Askofu agawa kondomu
Alhamisi ya tarehe 7 Juni 2007, BBC ilirusha kipindi cha Hard Talk ambapo mwandishi maarufu Steven Suckur alifanya mahojiano na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Rusternburg Nchini Afrika ya Kusini. Askofu huyo, Kevin Dowling alikiri kugawa kondomu kwa watu ili wajikinge na maambukizi ya UKIMWI. Alisema kwamba yeye kama askofu ameshuhudia mengi, anaona watu wakifa ambapo pengine wangestahili kupona. Alisema katika moja ya kliniki sehemu hizo, asilimia 50 ya wanawake wanaohudhuria kliniki ya wajawazito wameambukizwa virusi vya UKIMWI. Wengi wa wanaothirika ni wahamiaji masikini kutoka katika majimbo yenye hali mbaya sana kimaisha hase jimbo la Eastern Cape. Baadhi ya wahamiaji hao huja kutafuta namna ya kujikwamua kimaisha katika maeneo hayo ambapo kuna mgodi wa madini, lakini wengi hasa wanawake hujikuta wakijihusisha na ngono kama njia ya kujikimu baada ya kukuta hakuna cha kufanya.
Alipoulizwa kama haoni huku ni kupingana na Vatican, Askofu huyo ambaye pia alikuwa mmoja wa wapambanaji wa mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini humo alisema ni kweli mtazamo wa kanisa si huo lakini yeye anaangalia hali halisi na mazingira aliyomo. Anasema akiwatembelea watu katika maeneo hayo wanaoishi kwenye vibanda vibovu kabisa anawakuta wengi wakiwa katika hali mbaya sana jambo linalomfanya ahisi kwamba wangeweza kupona kama wangejikinga. Hilo linamsukuma kuwagawia kondomu watu wengi ili kuponya maisha yao na madhara yanayoambatana na UKIMWI. Anaendelea kusema kuwa watu anaowahudumia si wakatoliki tu bali ni kutoka katika dini na madhehebu mbalimbali na kwamba anachofanya ni kujaribu kuwasaidia watu kutua mizigo na si kuwatwisha kama neno la bwana linavyonena!
10Comments:
Karibu tena, Umetukuta tuko vilevile, hata sisi huwa tunatoroka mambo yakiwa vile. Lakini kubwa ni uzima na kuonana kesho kama tulivyoonana tena leo.
Ila huyu askofu ana moyo wa ujasiri sana kufanya yale ambayo wenzake wanayafumbia macho.
Tumpe nafasi anaweza akaokoa maisha kadhaa.
Vipi masomo ulimaliza, na hilo baridi halikudhuru? Vipi wale jamaa wa chini ya madaraja, wana-"survive"?
Nilikuwa sijapita mitaa hii kwa muda. Karibu tena!
sawa !
Duu huyu inabidi atafutwe.
Ili atoe mengi zaidi anayoyajui ili wengine nao waige.
huna mpya babu? acha longo longo leta habari mpya ni miezi minne sasa unakomaa na issue moja we vipi? take a look on other blogers au unaumwa...
Mkuu upo, nimepita kwako leo. Naona shetani wa uzembe amekutembelea kama mimi, usimjali, kaza buti mzee. Sie tunajikongoja
I don't understand. What's your language?
auto parts said what yaou language
Auto Parts
hhansnn NANJN ajjkjk hjks jhkj hhsjajjk skkm dont understand?
Auto Parts
in wich country do you speak this language???
Post a Comment
<< Home