Kina Galileo wasingehoji tungekuwa wapi?
Ndani ya blogu hii kuna habari ya Askofu kuzaa mtoto na kujificha. Hoja hiyo imejadiliwa sana. Baadhi ya watoa maoni wanaonyesha ni jinsi gani wanavyotaka mawazo mgando yaendelee. Hasa yale yahusuyo imani. Hivi kama kina Galileo wa Galileo hawakuhoji baadhi ya mambo bado leo tungeambiwa dunia ni mstatili na jua linazunguka toka mashariki kwenda magharibi? Kama hawakubali adhabu ya kifo kwaa kuhoji leo tungekuwa wapi? Nimeamua kuweka hapa chini maoni ya mmoja wa wachangiajia ambaye hataki watu wahoji uhalali wa papa anayeongoza watu zaidi ya bilioni moja kuchaguliwa na wazee wanaume wasiozidi mia moja. soma sehemu ya maoni hayo hapa chini.
"Nakumbuka uliwahi kuandika katika gazeti la Rai ukihoji uhalali wa uchaguzi wa Baba Mtakatifu anaye chaguliwa na Makardinali na kuongoza kanisa zima! Wewe ni Padri mkatoriki unaye hoji uhalari wa Baba Mtakatifu?! Zaidi umehoji ukweli wa mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu utumiaji wa Kondomu. Kama "Padri" wa kwanza mkatoriki umeunga mkono matumizi ya Kondomu, kama kinga dhidi ya Gonjwa hatari la Ukimwi.Haya yote yamekupatia sifa katika ulimwengu unaopinga msimamo wa Kanisa katoliki katika masulala mbalimbali yanayo husu maadili"
Mambo sasa yameanza kubadilika. Huko Uchina wamebariki maaskofu katoliki bila mkono wa Vatican. Wametolewa macho lakini wachina wameendelea. Huko Marekani wamemkabidhi uaskofu mtu aliyeoa. Sasa hapo ndipo utaona watu wameanza kuhoji na kutekeleza mambo ambayo awali yalikuwa mwiko kuyahoji. Miaka ya sitini Mwanaharakati Malcom X, katika moja ya hotuba zake alisifia sana Uchina kwa kuwa nchi ambayo ilikuwa ikifanya maamuzai yake mengi bila kuwasikiliza mabwana wa magharibi na mavyombo yao yanayoitwa UN, Benki ya Dunia, IMF nakadhalika. Alibashiri kwamba China ingeendelea sana. Sote tunaona yanayotokea China. Sasa wameanza kuchoka na kutawaliwa na Vatican. Baada ya kukubali dini za kigeni kwa mbinde sana sasa wameanza kujichukulia maamuzi yao wenyewe. Wacha watu wahoji. Kama watu wasingehoji basi tungekuwa mbali sana.
6Comments:
Unajua Nkya kinachoshangaza ni kuwa waumini wengi hawajui kuwa manabii na mitume wanaowafuata ni watu waliohoji imani na tawala zilizokuwepo wakati ule. Yesu mwenyewe alishangaza watu alivyokuwa akihoji amri za Musa na desturi za wayahudi. Akapinga mambo kibao. Akabadili mambo. Akavunjavunja desturi. Unakumbuka walipomwendea na mwanamke aliyedaiwa kukamatwa akizini. Unakumbuka walipomuuliza inakuwa anakiuka desturi ya kutofanya kazi jumamosi akatoa mfano wa mchungaji mwenye kondoo aliyeanguka shimoni siku ya jumamosi. Imani ya wayahudi ilikuwa ikisema jicho kwa jicho, jino kwa jino, yeye akaitupilia mbali. Alikuwa akipenda kusema, "Musa aliwaambia hivi...ila mimi nasema..." Aliwapinga vikali wakuu wa dini, wanasheria na waandishi wa wakati ule. Walimwendea wakimjaribu kwa kila njia bila mafanikio. Wakati "mababa askofu" wa wakati ule walikuwa wakihubiri kwenye masinagogi, yeye alikuwa akichukua umati na watu na kuwapeleka milimani kwenda kuwapa somo.
Ukija kwa Martin Luther, mmoja wa waanzilishi wa imani ya Kiluteri. Alihoji kanisa katoliki bila woga. Alitaka kujua ni wapi kwenye biblia panasema kuwa unaweza kununua msamaha wa dhambi na mambo mengine mengi.
Hata kwenye siasa: wagombea uhuru Afrika wasingehoji uhalali wa wageni kuja kututawala tungekuwa tunapigishwa mijeledi hadi leo (ingawa bado tunapigishwa mijeledi ya aina nyingine leo hii!).
Cheo cha uaskofu au upadri au ushehe kinatisha sana baadhi yetu. Kuna watu wanaamini kabisa kuwa hawa watu na misalaba yao mikubwa na matasbihi huwa "wanaongea" na mungu. Hawa ni wanadamu na wengi wao uaskofu na upadri ni kazi tu kama ualimu au uaskari.
Kwanza tukianza kutazama itikadi na misingi ya imani walizosimamia na vitabu vyao wanavyoviita vitakatifu na vitukufu utagundua kuwa wanahitaji msaada wetu. Wamesimama katika misingi ya uongo na utumwa wa desturi za kuja.
Nkya naungana na wewe kwa asilimia zote.Uvivu wa kuhoji ni dhambi kama zilivyo zingine.ni lazima tuhoji,kila kitu.
Huu uvivu naapa utatufikisha kubaya. Huko Kenya si mmesikia tena padre mwingine kaoa. Yuko ndani ya reformed catholic church. Sasa wengine wakihoji uchaguzi wa papa kuna tatizo gani?
"Hao wanohoji ukatoliki wanafanya hivyo kwa sababu wako hivyo"
ingekuwa kila mtu anuwezo wa kufanya hivyo dunia ingekuwa mahali pazuri sana, uwongo ungetoweka mara moja, na unafiki pia.
Sijui kwanini mtu aamini kile asichoamini? kwanini usiseme mimi ninaamini kama anglikana, au... na ukaishi kama wao. Unakuta kuna Padre anakaa ameficha familia yake. Sijui kwanini hawawi wakweli kwa jamii wanayoiongoza. Kama mbele za mungu wao wanadang'nya hivi sisi wengine tutaacha kudang'anya.
Nimekuwa nikijiuliza mambo mengi kuhusu ukristo kwamba imekuwaje yakawa hivyo yalivyo. Ukweli ni kwamba yanahitaji imani fulani hivi kuyaelewa. Na tunaambiwa kuwa "mambo hayo yamefichwa" na eti tutafunuliwa huko mbinguni tukifika. Nashangaa.
Mfano ni misimamo mingi ya Ukristo ambayo haina mashikio ya kibiblia. Ni mawazo ya watu fulani fulani tu lakini tunambiwa haitupasi kuyahoji.
Falsafa inaniruhusu kurejea imani yangu upya, nijue inakuwaje ninakiamini kitu ambacho sikielewi halafu naambiwa ati nisubiri ntakielewa mbinguni kwa baba!
Nakubaliana na mtazamo huu wa kuhoji. Kila kitukihojiwe ikiwezekana. Tuelewe kwa nini tunaaminishwa hivyo tunavyoaminishwa.
I want to encourage you to definitely continue your great
job, have a nice evening!
selaput dara buatan
selaput dara keperawanan
selaput keperawanan
Jual Selaput Dara
selaput dara palsu
selaput dara
MACAM - MACAM ALAT BANTU SEX PRIA DEWASA
JUAL BONEKA SEKS FULL BODI TERBARU
JUAL VAGINA PANTAT BERTATO GETAR SILIKON
JUAL TENGA ALAT BANTU SEX
JUAL ALAT BANTU ONANI FLESHLIGHT
JUAL VAGINA PINGGUL FULL SILIKON
JUAL VAGINA BULU GETAR
MACAM - MACAM ALAT BANTU SEX WANITA DEWASA.
JUAL VIBRATOR FANTASY BLISS MURAH
JUAL ALAT BANTU WANITA VIBRATOR THORN DRAGON
JUAL SEX TOYS HAPPY SOME
JUAL PENGGELI PUTING PAYUDARA
PENGGELI VAGINA TERBARU MIC
JUAL C-STRING ALAT SEX WANITA
PENGOBATAN DAN OBAT KESEHATAN HERBAL ALAMI
SEMENAX OBAT HERBAL PENYUBUR SPERMA
OBAT PERANGSANG UNUTUK PRIA ATAU WANITA
OPIUM SPRAY
JUAL PERANGSANG RED SPIDER CAIR
OBAT DAN ALAT PEMBESAR PENIS
VMENPLUS HERBAL
VIMAX PEMBESAR PENIS DEWASA
MAXMAN CAPSULE
PRO EXTENDER
VMENPLUS
VMENPLUS HERBAL
PEMBESAR PENIS ALAMI
OBAT EJAKULASI DINI
OBAT VMENPLUS
Post a Comment
<< Home