Friday, May 06, 2005

Wananchi na kuwapokea viongozi

Hivi tutaacha lini hii tabia ya kuwaambia watu waache kazi zao kwenda kupokea viongozi? Hii ni dalili mbaya lakini sijuhi kama inamwonyesha kiongozi kwamba kuna mzigo mkubwa unaomkabili. Sijuhi kama mtu mwenye shughuli yake ya maana ya kufanya ataicha na kwenda kukaa barabarani kumlaki kiongozi. Kiongozi anapaswa ajue kwamba akiona umati mkubwa sana aelewe wengi wao hawana shughuli ya kufanya. Badala ya kufurahi na kushangilia kwamba amepokelewa kwa kishindo ajue ana mzigo wa hawa ndugu- nina maana mzigo wa kuzalisha kazi za kufanya. Wengi wa wapokeaji hao bila shaka ni vijana (sina maana ya vijana wenye umri wamiaka 50 na kuendelea). Hili ni kundi ambalo limeathirika sana kwa kukosa shughuli ya kufanya. Kiongozi mwenye mtizamo mpana asifuraie kupokewa kwa kishindo, aione hiyo kama changamoto mbele yake. Aone kwamba watu wanaompokea, kumsikiliza na kumpamba siku nzima asilimia kubwa hawana cha kufanya. Wenye cha kufanya wako kwenye shughuli zao. Cha muhimu zaidi na zaidi ni kutowalazimisha watoto wadogo washiriki katika mapokezi kama hayo.

1Comments:

At 11:29 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Au kama wanaompokea wana kazi, basi kiongozi huyo ajue kuwa shughuli za uzalishaji katika taifa lenye matajiri asilimia moja na masikini asilimia 99 zimesimama!

 

Post a Comment

<< Home

KITABU CHA WAGENI