Saturday, December 17, 2005

Igizo limeisha, tungoje miaka mingine mitano

Mchezo wa kuigiza umekwisha. Miaka mingine mitano wananchi watalishwa tena maneno, pilau, khanga, sukari watauza tena kura zao. Mchezo unaendelea. Lakini mchezo huu utaendelea hadi lini? Na watanzania tulivyo hatutawauliza wale walioshinda chochote hata kama hawatatimiza moja kati ya walioahidi. Lakini hata hivyo ni wangapi tunakumbuka hata ahadi zenyewe? Pilau na khanga na fulana zinatosha. Jamaa mmoja kaniacha hoi sana. Ameniambia jinsi ambavyo bado kuna kibarua kigumu mbele yetu. Alishuhudia watu wakibishana baada ya kampeni. Hawakubishana chochote kuhusu yaliyozungumzwa kwenye mkutano wa kampeni. Ubishi ulikuwa juu ya vifaa na magari ya vyama vyao. Mmoja akiwa anasema umeona spika za chama chetu? Ni nzito bwana si mchezo. Mwingine akamwambia acha utani, uliona gari walilokuwa wakitumia wagombea wa chama changu walipokuja hapa? Kazi ipo. Kwa kweli kama tunataka mabadiliko inabidi tusilale usingizi. Tupambane kweli.


14Comments:

At 11:00 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Nadhani wanasiasa wetu wanapaswa kupewa vyeti vya uigizaji bora toka chuo cha sanaa Bwagamoyo.

Ubishi huo unasikitisha. Watu wanabishana mambo ya ajabu kabisa. Eti spika za chama babu kubwa...mtoto wako atakapokuwa anakwenda shule yenye wanafunzi 137 darasa moja na mwalimu mmoja ambaye anafikiria biashara yake ya mtumba ili aongeze kipato chake...sijui spika itasaidia nini.

We ngoja.

 
At 1:20 PM, Blogger mark msaki said...

kwa kweli hata mimi ninasikitika sana kujifunza kinachoendela katika kanisa la tanzania. kuna huyu bwana ameandika makala yake hapa
http://allafrica.com/stories/200512170032.html

kuhusu dosari za maana tu ambazo zinatosha kuufanya uchaguzi kutokuwa huru na haki. sikuamini niliposoma kuwa kuna mamilioni walinyimwa haki ya kupiga kura mikoani!! nikasoma kwa huzuni pia kuwa eti pale kigamboni kuna wanachama wa upinzani walifuatwa nyumbani kwao na kuzuiwa wasiende kupiga kura JAMANI!!! tumeona inspekta mahita alizuia watu wa zanzibar wasirudi kwao kupiga kura kwa kuzuia safari za meli kati ya unguja na dar siku mbili kabla ya uchaguzi eti ili waweze kulinda vizuri!!! tunaona kuwa mamia ya wanajeshi walio hata kwenye mafunzo walisafirishwa kwenda unguja kupiga kura! tunaona wananchi waliambulia kipigo toka kwa polisi pale walipozuia sura ngeni na mamluki kupiga kura!!! tunaona jinsi matumizi ya nguvu ya ziada yalivyokuwa kwenye uchaguzi hata huko unguja!! mimi swali langu ni kuwa kwa habari hii ya mamilioni kunyimwa kupiga kura? si ndio imeua haki ya watu kuamua? kwani kura za ubunge zi huwa ni elfu kadhaa tuu?? mimi niadhani ukifuatilia kwa ukaribu hawa walionyimwa kupiga kura walijulikana kabisa kuwa msimamo wao ni upi kwa kifupi "SIO WENZETU"!! MIMI NINACHOOGOPA NI KUWA KWA MFUMO HUO WA KUENDEKEZA UENZETU KWENYE UCHAGUZI SI UTAENDELEA KUATHIRI MWENENDO MZIMA WA SEREKALI MPYA?? JAMANI HATA KAMA MIMI CCM HAYA MENGINE SASA SI SAHIHI!!! YANABOA!! PROFESA OTHMAN alisema kuwa tatizo ya tanzania ni kujeshisha siasa!! ambayo ni hatari sana!! sio tu hivyo bali hata kwenye utendaji wa kazi au biashara! wakikujua kuwa wewe SIO MWENZETU BASI KUNA HATARI ya kuachishwa kazi, kutopanda cheo au kufungiwa biashara!! - lakini sasa tukae chini na kufikiri, dr. salmin kaanzisha kimbembe unguja sasa kuwa muungano ni kazi ya kwanza ya raisi!! mimi ninamuunga mkono kuwa ule muda wa kutawaliwa na MAWAZO YA MTU MMOJA YAMEKWISHA! wakati huo huo kutafakari matokeo kuwa ikiwa tatizo liko kwenye viongozi wa kambi ya pili au wananchi wenyewe basi yaanze kushughulikiwa mara moja kuzuia serekali isishushe wavu wa mbu kabisa! - pia tusikadirie chini ya uwezo wa kura zaidi ya milioni ambazo hazikupigwa JAMANI KUNA SAYANSI NYINGI TU HAPA!!!

 
At 4:56 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Wandugu,
Tuanze kutokulia tu na kuacha jahazi lipotelee baharini.Hivi sasa ukiniuliza mimi njia ni moja tu.Tushikamane na kuelimisha wenzetu kule nyumbani na ughaibuni pia.Lazima viongozi wawajibike.Ule upuuzi wa kumchagua mtu halafu anapotea kwa miaka mitano uishe sasa.Wote wenye uwezo wa kufungua blogu wafanye hivyo.Halafu tuchokonoe kila kiongozi aliahidi nini.Baada ya mwaka mmoja kama hamna ambacho amefanya basi atoke.Nakumbuka Ndesanjo aliwahi kuongelea suala la mabadiliko ya kikatiba kuanzia hapa.Ni muhimu sana.

 
At 9:09 PM, Blogger Boniphace Makene said...

Jeff na wachangiaji wengine nimewapata vilivyo. Blog ziongezeke na hii ni dira. Mwaka huu uchaguzi ulitawaliwa na magazeti kuweka viongozi. Hapo kuna madhara hasi na chanya maana ukumbuke haki ya kuzungumza kwa usawa bila woga katika Tanzania. Blog zaweza kuwa mhimili mkubwa na hili halina masihara kwani kama tukichanja mbuga kiasi hiki kuna haja tukaanza kuweka agenda za kitaifa tunazotaka viongozi wa Tanzania wafuate. Twaweza anza na aina ya Muungano na kero zake kisha tukafuata aina ya maendeleo na shemu kwa hasa mambo tunayoamini yanaweza kutekelezeka. Nisisahau kubwa ni hili na rushwamaana mtu anayeitwa Mkapa aliitangaza kuwa haki ya chama chake akaipitisha kuwa sheria.

 
At 10:19 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

NKya, nilisahau kukukaribisha maana ulituacha yatima!

 
At 11:18 AM, Blogger mark msaki said...

ndugu wanablogu!

blogu ni njia nzuri tu ya kuelimisha jamii! kanisa la Tanzania ambalo linapendelea kuwekeza katika jeshi na usalama (matumizi ya nguvu)kuliko maendeleo lilimfanya hata mgombea uaskofu kwa tiketi ya chama cha askofu mkuu mkapa kujibu maswali ambayo yalitolewa kwenye midahalo!! hivyo mgombea huyo akajicommit kutekeleza mambo ambayo ni kero kupitia njia za forum! blogu ni njia nzuri pia kuwafafamu kuwa ni nani wanamapinduzi wa ukweli na wanafikiri vipi!!- blogu pia ni njia nzuri ya kuusaidia upinzani kuwa imara, na hii ni pamoja na kubadilisha vyama vya siasa kubadilika toka kuwa makampuni binafsi kuwa VIKUNDI VYA WATU WENYE NIA YA KUCHUKUA HATAMU YA UONGOZI WA NCHI! - hii ni njia nzuri ya kuanzisha NARC kwa ajili ya 2010!!inasaidia pia kuwa chekecho zuri kwa hatima ya WAUMINI WA tanzania kubadili nchi yetu kutoka kwenye mfumo wa kanisa hadi taifa huru! katiba nayo ijadiliwe kwa kina na sera ambazo hazina manufaa zifutwe kuanzia kwenye vyama hadi serekali!!

http://www.bcstimes.com/majira/viewnews.php?category=1&newsID=6416

nina uhakika kufuatilia jinsi mwenendo mzima wa uchaguzi na uendeshaji wa vyama wako wengi tu hata wazito wtakaokatiza sakafu kutoka hata huko ndani ya chama chenye utamu ambako kumejaa (professional leaders - viongozi wa kulipwa) kwa ajili ya kutengeneza mazingira mazuri ya kukuza demokrasia tanzania!

jamani ninajua ninyi wote huwa mna marafiki ambao wako katika secta mbalimbali na adress zao mnazo! wakaribisheni mfano kupitia hii globu ya freddy macha ili watembelee na kufungua globu yao! mfano kuna hii message niliipata kutoka kwa bwana fikra mkombozi ambayo imealika watu zaidi ya 300.

Wandugu wapendwa,

je wewe ni mtu unayependa kujumuisha mawazo wako na ya wengine? unapenda ujulikane kuwa wewe ni nani, unafanya nini na una mategemeo gani? unadhani mawazo yako ni sahihi au la? je lipi ni sahihi?

karibu kwenye ulimwengu wa wanaglobu. pitia kwenye globu la bwana freddy macha

http://jikomboe.blogspot.com


ukiwa hapa utapata fursa ya kufahamiana na wana globu wengine na pia utapata shule ya kufungua blogu lako (mtandano wako)! ambalo utakuwa unawasiliana na wanaglobu wenzio wa kitanzania na wale wasio watanzania wakiwa ndani na nje ya tanzania!dunia sasa ni kijiji! global voices wametuwezesha kufikiria kwa namna moja bila kujali unatokea wapi! ruhusu mawazo na ndoto zako zikamilike! sky should be the limit!karibuni sana.mkombozi

sio mbaya: tunamshauri bwana freddy macha kama kuna uwezo aweke kiunganishi cha globu zote wa watanzania!

 
At 11:58 AM, Blogger mark msaki said...

nyerere alitumia miaka 30 kuvuruga fikra za watanzania! kile kipindi cha mazungumzo baada ya habari na moshi wa mwenge umewaathiri wengi sana sasa! ni kwa mbinu hiyo hiyo ya mawasiliano tutabadilisha mwelekeo wa gurudumu !! hata hivyo, tunahitaji kwenda kwa kasi ya roketi! nashukuru mungu kwa msaada wa teke linalokujia hilo linawezekana, LABDA KAMA KAWAIDA YAKE TUME YA MAWASILIANO IZUIE MATUMISI YA MTANDAO!!!leo hii bado wanatumia fedha nyingi kumjengea minara "sanamu za kuabudu" kama zile za stallin na saddam hussein. walisema ile ya dodoma ilijengwa na wachina kwa thamani ya shilingi milioni 100!!!achilia mbali ile ya tanga ambayo watu walilalamika kuwa haifanani naye! - ninachojiuliza ni hivi? watu wangapi wangenufaika na hizo milioni 100 angalau kama kianzio cha biashara kuliko kuweka mijisanamu ambayo itabomolewa kabla hatujafa na watoto wetu huku wengine wakiingia maabara na mafuvu yetu kuchunguza kama tulikuwa hamnazo?? kwanini kuteketeza milioni nyingi hivyo wakati milioni moja moja ingebadilisha kiuhakika maisha ya watu 100? ina maana viongozi wa kanisa letu hawatambui kabisa matatizo ya watu wao? - ninaomba pia viongozi wa vyama vya siasa wahimize wananchi kufungua globu! ni lazima wafanye hivyo ili tuwe na uwezo wa kuamua hatima ya nchi yetu!!

 
At 1:51 PM, Anonymous Anonymous said...

Nimepotea!, Tumekuwa na chama kimoja; ni malalamiko, sasa ni vyama vingi; bado ni malalamiko tu. Na kama hayo ndo matatizo ya uchaguzi, kwa nini sasa tuwe na huo uchaguzi?. Labda hatuuhitaji huo uchaguzi. Wana historia mko wapi mtupatie chimbuko ya hili dudumizi uchaguzi na mtuelimishe juu ya hili? uchaguzi ni nini? wakati hakifanyiki Saudia na maeneo ya Ghuba na hali za watu huko ni nzuri tu. Uchaguzi, nikiwa na maana ya jinsi ya kupata viongozi wetu, kwa nini huo wetu ufanyike katika misingi inayofanana na ile ya ughaibuni wakati mazingira yetu ni tufauti?. Nadhani kama ni huo uchaguzi ambao mpangilio wake na pesa za kuundesha tumepewa na tukazikubali basi tusilalamike maana hicho ndicho kile kinaitwa uchaguzi. Hatuna asili nacho na hatujui maana yake. Kwani je hapawezi kuwepo na mbadala ya uchaguzi.

 
At 2:11 PM, Blogger mloyi said...

Umekwisha, lakini sio mwisho! Raisi mpya amepatikana vita mpya imeanza, umasikini ,maradhi, rushwa, makazi mabaya.
Hii ni nafasi ya kuonyesha ulichosema kwenye kampeni na kwa wale wengi, walichochagua.
Kila mtu sasa atimize wajibu wake.

 
At 2:12 PM, Blogger mloyi said...

Umekwisha, lakini sio mwisho! Raisi mpya amepatikana vita mpya imeanza, umasikini ,maradhi, rushwa, makazi mabaya.
Hii ni nafasi ya kuonyesha ulichosema kwenye kampeni na kwa wale wengi, walichochagua.
Kila mtu sasa atimize wajibu wake.

 
At 3:52 PM, Blogger Innocent said...

Aise mimi niko Moshi. Uchaguzi umekwisha lakini watu hawaamini eti jamaa kashinda urais kwa 80%.Kuna kiini macho watu wanasema kuna wizi wa kisayansi mi sijui lakini mambo ndio hayo na sasa tumerudi kwenye bunge la chama kimoja.
Upinzani kwisha kabisa.

 
At 1:12 PM, Blogger Fikrathabiti said...

Brother innocent hivi Mrema atazikwa wapi baada ya CCM kuchukua jimbo la vunjo kwani nilisikia yeye kaapa hadharani kua hawezi zikwa mikononi mwa jimbo la CCM

Jee unafahamu kiboriloni??Ndipo mie nitokeapo>

 
At 1:33 PM, Blogger Bwaya said...

Ninachoshukuru ni kwamba siku hizi watu wanaonekana kuwa wanaendelea kubadilika. Ujue mabadiliko yanaanza taratibu, lakini yapo.
We fikiri, mpaka wabunge wameghamua kuwa Msekwa anatakiwa kupumzika, japo Msekwa mwenyewe anasema ni wabunge hao hao walkimwomba agombee tena!
Haka kamchezo kanachekesha kweli. Hivi kama walimwomba imekuwaje wamemtema kwa kishindo hivi? Au walikuwa wanamsanifu, Mzee akafikiri wako siriaz?
Nadhani, Bwana Nkya haka kamchezokanaendelea, hakajaisha!

 
At 3:26 AM, Blogger HappySam said...

swahili
http://hotcelebfemales.blogspot.com/

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI