ujenzi wa taifa.

Kumbe nilivyomuacha Bwana Mavuto akaendelea kulifuatilia suala hili kwa kuwasiliana na Waheshimiwa Watanzania kadhaa wanaojua mambo kwa undani. Jioni akanifuata kibanda-umiza nilipokuwa nikisaga manoti na kujitia ugonjwa wazimu.

Taarifa aliyonipa ilikatisha raha yote ya bia. Ndugu yangu, hili suala linasikitisha, kukarahisha na linaumiza ukijua undani wake zaidi. Kwa ufupi tu ni kwamba hawa Waheshimiwa wa serikali ya awamu ya tatu wameamua wao kwa wao, kuuziana wao kwa wao, mali zisizo za kwao,kwa utaratibu wala siyo sheria walioupanga wao,na kwa bei walizozipanga wao!

Nina hakika ipo siku kuna Mtanzania atataka hizi mali zirudi kwa wenyewe. Ndiyo hapo utakapoanza matafaruku kati wadai na Waheshimiwa hao.

Mungu Ibariki Tanzania.

Watakabahu, ni mimi maridhiya,
F MtiMkubwa Tungaraza.

 
At 2:09 PM, Blogger Indya Nkya said...

Huo ndio ukweli Fide. Mnunuaji anachagua halafu anapanga anachotaka kulipa. Ni kweli hiyo Nyumba nasikia anaitaka Sarungi. Na magufuli huwa ni mropokaji. Na hapa karopoka. Kwamba; kama huyo bwana anataka kuwa kigogo akagombee. Ukigogo ni kugombea. Sijawahi kutokuwa na matumaini kama yako. Mzalendo atatokea kama si leo ni kesho. Hata keshokutwa. Atataka vya wenyewe virudishwe kwa wenyewe.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI