Thursday, February 16, 2006

Afrika haitaji msaada wa Chakula

BBC iliendesha mdahalo mzuri sana kati ya Nicholas Crawford toka WFP na Tajudeen Abdul-Rahem Wa Justice Afrika kuhusu chakula barani Afrika. Jamaa wa Justice Afrika anadai kwamba hakuna haja ya Afrika kupewa msaada wa chakula na anajaribu kuelezea kiini cha tatizo la njaa barani Afrika na jinsi misaada inavyolemaza bara hili. Mzungu wa WFP anatetea umuhimu wa msaada wa chakula. Kwa kweli nakusihi usome mdahalo huo hapa. Ni mdahalo mzuri mno.

4Comments:

At 4:54 PM, Anonymous Anonymous said...

Safi sana kiungo hiki. Mjadala huu umenisaidia sana kwa nondo kwa ajili ya mjadala nitakaoshiriki kuhusu suala hili la njaa Afrika.

 
At 9:42 AM, Blogger Reggy's said...

Indya hapa umefanya jambo la mbolea. Njaa Afrika ni tatizo la mwaka hadi mwaka. tatizo ni kutegemea mvua za mwenyezi mungu kwa ajili ya Kilimo. Labda mapinduzi ya kilimo yakifanyika ndipo njaa itatoweka. Hao wazungu lazima wajue kuzisaidia nchi za afrika ni wajibu wao, lakini wasaidie kuinua kilimo cha umwagiliaji, si tu danganya toto ya chakula.

 
At 3:41 PM, Blogger Indya Nkya said...

Aisee Miruko hamna kitu kibaya duniani kama msaada wa chakula. Wanakulemaza kabisa. Wanakufanya usilime wanataka upate msaada kwa sababu ukilima utajitegemea. Kama unavyosema si wangesaidia kilimo?

 
At 6:03 PM, Anonymous Anonymous said...

Njaa haisababishwi na ukame wala kutokuwa na kilimo cha umwagiliaji. Tunaweza kulima na kuvuna chakula cha kutosha kwa zaidi ya mwaka. Na hatuhitaji kumwagilia ili kupata mavuno mengi kama hayo kwani mvua tunapata ya kutosha na ukame ni kitu cha kawaida. Kinachotakia ni mkulima ajue: (1) ni mazao gani yanastawi vizuri katika eneo analoishi (2) alime vipi (msimu, utunzaji wa mazao shambani na baada ya kuvuna, etc) ili kuongeza mavuno kwa kila eka (3) awekeze muda na nguvu shambani msimu wa kilimo. Bila shaka atavuna. Hahitaji teknologia ya juu kujilisha.

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI