Friday, November 11, 2005

Tanzania yaingizwa kwenye kapu la Misaada mingine ya Marekani

Tanzania imefanikiwa kuingizwa katika mpango wa misaada wa Marekani unaoitwa Millenium Challenge Corporation (MCC). Ili uingizwe humo ni lazima kwanza uwe na utawala bora kwa vigezo vya jamaa wa Benki ya Dunia na Wizara ya Fedha ya Dunia (International Ministry of Finance), wenyewe wanaita International Monetary Fund. Sasa tungoje majivuno na matusi toka kwa mwenyewe. "Wale wote mnaosema nchi haina utawala bora ni vipofu. Hamuoni hata Marekani inatambua? Nyie watanzania msioona ni watu wa ajabu sana". Tutayasikia haya karibuni. Soma Hapa habari hiyo.

4Comments:

At 9:19 PM, Blogger Innocent said...

Kama unavyojua brother,hapa ndio tumekwisha.Hawa wazito wa benki ya dunia ndio watawala wa dunia.Na wanasiasa wetu( Mkapa na marais wenzake wanafyata mkia; hapa sio rais kwa maslahi ya wananchi ila wakubwa wa majuu.
Tumekwisha yaani ni lazima tumridhishe mkubwa ndio tuendeshe nchi?

 
At 4:17 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Kama aliyesema kuwa nchi yetu ina utawala bora ni mzungu lazima wote tukubaliane naye. Unajua wazungu wana akili sana kutushinda!

 
At 6:25 PM, Blogger Indya Nkya said...

Nilifikiria Macha ulivyo mbishi ungebishana na hilo. Mzungu kasema bwana!! Nakubaliana na wewe.

 
At 12:36 PM, Blogger Fikrathabiti said...

Nimecheka sana Nkya kwani uliyemnukuu nadhani ni Mheshimiwa BENNY!

Hakuna jipya katika hilo kwani ni yapi mpaka sasa yamefanikiwa kutoka kwenye AGOA-African growth opportunity act.Hizi kwangu ni kama kelele tu zibadilishwazo milio.

Nadhani sasa tuanze mijadala ya hizi Bilateral cooperations kati ya nchi yetu na hao wajiitao wahisani wasio na Hisani

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI