Wednesday, November 09, 2005

Wanywaji wa Kahawa Huree

Tafiti zinachanganya Kweli. Tofauti na inavyoaminika kwamba kunywa kahawa kwa wingi husababisha Magonjwa ya moyo, utafiti mpya umegundua kwamba unywaji wa Coca Cola unaweza kuwa hatari zaidi. Soma hapa

3Comments:

At 9:24 PM, Blogger Innocent Kasyate said...

Yaani nakwambia mimi ni mnywaji mzuri sana wa kahawa na sijawahi kuona madhara.Hapa sasa hivi niko ninajisomea na ni kikombe cha 4 lile mug kubwa huwezi kuamini.
Lakini isije ikawa ni mambo ya kuvutia biashara, bado siwaamini sana hawa wamarekani.

 
At 1:02 PM, Blogger Indya Nkya said...

Ni kweli kuna sababu ya kutowaamini kabisa. lakini kuna kitabu kimoja ambacho bado naendelea kukisoma kinauliza; Why Human being get Heart Attack and Animals Dont? Kimeandikwa na Dr. Mathias Rath. Hoja yake ya msingi ni kwamba magonjwa ya moyo husababishwa na ukosefu wa Vitamin C. Wanyama wana uwezo wa kutengeneza vitamin hizo ndani ya miili yao. Sisi binadamu hatuwezi inabidi tuzipate nje. Sasa kwa vile tunakosa sana vitamini ndiyo maana hupata magonjwa hayo. Mimi biashara ya dawa naigopa sana. lakini ukiangalia jamaa waliopata Tuzo ya Nobel katika utabibu mwaka huu walifanya utafiti na kugundua kwamba vidonda vya tumbo husababishwa na Bacteria na si kama tulivyoaminishwa miaka yote. Kwa hivyo kuna mambo mengi ndugu yangu.

 
At 10:02 PM, Anonymous Anonymous said...

Hello, my name is anira. I'm in Poland/Europe.
Can you help me to translate this sentence?:

NAMI JEURI NAIJUA LAKINI NAIGOPA DUNIA

Can You help me? Can you write me at
anirawojan@tlen.pl

BEST REGARDS

anira

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI