Thursday, January 19, 2006

Vyama Viendeshwe na wanachama

Ule uchaguzi wa mwaka jana umetoa funzo gani kwa vyama vinavyoitwa vya upinzani?( Sipendi hili neno upinzani; tuviiteje? Shindani?). Kwanza kabisa ingebidi wajifunze kwamba ruzuku haiwasaidii bali inawamaliza. Unajua ruzuku ndio inayofanya kila chama kitake kuweka mgombe wake ili angalau kipate mbunge na hatimaye ruzuku? Sisemi kwamba kuna vyama ambavyo vinaweka wagombea kwa sababu nyingine nje ya ruzuku. Ukiangalia kiundani kabisa ruzuku haifaidishi upinzani bali chama twawala. Katika ruzuku ya shilingi bilioni nane kwa mwaka CCM itaondoka na zaidi ya bilioni saba halafu kitakachobaki jamaa watagawana. Turudi kwenye hali halisi; ukitoa CCM ni chama gani kingine kinaweza kujigamba kwamba ruzuku inasaidia katika kampeni au katika kuimarisha chama? Ni asilimia ngapi kwa mfano ya fedha za kukodi helkopta ya CHADEMA ilitokana na ruzuku?

Ukweli ni kwamba kwanza kabisa chama ni kikundi cha watu wenye mwelekeo unaofanana au wanakubaliana kiitikadi. Kama ni kikundi basi inabidi kiendeshwe na hao wanachama. Hakuna haja ya kila mtanzania kuendelea kuendesha vyama ambavyo ni vya watanzania wachache sana. Hivi ni asilimia ngapi ya watanzania ni wanachama wa vyama vya siasa? Hili tulivalie njuga ili hii ruzuku ifutwe. Sioni kama eti ruzuku inasaidia kukuza vyama na hatimaye demokrasia. Kwanza hili suala la kufikiria demokrasia ni vyama vingi sijuhi limetoka wapi. Hata kama pesa hizi kinadharia zina lengo la kuimarisha vyama basi kinachoimarika ni kimoja tuu. Hata kama vingeimarika vyote, viimarishwe na wanachama wenyewe. Wanaopenda vyama wavichangie.

Hivi vyama vya upinzani ingebidi vianze kuchimba masuala ya msingi ambayo yanafanya CCM kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha. Kwa mfano mali ambazo CCM ilirithi wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanza. Angalia viwanja vya mpira kibao bado ni vya CCM, majengo mengi ambayo yalijengwa kwa kodi za wananchi bado ni ya CCM. Kwa nini mali hizo ziendelee kubaki za CCM? Tume ya Nyalali ilipendekeza kwamba mali hizo zirudishwe Serikalini lakini mpaka leo hakuna kilichorudishwa. Halafu jamaa wa upinzani wanakaa kukimbilia ruzuku ambayo kila mwaka itaendelea kuongezeka kw CCM huku ikipungua kwao, huku Chama hiki twawala kikiendelea kufaidika na mapato ambayo ni mali ya kila mtanzania. Pamoja na mambo mengine ya katiba na tume huru ya uchaguzi mimi nimeongele mambo mawili yanayohusu pesa.

Hili la ruzuku wanablogu wote tulivalie njuga. Vyama viendeshwe na wanachama hizo hela za ruzuku zikabiliane na kipindupindu au shughuli nyingine za kimaendeleo.

6Comments:

At 8:03 AM, Anonymous Anonymous said...

Hahaha!! Kwani hujui hata wazee wazima unaweza kuwaimbia kawimbo ka Danganya toto?!! Ndio hivyoo wanayeyushwa na danganya toto tuu. Kwanza mimi nadhani wengi wao bado ni CCM tuu.

 
At 1:52 PM, Blogger mark msaki said...

nkya nimeona wazo hili..mjadala mzuri....ila kwa sasa nimechoka kiakili nitarudi baadae kusema chochote ninachotaka!

 
At 4:02 AM, Anonymous kikwembo said...

Yap mkubwa nakuunga mkono asilimia mia mbili hili swala la ruzuku lazima liangaliwe upya kwa kweli kwani halina msingi wowote ukizingatia kwamba sio watz wote wenye itikadi za kisiasa au ni wanachama wa vyama vya siasa.Sasa kama ni hivyo haina maana kutumia hela zao kuwapa watu ruzuku huku hiyo ruzuku ikiwa inawatia ujinga na kuwaua kisiasa badala ya kuwajenga zaidi lazima kila chama kijiwekee njia madhubitu ya kuingiza kipato badala ya kutegemea ruzuku vipĂ® ukiwa huna vigezo vya kupata hiyo ruzuku lakini una msimamo mzuri kisiasa na malengo mathubuti kwa taifa letu utafanya nini sasa hapo.Kwa misingi hii ni lazima uwe na mipango maalumu kama unataka kuanzisha chama jua kabisa wapi utatoa pesa sio kutegemea ruzuku ya serikali iliyo jaa ufisadi mtupu.

 
At 4:14 AM, Anonymous Sir Kikwe said...

sipendi kabisa siasa lakini kuna mada fulani huwa zinanigusa sana alafu naumia sana moyo wangu ndo maana naona bora niongee tu kwa kweli ruzuku sio issue mie binafsi siipendi kabisa.Kweli wanasiasa wetu wengi bado wanafiki,waongo na wabinafsi hili suala wanalifahamu kabisa ila basi tu mtu kama Prof Lipumba msomi yule najua kabisa ila basi ubinafsi tu umewajaa tu wale wote.Kila mwaka wanataka ruzuku iongezwe huku wakijua kwamba wao wana wabunge wachache sasa kwa mtindo huo ruzuku yote inakwenda kwa CCM peke yake sasa hapo wanajenga chama gani hahahahahha.

 
At 8:29 AM, Blogger oscer said...

kwa upande wangu nizungumzie kuhusu timu yetu ya taifa,jamani watanzania tukubali kwamba kwa kiwango flani hivi timu yetu imeimarika tangu tuwe na huyu kocha marcio maxmo,hata kuingia kwenye mashindano ya CHAN ni bonge la title kwa nchi yetu ya tanzania kwa hiyo naona tumpe kocha mda zaid tuone mafanikio yake.

 
At 8:35 AM, Blogger oscer said...

jaman watanzani kwa sasa tuwe kama watu ambao tiyari tumeelimika,tuweze kuitambua siasa ni kitu gani.kwanza tujue chimbuko lake alafu ukisha ielewa ujuye ni jinsi gani gani utaweza kuizungumzia na sio kukurupuka na kujifanya waielewa siasa kumbhe wazaliwa jana tuu,tukae tuisome kwa umakini na kuilewa zaidi na ndo tuianze kuizungumzia na siyo kukurupuka tuu.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI