Thursday, January 19, 2006

Natamani Kipindupindu kifike Ikulu

Kuna mwanamuziki mmoja mtanzania, kati ya wale wanaoitwa wa kizazi kipya anatamani mambo ya kuchekesha sana katika moja ya nyimbo zake. Kwa mfano anatamani mlima Kilimanjaro uamie sijuhi wapi na bahari pia ihame. Mimi leo nakuwa kama yeye. Natamani Kipindupindu kilipuke Mikocheni, Osterbay, Masaki halafu kipige hodi Ikulu pia. Kila siku kinavamia Buguruni, Manzese na sehemu zingine za walalahoi. Hivi kweli tumeshindwa kabisa kudhibiti kipindupindu? Labda kikifika ikulu kitapatiwa ufumbuzi. Rais mpya kaanza kazi kwa kukaribishwa na mlipuko wa kipindupindu kama ilivyo kawaida ya kila mwaka. Sijuhi kama atakivalia njuga kwa Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu mpya au kitaendelea kumaliza watu kwa Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya? Kama waziri wa Afya ataendeleza mapambano ya magonjwa kwa warsha, semina na makongamano na kuchapisha fulana na kofia basi hakuna kitakachotokea. Safari hii Waziri wa Afya ni Profesa. Sijuhi kama atasadia lolote kwa sababu huko nyuma alishawahi kuwepo Profesa akaboronga pia. Mimi sijuhi aibu hii ya kipindupindu itaisha lini.

3Comments:

At 8:21 PM, Blogger Bwaya said...

Nkya, umenichekesha sana maana umezungumza kitu ambacho sikuwahi kukifikiri kabla.
Tatizo la kipindupindu naona kama vile halitakaa lipate ufumbuzi wake. Nasema hivi kwa sababu mbinu tunazotumia kupambana nacho ni za ajabu kabisa. Huwezi kumaliza kipindupindu kwa kuendekeza warsha ambazo matokeo yake hayawafikii wananchi kwa ujumla wao. watu wanagawana hela kwenye masemina, wanasahau kuwa walikuwa kwenye semina ya kupambana na kipindupindu!
Tunajaribu kumaliaza tatizo kwa mbinu za zimamoto, hatutaliweza. Labada iwe kama unavyotamani, kipindupindu kiivamie ile nyumba ya magogoni, hapo watastuka.
Ujue, hili suala halina tofauti na namna vita dhidi ya malaria inavyopiganwa. Huwezi kumaliaza malaria kwa NGAO pekeyake. Kuna haja ya kubadilika.

 
At 7:29 PM, Blogger Indya Nkya said...

Aisee kwa hili la Malaria linahitaji kitabu. Dawa ya Malaria ni kuangamiza mbu na si kuwakukuza kila usiku. Ukitaka kuona mambo yanawezekana nenda Mwadui walipowekeza jamaa kwenye almasi. Hakuna mbu. Wanawaua si kwa Doom bali kuangamiza vyanzo vyake. lakini hili la kumaliza mbu lina siasa kali za biashara ya dawa kimataifa

 
At 1:51 PM, Blogger mark msaki said...

bwana nkya sikuwahi kufikiria hilo!! nashukuru sana. maana mfano ukiwa afrika kusini malaria ni jambo ya kufikirika. hivi majuzi ilitokea outbreak pale limpopo - mpakani na zim kila mtu akachanganyikiwa.......sasa nimeelewa...zidumu blogu...

niliwahi kusikia hata ile brazaville congo wabelgiji walikuwa wanaspray juu ya jiji .....nadhani sasa tunahitaji ukombozi wa dhati!!! malaria is a leading killer in Africa!!

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI