Tumepoteza maelfu ya miaka ya elimu
Hivi lile Sakata la kufukuzwa kwa madaktari limeishia wapi? Kama wote walifukuzwa basi ni kwamba taifa limepata hasara ya maelfu ya miaka iliyowekezwa kwenye elimu. Tunaambiwa kwamba, kila mwaka mmoja wa elimu mtu anaopata unaongeza ufanisi katika utendaji kazi ambao hutoa mchango katika ukuaji uchumi na kuongeza maslahi ya anayepata elimu hiyo. Kwa kifupi ni kwamba rasilimali watu ni mtaji mkubwa mno katika ukuaji wa uchumi. Kwa nchi yenye watu wachache wenye elimu ya chuo kikuu kama Tanzania, kufukuza madaktari 200 waliosoma kwa wastani wa miaka 19 kila mmoja ni hasara kweli. Ngoja niweke tarakimu rahisi kabisa. Chukua miaka 7 ya shule ya msingi, halafu ongeza 6 ya sekondari, kisha ongeza mitano ya shahada ya kwanza ya udaktari na mwisho ongeza mwaka 1 wa mafunzo ya vitendo (Internship) inakupa jumla 19 kwa kila mmoja. Sasa ukizidisha miaka 19 kwa watu 200 unapata miaka 3,800 (Elfu tatu na mianane). Kwa hivyo miaka yote hii imepotea. Wakiamua kwenda kufanya kazi nchi nyingine, nchi hizo zitafaidi sana hiyo miaka 3,800 ya elimu. Kwamba walikuwa na haki ya kugoma au la ni mjadala mwingine. Leo nimejadili idadi ya miaka ya elimu itakayopotea kwa kufukuza madaktari 200.
9Comments:
Karibu tena Nkya. Usiwe unapotea hivyo! Ulikosekana sana nyumbani kwako nikawa naogopa kuja manake kila nikija "nakutaga" ukimya tu! KAribu tena tuendelee na changamoto.
Miaka mingapi wewe unajali? Mbona miaka iliyopotezwa kwenye utumwa na ukoloni hawaongelei wala hawatafuti haki yake hata siku moja! itakuwa hivi vimiaka vya kufundishia kazi watu kama 200 hivi.
bwana nkya umenigusa sana hapo...unajua siku moja nilikuwa ninafikiria je ni kwa nini marekani huchezesha bahati nasibu ya uraia wao? je bahati nasibu hiyo inafuata vigezo vya funga macho na nyakua kama hizi tunazozijua? wataalamu mtatambia hapo....
turudi kwa mataifa ya wenzetu kama ya ulaya na mfano Uingereza..kuna jarida moja huwa naliona hapa SA linatangaza nafasi nyingio tu za kazi kule kwao...na linataka wafanyakazi katika maeneo hayo toka dunia nzima....nilkajiuliza tena je unajua jiji la london peke yake lina watu biliono ngapi? je wana mashamba ya kulima? na kila siku wanapokea watu wengi kutoka kila kona ya dunia....
kumbe basi nikagundua kuwa nchi za wenzetu ni janja sana kwa kuwa na akili zaidi ya kuvuta VINAVYOELEA TOKA KWA WENZAO....je ni wajibu wa serekali zetu kuwatenda wema wanataaluma ili wabaki nchini, kuwatenda vibaya ili waondoke na waache kuwasumbua wanene na vimatatizo vyao kama ilivyozoeleka?
bwana nkya, labda hukuwa na habari, madaktari walirudisha kazini isipokuwa wale 29 walioitwa kiini cha mgogoro.....lakini sielewi, kwani wale waliobaki wote walikuwa wanamsemelea nani? hii inaonyesha kuwa devide and rule bado inatumika kwenye nchi huru kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni...na kama scandal si scandal tu kuna haja gani kusema hawa ndio hawa sio? tufike wakati tukubali kosa / udhaifu likitokea!
Nkya,ingawa hesabu nilizikimbia tangu kidato cha pili,hizi zako nimezielewa.Sio kwamba ni rahisi bali zinaingia na kujikita ndani ya moyo kirahisi.
Mark,nchi za huku ni kweli zinachukua vinavyoelea.Canada ni mojawapo.Hapa Canada usishangae kabisa mtu mwenye PHD akiwa msafisha vyoo au dreva taksi.Nani alaumiwe?
Ndugu Nkya na wengineo,
Natumaini mmeona makala ya mapambano ya wabunge kutaka kuongezwa mshahara. Nimeituma hiyo makala kwa baadhi ya watu ambo nina anuani pepe zao! Kwa wale ambao mmeiona hiyo makala naomba muilete kwenye blog zenu ili yuweze kuizungumzia kwa kuijadili hatuwezi.
Kwa roho yenye machungu,
F MtiMkubwa Tungaraza.
Nkya, huwa napendanga unapoingiza hisabati kwenye uchambuzi wako yakinifu. Ila kubwa karibu. Umerudi kwa nguvu. Nimependa uliposema vyama shindani badala ya vyama vya upinzani.
Naam,
Ujinga, uchoyo, ubinafsi, unafiki, uongo, roho mbaya vikikithiri ndiyo huleteleza mambo kama haya ya kupoteza maelfu ya miaka ya elimu. Kwa miaka mingapi sasa tumekuwa tunasikia hili sakata la madaktari na serikali? Miaka hii yote lilipokuwa linaendelea hili sakata kwa nini halikutafutiwa ufumbuzi wa kudumu? Suala hili limekuwa kama barabara ya lami kuitia kilaka cha mchanga. Mchanga utakijikita kwa muda na baadaye korongo litaibuka tena.
Siye Watanzania tuna utajiri sana wa madaktari mpaka tunaweza kuwatupa tu. Palipo mabishano au kutoelewana lazima patafutwe muafaka. Kuwafukuza kazi madaktari na kuleta madktari wa mkopo toka jeshini na wizarani siyo suluhisho la kudumu. Hapa lilitakiwa lipatwe suluhisho la kudumu.
Halafu kuna swali "..HAO MADAKTARI WA JESHI WALIOKOPWA KWENDA KUZIBA NAFASI ZA MADAKTARI WA MUHIMBILI HUKO MAHOSPITALINI WALIKOTOKA WAGONJWA WANATIBIWA NA NANI?"
Waheshimiwa wabunge walipokutana kwa mara ya kwanza, kitu cha kwanza walichokijadili ni kuongezewa mishahara. Tena wanazungumzia mshahara wa mamilioni ya shilingi. Zaidi ya hivyo Mheshimiwa Kimiti alidai kwamba wabunge ndiyo watu wenye kazi ya muhimu kuliko zote. Ningekuwa na uwezo ningewaamrisha madereva wa nyonya mavi wagome mwezi mmoja halafu tungejua nani ana kazi muhimu kuliko zote. Tanzania ingenuka mpaka nchi zote nane tunazopakana nazo zingeanzisha vita na sisi kwa sababu ya harufu ambayo ingewafikia.
Halafu waheshimiwa wakishamaliza kujipandishia mishahara. Watanzania wote nao wagome kazi mpaka wapandishiwe mishahara. Pale nyumbani kuna watu hawajawahi hata siku moja kushika shilingi elfu kumi halafu ndugu waheshimiwa wanataka zaidi ya milioni moja!
Kila kheri,
F MtiMkubwa Tungaraza.
Mti mkubwa umehoji suala la msingi kabisa. Hao madaktari walipotoka ni nani kaziba mapengo yao? Lakini lingine(japo kasheshe lenyewe liliisha) ni kwamba kama hakuna aliyeziba mapengo yao basi walikuwa hawana kazi ya kufanya walikuwa wakistarehe na kula pesa ya bure
Madaktari wa jeshi wametumika kama mamluki wa serikali! Walichokifanya ni kusaidiana na serikali katika kupinga maombi ya kuongezewa mshahara yaliofanywa na madaktari raia. Hilo ni kosa la kimaadili la kuwasaliti wanataaluma wenzao. Wamechezewa shere na wanasiasa na sasa wanaonekana kama mbwa aliyetupiwa fupa anavyofurahi kwa kutingisha mkia. Nina hakika baadhi yao wametahayari waliposikia madai ya waheshimiwa wabunge ya kutaka kuongezewa mshahara. Kwa kuelewa muundo wa uanajeshi ninaelewa ilivyowawia vigumu kuwaunga mkono madaktari wenzao na kutokana na ugumu huo ndipo wansiasa wakawageuza kuwa vibaraka wao na kuwafanya waonekane kama vikaragosi. Mchezo huu ukichezwa vibaya unaweza kuleta hatari kubwa ya mapambano ya silaha kwa sababu nguvu ya mwanajeshi imelalia kwenye silaha siyo mazungumzo.
Mungu Ibariki Tanzania,
F MtiMkubwa Tungaraza.
Post a Comment
<< Home