Thursday, February 09, 2006

umeshasoma Makuhadi wa soko Huria?

Kama hujakisoma basi umekosa mengi. Nilikisoma mara ya mwanzo mwaka 2003 nikakirudia 2004 nimemaliza kukirudia tena mwaka huu. Chachage si mchezo. Ameandika. Ni riwaya yenye matukio yanayoendana na hali halisi ya Tanzania. Ukikisoma huwezi kushangaa kwa nini Chinua Achebe alikimbia nchi baada ya kitabu chake cha A man of the people. Alimaliza kitabu chake kwa kuonyesha kwamba jeshi limepindua nchi. Na ikapinduliwa baada ya muda mfupi. Wengi walidhani alihusika. Lakini wapi mwenyewe anasema ni kule kuisoma jamii na kuielewa. Chachage ndivyo alivyoielewa jamii ya Tanzania. Amegusa kila eneo; usanii wa wabunge; rushwa mahakamani; waandishi wa habari kuingizwa mtegoni; na mengineyo. Kitabu kina historia nzuri sana. Kuna michapo ambayo hutajutia wala kitabu hakitakuwa kirefu kukisoma. Mchapo wa mzungu kala fenesi kwa mfano au wa padre huko Musoma ambaye aliamua kumpa mtoto shilingi mia na mama shilingi 20! Soma tafadhali. Utakutana na jinsi Salama mke wa Mjuba alivyoamua kumpa mwanae jina la Mchungaji anayeombea vita huko Marekani baada ya kuokoka. Kitabu kimekamilika. Ujuhadi unavyofanywa na watu wenye nyadhifa. Elimu waliyo nayo waze wetu nakadhalika ni mambo ambayo yamesheheni ndani ya kitabu Hicho. Soma Makuhadi wa Soko Huria ufaidi.

5Comments:

At 11:45 AM, Blogger Reggy's said...

Inda, Muhtasari wa Kitabu hicho kama ulivyouleta kwenye blogu unamaanisha kuwa kweli ni kizuri sana. lakini sisi tulioko huku, opposite ya ughaibuni tutakipataje, lini? Pse, Saidia kueleza kinaweza kupatikanaje kwa haraka.

 
At 6:53 PM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

mh ja! nilidhani kitabu hiko kinapatikana Tz. kwani prof. Chachage si yuko pale UD? pia hata mimi nina hamu sana ya kukisoma....

Prof. Chachage mimi humuhusudu sana kwa jinsi anavyoyafurumusha bila huruma. nakumbuka jinsi alivyomfurumusha hata bwana Mungai na mambo zake za kuban HAKIELIMU...huwaga ninapata feeling kuwa mtu kama Prof. Chachage akisimamishwa na umoja wa upinzani kama presidential contestant...kuna uwezo wa kufanya mabadiliko Tanzania...japo kwa kuwa na namba nzurio tu ya ma MPs...na angalau kukabiliana na JK maana kwa sasa JK anaenda vizuri!

cheers!

 
At 11:22 PM, Blogger boniphace said...

Ni kikubwa hivi kama mvivu Miruko hutaweza kukisoma lakini kizuri sana. Nkya nashukuru umewahi kuanza kufanya kazi hii tuliyowahi kuzungumza na Jeff kuhusu kuweka muhtasari wa vitabu katika blogu maana umma wa watanzania wengi hawasomi siku hivi ni bora tukawasomesha hata kwa muhtasari hivi hivi hongera sana. Kwa kazi nzuri. Wikim ijayo nitakuwa na Bob Woodward kwangu hapa na baadaye nitawasilisha kidogo pale Kasirini kuhusu kumbukumbu ya Watergate na Nixon.

 
At 11:37 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Binafsi sijawahi kukisoma kitabu hicho.Lakini tambo alizotuwekea Nkya zinatosha kunifanya nikabwe na kiu ya kukisoma.Kinapatikana wapi na vipi ndio swali gumu hapa.Kama alivyodokeza Makene,kusoma ni muhimu sana,dunia inazunguka,lazima nasi tuzungushe bongo zetu kwa kusoma mambo mbalimbali.

 
At 4:23 PM, Blogger Indya Nkya said...

Msangi sasa sijuhi utakipataje lakini kama ungeweza kumwagiza mtu aliyepo Dar anaweza kukinunua pale TPH kilikuwa kinauzwa 10,000. Mimi nina nakala yangu moja. Kwa kweli ni kitabu kizuri ukikosa kukisoma!!!

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI