Wednesday, February 15, 2006

Ilikuwa lazima Yesu afe?

Rafiki yangu mmoja ameniacha hoi aliponiuliza kwamba; hivi Mungu alikosa njia nyingine ya kumkomboa mwanadamu mpaka amtume Mwanae wa pekee afe kwa ajili ya dhambi zetu? Kulikuwa na ulazima wa damu kumwagika? Huyu jamaa yangu yeye si mfuasi wa dini za kuja kwa hivyo nikaona kwamba pengine anauliza mambo hayo kwa ajili hiyo. Baadaye nikaingia kwenye mjadala mwingine na jamaa mmoja mfuasi mzuri wa madhehebu ya kikristo. katika maongezi yake akasema angekuwa rais wa dunia angewaua watu wa jinsia moja wanaotaka kuooana. Jamaa akambana hivi wakristo mnaua? Nikapata jibu langu la awali la kwa nini Yesu afe? Jamaa alisema ndio maana Mungu alimtuma Yesu aje afe kutoa ishara kwamba hakuna ukombozi pasipo kumwaga damu!!

6Comments:

At 5:22 PM, Blogger mark msaki said...

clever finding!!! hahahahaha!!! ni kweli kabisa. ukichunguza hata historia ya dunia tangu mwanzo wengine inabidi wateseke ili wengine wasonge front!!

kuna bwana mmoja tunaye hapa anaitwa Albert Modi (daktari wa falsafa ya kilimo) yeye pamoja na kuzunguka na kwenda shule kote bado hajaona cha kumtoa kwenye roots!! juzi juzi alikuja akasema kuwa kumwaga damu kumekuwa ni historia ya dini za watu weupe, tangu enzi za nyuma kama "makafara". cha ajabu hata waliouliwa waliona ufahari... akasema utaratibu huo umeendelea hadi leo ambapo Joji kichaka na toni blea wanaendelea kutoa kafara huku na kule ili waendelee kuwa juu...nikahisi kweli kwani saa nyingine nikiangalia video za irak sikuwa ninaona mantiki za upigaji waliokuwa wanafanya....na hizi mambo zinaitwa cluster bombing!! - kufacilitate vifo vingi kwa muda mfupi!! bwana albert alisisitiza kuwa dini zetu zilihubiri mambo mema tu kama vile amani, upendo, na kuomba mvua!!! yeye ni wa kabila la Xhosa..na anaamini katika dini ya asili!!

wakati ninatafakari jioni yake nikasoma bible yangu nikashtuka kuona kuna bwana mmoja (jina limenitoka)alikwenda vitani, akamuambia mungu nikishinda wakati ninarudi cha kwanza kunijia ni chako... akaenda aliporudi ameshinda, bintiye akatoka kumlaki!! akasononeka sana, bintiye akasema baba uliahidi, na hivyo itakuwa, lakini niache niende nikaulilie uanawali wangu milimani , na alikuwa hajamjua mtu mume (nadhani siku 40)halafu nirudi na iwe ulivyoahidi kwa mungu...yule binti akaenda na wenzake wakamlilia uanawali wake kisha akarudi, babaye AKAMTOA KAFARA!!.....Swali lililonitatiza hapo ni

1. iweje uue mwanao na mungu afurahi?

2. inaonekana ulikuwea ni utaratibu wa kawaida kuua. kafara lakini laenda kwanza milimani...kwani ingekuwa sio kawaida si binti angetoroka? na inaonekana kabisa kuwa huyu bwana aliposema atatoa cha kwanza kama kafara mie nilikuwa ninadhani labda anamanisha mnyama kama ng;ombe au mbuzi lakini nikaja kuona alikuwa ana maana zaidi kwa binadamu!! je angetoka mkewe ingekuwaje??

3. je mungu wa wazungu amekuwa na nguvu zaidi kwa kuwa wao hutoa makafara ya watu badala ya mbuzi kama sie? ndio maana wametuzidi??

niliogopa sana baada ya hapo, nikaona kama nachanganywa vile!!

 
At 9:04 PM, Blogger Indya Nkya said...

Hapo Msaki umeuliza maswali ya msingi kweli. Hasa unaposema kwamba mungu wa wazungu anakuwa na nguvu kwa vile anapewa damu ya binadamu na ndio maana wametuzidi. Mimi nawaza vingine. Pengine tunamuomba mungu wa Abraham, Isaka na Yakobo badala ya kumuomba wa Msaki, Macha, Tunga, Msangi Nkya nakadhalika. Sasa Mungu wetu amekasirika kwa kumruka na kwenda kumuomba mungu mwingine ambaye hatuhusu!!

 
At 1:02 PM, Blogger mark msaki said...

au kwa maana nyengine ni kuwa unapomuomba mungu wa Abrahamu, atakusikiliza ikiwa tu, interest yako haitapingana na ya watoto wa Abrahamu? sasa basi kama ni utandawazi, tunashindana na watoto wa abrahamu, si atavutia kamba upande wa wanae? mbona ilimshinda Nyerere kukaa kimya alipoona CCM mambo mazito akazunguka na Mkapa na kifimbo chake inji (kimrema mrema) nzima? ciao!

 
At 5:22 PM, Blogger Indya Nkya said...

Kwa vyvyote ukiomba na wayahudi hata kama mungu wao angekusaidia, basi atakusaidia akishawasaidia watu wake. Msaada utataegemea kama kuna lolote analoweza kusaidia kama hakuna basi

 
At 8:48 AM, Blogger Bwaya said...

Hapo ipo kazi kwelikweli!

Hivi Nkya unadhani wayahudi wanamtambua huyu Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo?

 
At 12:52 PM, Blogger Indya Nkya said...

Unajua kuna wayahudi wa aina nyingi. Kuna wanaomkubali kuna ambao wana utaratibu wao mwingine

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI