Tuesday, November 22, 2005

UKIMWI bado ni tishio

Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia UKIMWI, UNAIDS kwa kushirikiana na Shirika la Afya duniani, WHO limetoa taarifa ya mwaka inayoonyesha jinsi UKIMWI ulivyo bado ni tishio hasa Afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Unaweza kuisoma taarifa hiyo kwa kubonyeza hapa

3Comments:

At 3:15 PM, Blogger mwandani said...

Ndugu yangu Nkya, hili meme linatisha.
Na wameshabaini kuwa malaria na ongezeko la ukimwi vinakwenda sambamba. Akina mama wajawazito wenye malaria huambukiza watoto wao wakati wa kujifungua asilimia 40 zaidi ya wale wasiokuwa na malaria. Na watu wenye virusi ambao manaugua malaria hudhurika kwa ukimwi haraka kuliko wale wasio na malaria.
Na mi-mmbu kwetu nyumbani ilivyojaa! kwa wale tunaofuata nadharia za njama 'conspiracy theories' tutasema gonjwa lilitengenezwa kwa ajili yetu.

hebu fuata kiungo hiki upate unono.

http://allafrica.com/stories/200511180564.html

 
At 9:24 AM, Blogger Indya Nkya said...

Kwa kweli inaogopesha!! Asante kwa kiungo hiki

 
At 12:23 PM, Blogger Fikrathabiti said...

Unajua Nkya ukimwi kweli unatisha lakini ziko wapi jitihada za makusudi kukabiliana nalo.

Kina haja gani kwa watu kukaa kwenye warsha na kulipana 80,000 kwa masaa matano katika siku.Ni wazi kua kampeni na misaada ya kifedha inayotolewa haiwafikii walengwa.

Nadhani ulipata kuona kwenye kituo cha Channel ten jinsi hali inavyotisha huko makete lakini wadau wametulia katikati ya jiji wakila kuku na kenda kupumzika ufukweni nyakati za jioni kupunga upepo murua wa pwani na kuacha walengwa wakiteseka kila kukicha.

Au tuamini kua msemo wa KUFA KUFAANA NDO UMESHIKA HATAMU??????
Nami nakuomba utembelee kibarazani mwangu.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI