Wednesday, November 23, 2005

Bendera ya Uingereza yafanyani katika tovuti ya CHADEMA?

Ndesanjo amekuwa akipigia kelele matumizi ya lugha ya kiingereza katika tovuti za kitanzania. Sasa leo katika kuipitia tovuti ya CHADEMA nimeona wameweka bendera ya Uingereza juu kabisa kwenye tovuti yao. Hiyo bendera inafanya nini hapo? Mimi sijuhi sababu labda kama kuna anayefahamu anisaidie.

15Comments:

At 3:32 PM, Blogger Indya Nkya said...

Nimegundua kwamba ni kiunganishi kinachokupeleka kwenye tovuti yao ya kiingereza ambayo bado ipo kwenye matengenezo.

 
At 8:04 PM, Blogger boniphace said...

Subiri tuone kama watabadili maana tabu za kuweka viunganishi ni jambo la kawaida katika Blogu

 
At 10:39 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Nadhani ni kweli kwamba inawezekana kuna makosa ya kiufundi yametendeka.Lakini kama nia yao ni kumpeleka mtembelea tovuti kwenye tovuti yao ya kiingereza,nadhani sio sahihi kuweka bendera ya Uingereza pale.Sijui kama wataeleweka kirahisi wakifanya hivyo.

 
At 12:30 PM, Anonymous Anonymous said...

Linaweza kuwa tatizo kubwa sana la kiufundi. Jirani zetu wanasema tembelea nchi yetu uuone Mlima Kilimanjaro. Matokeo yake watu wanaelewa mlima upo kwao - wakiulizwa wanakana kuwa hawajawahi kusema mlima upo nchini kwao. Hiyo bendera isije ikawa inafanya kazi tofauti wakati ina malengo ya kutoa ujumbe tofauti.

 
At 3:22 PM, Blogger mwandani said...

Nilipata kusikia kuwa chama cha Conservative cha uingereza kinadhamini chadema. Hapo nyuma kidogo wakati helikopta ya kampeni ilivyozuzua watanganyika...
Kuna kiungo cha bwana Miruko kinaeleza uzuri... tafuta tafuta utaona.
Hayo mengine... hebu wafute hiyo bendera haraka

 
At 2:07 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mwezi wa sita mwaka huu niliwaandikia jamaa wa Chdema juu ya hiyo bendera ya waingereza na makoloni yao. Hakuna ubaya wa tovuti yao kuwa na toleo la kiingereza. Ila hakuna sababu za kimsingi za kuweka bendera ya nchi nyingine kuelekeza watu kwenye toleo hilo la kiingereza. Nilipowaandikia sijui kama walinielewa vizuri maana waliponijibu ilionekana kuwa walidhani ninawalaumu kwa kutaka kuwa na toleo la kiingereza. Kumbe nilikuwa ninawataka waondoe bendera Uingereza kwenye tovuti ya chama cha siasa Tanzania

Nilipowaandikia mwezi huo wa sita hivi ndivyo walivyonijibu:

Bwana Macha,

Asante kwa ushauri.

Tunao marafiki nje ya nchi (afrika na ulimwenguni kote) ambao tunasaidiana nao katika kuendeleza demokrasia. Wao pia wanapenda kujua msimamo wetu na vilevile nini kinaendelea Tanzania. Kwa vile tovuti ni njia rahisi ya kuwasiliana hatuna budi ila kuwa na tafsiri ya tovuti yetu katika lugha ambayo wao wanaielewa.

harakati njema.

 
At 2:19 PM, Anonymous Anonymous said...

mimi sioni shida ktk hilo, dont be too much suspicious of unknown facts.

 
At 5:46 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Sidhani kama tatizo letu ni kuwashuku Chadema kwa lolote baya. Tunachouliza ni swali rahisi tu: kwanini bendera ya Uingereza iwepo kwenye tovuti ya chama cha siasa cha Tanzania?

Iwapo bendera hiyo inaelekeza watu kwenye toleo la kiingereza, basi wako tunaoamini kuwa hakuna sababu za kimsingi za kutumia bendera ya nchi nyingine kufanya kazi hiyo (ya kuelekeza kwenye toleo la kiingereza la tovuti hiyo). Bendera za nchi zina maana kubwa pengine kuliko tunavyodhani (ingawa wenzetu huruhusu zitumike hata kutengenezea nguo za ndani!). Lakini pia kuna jambo jingine (hili naweka hapa kuchokonoa tu fikra): ukisoma kitabu cha Mazrui kinaitwa "The Power of Babel" utakutana na hoja kuwa kiingereza hivi sasa "kimetekwa" na wengine toka kwa Waingereza. Kimechukuliwa na Wajamaika wakazalisha "patwa" wakachukua Wa-Sierra Leone, Wanigeria na Waliberia wakazalisha "pidgin". Wakachukua Wamarekani wakazalisha chao. Na Wakanada. Na kule Australia.

Lakini hilo ni dogo. Kubwa ni swali la mantiki ya kuweka bendera ya nchi nyingine kwenye tovuti ya chama cha nchi nyingine. Kwani bendera iwakilisha taifa na mapana yake (sio lugha tu).

 
At 7:08 PM, Anonymous Anonymous said...

Kama ni announi fakti, tupe hiyo nouni fakti ndugu? Lakini nadhani huwezi kuona tatizo, na hilo halishangazi ukiwa mmoja wetu, kama Chadema yote hawakuliona (endapo hawana malengo mengine) sisi wengine tutaweza?

Bila historia, utamaduni na saikolojia ya binadamu duniani inayoeleweka na uzoefu katika masuala masuala na kujiamini na kujipenda na kujiheshimu binafsi yetu hatuwezi liona hilo. Sasa kuna siku hawa waheshimiwa wakitawala watapakaa bendera hiyo kwenye ndege zote za ATC na meli zetu zinazokwenda Uingereza, na kwa wengine itakuwa ni sawa tu. Lakini tuombe wapakae tu kwenye ndege na meli hizo na siyo kwenye (ubongo/fikra za) wananchi wao.

Siku zote tumekuwa na asili ya kudharau udogo wa miiba inayotuchoma huku ikituachia vilema kibao mwilini na vichwani, lakini si ubongo wala macho yetu yanafunguka kuyaona hayo - angalau hata sikio basi lifunguke.

Kwangu ndugu bendera ni kitambaa! hapana. Wenzetu wanacheza mchiriku katika redio ya sikioni (wokman) halafu tunataka kucheza na kwenda sawa sawa na midundo ya mchiriku kama wanavyocheza wao; sheshe hilo hatuwezi!

 
At 5:38 PM, Blogger Indya Nkya said...

Jamani niliwaandikia watu wa CHADEMA kuhusu hii bendere wamenijibu kama ifuatavyo:

Bwana Nkya,

Pole na usumbufu ulioupata kwa bendera ya Uingereza kuwa kwenye tovuti yetu.

Lilikuwa kosa la kiufundi na sasa limesharekebishwa. Tovuti nyingi sasa zimekuwa na mtindo wa kuweka bendera kuashiria lugha inayotumika. Kama ungebofya kwenye bendera hiyo ungeeona unapelekwa moja kwa moja kwenye tovuti yetu iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza. Ninakiri, kwa tovuti ya chama cha siasa halikuwa wazo zuri kutumia mtindo huu wa bendera. Tutakuwa makini zaidi siku za mbeleni.

Ninashukuru uliliona hili na ukaamua kutuandikia.

Harakati njema,

 
At 1:27 AM, Blogger patashika said...

kwanza nataka kukuambia akili zako zimekomaa na unanifurahisha kwa tabia yako ya kuresearch maswala mengi mbali mbali ni wengi tumeona hii bendera lakini hatukugundua chocote kuhusu hako kabendera kengine kanafanya nini hapo juu???

sikufichi unanipa moyo sana kila ninaposoma kazi zako na maoni yako mbali mbali.

 
At 6:57 PM, Blogger Indya Nkya said...

Asante Fatma tuendeleze mapambano

 
At 7:44 PM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

bwana idya,

akhsante sana kwa utafiti wako mahiri! ni kweli pia kuwa hata hao wasituchukulie kwa bei rahisi sana! pengine ikachukuliwa kuwa ni gharama ya demokrasia! heko bwana idya!

mark!

 
At 5:26 PM, Blogger Indya Nkya said...

Shukrani Bwana Mark. Mapambano yanendelea

 
At 12:12 PM, Blogger Fikrathabiti said...

Mambo ya msingi yanayogua Taifa letu si ya kuyaacha hivi hivi yapite!!!Labda yahojiwe kwa nguvu zote.

Chadema walikua wanahoji sababu za chama tawala kuchangiwa na wafanyabiashara,je wao msaada wa takribani bilioni Tatu walizopata toka Conservative watatupa jibu gani nasi tusiokua na vyama tukiamua KUHOJI????

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI