Wednesday, February 15, 2006

Gregory yuko wapi?

Nilikutana na binti mmoja ambaye tulikuwa wote Jeshi la Kujenga Taifa (Ndesanjo huliita la kubomoa taifa) akaniuliza: Hivi Gregory yuko wapi siku hizi? Nikamuuliza Gregory gani? Akanishangaa akasema kumbe urafiki wenu uliishia jeshini? Nikamuuliza jina lake la pili ni nani? Akaniambia Macha. Ohh!! Nikamwambia nimemkumbuka sasa. Nikamwambia kwamba Macha alirudisha jina lake la Gregory kwa Mchungaji wake kama mmoja wa wahusika katika kitabu cha Pambazuko Gizani alivyotaka kurudisha jina lake la Paulo kwa Padre. Binti wa watu hoi. Nakumbuka Macha alipokuwa kwenye jitihada za kurudisha jina lake alikuwa akinishambulia kila siku nirudishe la kwangu pia ikiwa ni ishara ya ukombozi mpya. Kabla ya kurudisha jina lake Ndesanjo alikuwa akiitwa Gregory!!!

6Comments:

At 5:26 PM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

Idya na wewe la kwako la zmani ni lipi?

magumu sana haya mambo! ndio maana mie huwa nawashangaa wale misimamo mikali! badala ya kukata kili zako na kitimoto unajiwekea masharti (uzio)kila upande!

 
At 2:28 PM, Anonymous Anonymous said...

Ugumu wa haya mambo uko wapi, Msaki? Hakuna jambo la aibu na kusikitisha kama kuwa na jina ambalo mama yako, marafiki zako, majirani, babu na bibi, n.k. hawawezi kulitamka. Na sababu pekee inayokufanya uendelee kuvaa jina hilo ni imani kuwa jina hilo ni la "kikristo." Dunia nzima Waafrika ndio tunaongoza kwa kuazima majina toka Ulaya na Uarabuni. Wachina, Wahindi, Wayahudi, Waarabu, Wajapani, n.k. wanatumia yao...sisi ndio tunahaha huku na kule kuchukua majina ambayo hata kuyatamka hatuwezi. Joseph inatamkwa Josefu, George inakuwa Joji, Godson inakuwa Gudisoni...

Nadhani suala la kujiheshimu kwa kutumia majina yetu, tunayoweza kuyatamka, tunayojua maana yake sio msimamo mkali bali ni msimamo wa busara na heshima kwa utamaduni wako.

Kuna makala hii hapa ipitieni:
http://tinyurl.com/dnyz8

 
At 8:58 PM, Blogger Indya Nkya said...

Macha umeniacha hoi kabisa. Halafu Reginold linatamkwa Rekyinolid kwa kifupi Rekyi. Gregory linatamkwa Kyirekori. Kule kwetu mlimani George wanatamka Kyoghikyi.

 
At 8:06 AM, Anonymous Anonymous said...

Naona nimechelewa haya mambo ya majina. Mimi pamoja na kaka zangu tuna majina ya kinyakyusa na sababu iliyomfanya baba yangu ambaye ni msomi wa zamani kutupa sisi majina ya kinyakyusa ni kwa sababu ya jina lake ELI. ELI lina maana hii (Means "ascension" in Hebrew. In the Old Testament he was the high priest of Israel and the teacher of Samuel) Sasa Baba anasema alikuwa Scout (Skauti) miaka hiyo ya zamani sana na alifanikiwa kwenda Israel na huko ndiko walimuuliza unajua maana ya ELI akasema hajui ila baba yake kaliona kwenye Biblia ndio maana kampa, wakamshangaa na kumuuliza hizi huko kwenu hamna majina ya kikwenu? Kwanza wewe ni nani hadi uchukue jina la mmoja wa watu wanaoheshimiwa katika Biblia? Ndio maana kuanzia siku hiyo katupa sisi majina ya Kinyakyusa woote. Na huwa najisikia nalo sana pale wazungu wanapolikosea. Na watoto wangu lazima wapate majina ya nyumbani. Nimefurahishwa na habari hii na sanasana maoni ya Ndesanjo.

 
At 9:08 AM, Blogger Indya Nkya said...

Safi sana Bwana Lusajo. Kwa kweli safari ya majina bado ni ndefu. Wasomi ndio wangetakiwa waonyeshe njia na kuhoji uhalali wa majina ambayo hatuyajuhi. Mimi watoto wangu wote nimewapa majina ya kilugha kisawasawa. yanawatambulisha popote walipo. Kuna watu wengine tena ambao wamechungulia darasani wananiuliza kwa nini nimewapa haya majina? Japo wao hawajuhi kwa nini wanawaitwa majina ya kikoloni watoto wao

 
At 1:08 PM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

sasa hapo patamu, nimnaelewa kwanini hata Michuzi aliamua kuniita Bwana Alama! - majina ya watoto ninaowafahamu wa kingunge ni Kinjeketile na Mpilig'ondo! si mnakumbuka aliapa na mkono mkavu juzi?

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI