Saturday, December 17, 2005

Igizo limeisha, tungoje miaka mingine mitano

Mchezo wa kuigiza umekwisha. Miaka mingine mitano wananchi watalishwa tena maneno, pilau, khanga, sukari watauza tena kura zao. Mchezo unaendelea. Lakini mchezo huu utaendelea hadi lini? Na watanzania tulivyo hatutawauliza wale walioshinda chochote hata kama hawatatimiza moja kati ya walioahidi. Lakini hata hivyo ni wangapi tunakumbuka hata ahadi zenyewe? Pilau na khanga na fulana zinatosha. Jamaa mmoja kaniacha hoi sana. Ameniambia jinsi ambavyo bado kuna kibarua kigumu mbele yetu. Alishuhudia watu wakibishana baada ya kampeni. Hawakubishana chochote kuhusu yaliyozungumzwa kwenye mkutano wa kampeni. Ubishi ulikuwa juu ya vifaa na magari ya vyama vyao. Mmoja akiwa anasema umeona spika za chama chetu? Ni nzito bwana si mchezo. Mwingine akamwambia acha utani, uliona gari walilokuwa wakitumia wagombea wa chama changu walipokuja hapa? Kazi ipo. Kwa kweli kama tunataka mabadiliko inabidi tusilale usingizi. Tupambane kweli.


Wednesday, November 23, 2005

Bendera ya Uingereza yafanyani katika tovuti ya CHADEMA?

Ndesanjo amekuwa akipigia kelele matumizi ya lugha ya kiingereza katika tovuti za kitanzania. Sasa leo katika kuipitia tovuti ya CHADEMA nimeona wameweka bendera ya Uingereza juu kabisa kwenye tovuti yao. Hiyo bendera inafanya nini hapo? Mimi sijuhi sababu labda kama kuna anayefahamu anisaidie.

Tuesday, November 22, 2005

UKIMWI bado ni tishio

Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia UKIMWI, UNAIDS kwa kushirikiana na Shirika la Afya duniani, WHO limetoa taarifa ya mwaka inayoonyesha jinsi UKIMWI ulivyo bado ni tishio hasa Afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Unaweza kuisoma taarifa hiyo kwa kubonyeza hapa

Friday, November 18, 2005

Kiswahili kitolewe utumwani kwanza

Jeff Msangi kaanzisha mjadala wa kiswahili katika blogu yake. Ametoa hoja za msingi ambazo zaweza kujadiliwa. Ili mjadala ule unoge naongezea makala iliyoandikwa na Prudence Karugendo anayetoa hoja kwamba tuanze kukitoa kiswahili utumwani kwanza. Hoja yake ni kwamba kiswahili kimeazima maneno mengi sana ya kiarabu wakati tuna lugha kwa mamia za kibantu ambazo tungeweza kutumia maneno yake na kubadilisha mengi ya kiarabu. Soma makala yake hapa na mjadala uendelee.

Uvutaji na unywaji wa pombe na Saratani tena

Engidio amesema kwamba kuna watu wametishwa sana na habari niliyoiweka hapa kuhusu unywaji pombe na Saratani. Sasa naweka kiungo kingine kuonyesha msisitizo wa jambo hili tena. Soma Hapa uone mambo zaidi kuhusu pombe sigara na saratani.

Wednesday, November 16, 2005

Saratani yazidi kuongezeka shauri ya kubwia pombe

Soma habari hii inayotoa onyo juu ya ongezeko la saratani kutokana na kunywa kupindukia. Bonyeza hapa

Tuesday, November 15, 2005

Uhuru si urithi

Nimekutana na nukuu hii:

"No people are really free until they become the instrument of their own liberation. Freedom is not a legacy that is bequeathed from one generation to another. Each generation must take and maintain its freedom with its own hands." By John Henrik Clarke

Kila kizazi inabidi kipambane kujipatia uhuru wake.

Sunday, November 13, 2005

Makala za Prudence

Mzalendo mmoja aitwaye Prudence Karugendo amenitumia makala zake ambazo angependa zisomwe na watanzania wengine ili kubadilishana mawazo na kuleta changamoto katika kujadili mustakabali wa nchi yetu. Nimeweka kona ya makala zake kwenye blogu hii chini ya Kona ya Padre Karugendo. Hawa ni watu wawili tofauti. Mmoja ni Privatus mwingine ni Prudence. Kwa leo naweka makala zake tatu. Moja inaitwa kiini macho cha kusamehewa madeni. Pamoja na mambo mengine anaongelea misamiati migumu inayotumiwa katika kuandika mambo ya kiuchumi. Anahoji pia kwa nini tunaambiwa sasa tusherehekee kusamehewa madeni wakati ambao hatukuambiwa yalikopwa lini, na nani, kwa ruhusa ya nani na yalifanyia nini? Isome hapa. Nyingine mbili zinahusu amani. Moja anauliza kama kweli Tanzania kuna amani au ni kiini macho cha amani. Isome kwa kubofya hapa. Nyingine anauliza je ni upinzania au chama twawala kinachohatarisha amani? Isome hapa

Friday, November 11, 2005

Tanzania yaingizwa kwenye kapu la Misaada mingine ya Marekani

Tanzania imefanikiwa kuingizwa katika mpango wa misaada wa Marekani unaoitwa Millenium Challenge Corporation (MCC). Ili uingizwe humo ni lazima kwanza uwe na utawala bora kwa vigezo vya jamaa wa Benki ya Dunia na Wizara ya Fedha ya Dunia (International Ministry of Finance), wenyewe wanaita International Monetary Fund. Sasa tungoje majivuno na matusi toka kwa mwenyewe. "Wale wote mnaosema nchi haina utawala bora ni vipofu. Hamuoni hata Marekani inatambua? Nyie watanzania msioona ni watu wa ajabu sana". Tutayasikia haya karibuni. Soma Hapa habari hiyo.

Wednesday, November 09, 2005

Wanywaji wa Kahawa Huree

Tafiti zinachanganya Kweli. Tofauti na inavyoaminika kwamba kunywa kahawa kwa wingi husababisha Magonjwa ya moyo, utafiti mpya umegundua kwamba unywaji wa Coca Cola unaweza kuwa hatari zaidi. Soma hapa

Makala kuhusu Askari kuwachapa Raia

Bwana Sakito Mallya ameandika maoni yake kuhusu Askari wa Tanzania kuwapa kipigo raia. Makala hiyo ilitoka kwenye Gazeti la Rai la tarehe 3/11/2005. Unaweza kuisoma kwa kubonyeza hapa

Monday, November 07, 2005

Mabaki ya kanisa la kale yagunduliwa.

Jamaa mmoja kagundua mabaki ya kanisa ambalo pengine lilijengwa kwenye karne ya tatu au ya nne katika nchi "Takatifu"-Israel. Jamaa wanasemakwamba itavutia sana utalii shauri ya imani waliyo nayo wakristo kuhusu Kanisa, Yesu na nchi Takatifu. Wanabashiri kwamba utalii utaongezeka kwa nguvu sana. Hata kama jamaa wamedanganya ili kukuza sekta ya utalii bado watapata tuu. Soma habari hiyo hapa

Weusi hawasomi

Nimekutana na haya maneno katika mlolongo mmoja wa barua pepe. Soma uone jinsi weusi watakavyoendelea kunyonywa. Ina maana hata hii hawataisoma.
BLACKS DON'T READ

I think that will interest youREAD AND WEEP!BLACKS DON'T READ.Please Note:For those of you who heard it, this is the article DeeLee was reading this morning on a New York radiostation. For those of you who didn't hear it, this isvery deep and true! BLACKS DON'T READ. This is a heavypiece and a Caucasian wrote it. THEY ARE STILL OURSLAVES we can continue to reap profits from the Blackswithout the effort of physical slavery. Look at thecurrent methods of containment that they use onthemselves: IGNORANCE, GREED, and SELFISHNESS. TheirIGNORANCE is the primary weapon of containment. Agreat man once said, 'The best way to hide somethingfrom Black people is to put it in a book." We now livein the Information Age. They have gained theopportunity to read any book on any subject throughthe efforts of their fight for freedom, yet theyrefuse to read. There are numerous books readilyavailable at Borders, Barnes & Noble, and Amazon.com,not to mention their own Black Bookstores that providesolid blueprints to reach economic equality (whichshould have been their fight all along), but few readconsistently, if at all. GREED is another powerfulweapon of containment. Blacks, since the abolition ofslavery, have had large amounts of money at theirdisposal. Last year they spent 10 billion dollarsduring Christmas, out of Their 450 billion dollars intotal yearly income (2.22%). Any of us can use them asour target market, for any business venture we care todream up, no matter how outlandish, they will buy intoit. Being primarily a consumer people, they functiontotally by greed. They continually want more, withlittle thought for saving or investing. They wouldrather buy some new sneaker than invest in starting abusiness. Some even neglect their children to have thelatest Tommy or FUBU, and they still think that havinga Mercedes, and a big house gives them "Status" orthat they have achieved the American Dream. They arefools! The vast majority of their people are still inpoverty because their greed holds them back fromcollectively making better communities. With the helpof BET, and the rest of their black media that oftenbroadcasts destructive images into their own homes, wewill continue to see hug profits like those of Tommyand Nike. Tommy Hilfiger has even jeered them, sayinghe doesn't want their money, and look at how the foolsspend more with him than ever before). They'llcontinue to show off to each other while we buildsolid communities with the profits from our businessesthat we market to them. SELFISHNESS, ingrained intheir minds through slavery, is one of the Major wayswe can continue to contain them. One of their own,Dubois said that there was an innate division in theirculture. A "Talented Tenth" he called it. He wascorrect in his deduction that there are segments oftheir culture that has achieved some "form" ofsuccess. However, that segment missed the fullness ofis work. They didn't read that the "Talented Tenth"was then responsible to aid the Non-Talented NinetyPercent in achieving a better life; instead, thatsegment has created another class, a Buppies classthat looks down on their people or aids them in acondescending manner. They will never achieve what wehave. Their selfishness does not allow them to be ableto work together on any project or endeavor ofsubstance. When they do get together, theirselfishness lets their egos get in the way of theirgoal. Their so-called help organizations seem to onlywant to promote their name without making any realchange in their community. They are content to sit inconferences and conventions in our hotels, and talkabout what they will do, while they award plaques tothe best speakers, not the best doers. Is there no endto their selfishness? They steadfastly refuse to seethat TOGETHER EACH ACHIEVES MORE (TEAM)! They do notunderstand that they are no better than each other ofwhat they own in fact, most of those Buppies are butone or two paychecks away from poverty. All of whichis under the control of our pens i our offices and ourrooms. Yes, we will continue to contain them as longas they refuse to read, continue to buy anything theywant, and keep thinking they are "helping" theircommunities by paying dues to organizations which dolittle other than hold lavish conventions in ourhotels. By the way, don't worry about any of themreading this letter, remember, THEY DON'T READ!!!!BLACKS DON'T READ"Euseby

Saturday, November 05, 2005

Kwa nini?

Umeshawahi kujiuliza kwa nini Amani Karume awe rais wa Zanzibar? Kwa nini Ndugu yake ni balozi? Kwa nini Hussein Mwinyi ni Naibu Waziri wa Afya? Kwa nini Watoto wawili wa Nyerere ni wabunge wa kuteuliwa? Kwa nini? Nimeulizwa. Mimi nikasema kwa vile ni wanasisiemu wazuri. Nikaulizwa je ni wao tuu ambao ni wanasisiemu wazuri? Je ni kwa vile baba zao walikuwa Rais kwa vipindi tofauti? Sijuhi.

Saturday, October 29, 2005

Uganda imeendelea sana, haiitaji msaada wa IMF

Kuna habari inayoifagilia kweli nchi ya Uganda ilivyopiga hatua ya kimaendeleo. Sijuhi. Kama vigezo walivyotumia ni sahihi basi Uganda iko mbali. Lakini kama ni suala la kucheza na takwimu tuu, basi kila nchi inaweza kuonekana imeendelea au haijaendelea. Naziogopa sana takwimu japo nacheza nazo kila ukicha. Kwa upande mwingine licha ya maendeleo haya, bajeti ya uganda inafadhiliwa kwa asilimia kama 50 hivi na wahisani wa nje. Innocent tuambie. Mtaani Uganda mambo yakoje? Soma habari hiyo hapa

Barua kwa rais mtarajiwa

Kuna Wazalendo wawili waliomwandikia rais mtarajiwa barua wakimtafadhalisha kwamba serikali ijayo ifanye mambo ya muhimu kwanza. Barua hiyo imetoka kwenye gazeti la Rai la Alhamis tarehe 27/10/2005. Unaweza kuisoma kwa kubonyeza hapa. Ukiwa na la kuwauliza waandikie: sakitomalya2001@yahoo.co.uk

Thursday, October 27, 2005

Ethan akiri ugwiji wa Ndesanjo

Ethan Amekubali kwamba Ndesanjo Si mchezo jinsi alivyoweza kuhabarisha wasomaji wake kilichokuwa kinaendelea katika mkutano wa Pop Tech huko Camden. Kilichomuacha hoi ni jinsi Macha alivyoweza kuandika karibu kila kitu kilichokuwa kikiendelea tena akitafsiri kwa kiswahili. Lazima na mimi nikupongeze kwa hili ndugu yangu. Ongeza bidii. Lisha jamii habari Mangi. Ukifungua blogu ya Ethan utakumbana na hiyo habari. Tumpe Ndesanjo hongera zake kwa hili. Ukibonyeza HAPA utasoma kwa undani alichosema Ethan

Wednesday, October 26, 2005

Sawa si sawasawa tena

Fide aliuliza binadamu wote ni sawasawa? Macha sasa nadhani huitaji mjadala tena. Kuna huyu mtu anayeitwa Magufuli -Waziri wa Ujenzi. Anasifika sana kwamba anachapa kazi. Lakini mgongoni mwa huo uchapa kazi ana mambo ya kusikitisha mno. Soma hapa uone moja ya mambo yake mengi ya ajabu.

Monday, October 24, 2005

Mijadala, mijadala na mijadala

Leo nilikuwa kwenye mjadala mmoja kuhusu mambo yanavyokwenda hapa Afrika ya Kusini. Waongeaji katika mjadala ule walikuwa rais wa zamani F.W. De Klerk na mtu anayeitwa Tokyo Sexwale. Huyu Sexwale ni mweusi ambaye alikuwa kati ya wapambanaji waliofungwa miaka mingi huko Robin Island. Lakini baada ya miaka 11 tuu ya utawala wa weusi amekuwa ni tajiri mkubwa sana. Mjadala ule ulikuwa wa kufurahisha. De Klerk anasema kwamba weupe wanaogopa sana hiki kinachoitwa Black Empowerment kwa sababu hatma ya weupe haijulikani na sasa baadhi wameanza kuwapeleka watoto wao nje ya nchi wakihofia kitakachotokea kwani huenda wakatengwa kiajira na mambo mengine. Anadai pia kwamba umasikini umeongezeka licha ya uchumi kukua. Kwa mfano anasema pengo kati ya walio nacho na wasionacho limekuwa sasa zaidi ilivyokuwa kabla ya kumalizika kwa utawala wa ubaguzi. Idadi ya weusi wasio na ajira imeongezeka kuliko kabla ya utawala wa kibaguzi. Madai yake kwa kweli ni ya msingi hasa ya ongezeko la umasikini na kukua kwa pengo la matajiri na masikini. Hoja yake nyingine ni kwamba kuwawezesha weupe haina maana kuwapa kazi za juu au fedha za biashara hata kama hawana uwezo huo. Uwezeshaji mkubwa ni kuwaelimisha ili waweze kushindana katika soko. Hili nalo halina ubishi.
Sexwale akasema kwamba licha ya kelele zote zinazopigwa, bado weusi hawajapata chochote cha kutisha. Ametoa mfano kwamba Katika soko la hisa la Johanesburg, weusi wanamiliki asilimia 1.8 tuu ya trilioni moja ya hisa zote. Hii ni baada ya miaka 11 ya utawala mpya. Akasema pia kwamba maajabu yasitarajiwe kwa kipindi kifupi kama hiki. Kwa maneno mengine watu weusi pia wasitarajie kila kitu kitamalizika kwa miaka 11 tuu. Lakini hakutuambia yeye amewezaje kuwa tajiri hivyo kwa miaka 11 tuu.
Niliwahi kusema huko nyuma kwamba Afrika ya Kusini imeshazalisha tabaka jingine la matajiri wachache weusi ambao wanapewa mitaji ya biashara na vyeo vikubwa badala ya kuimarisha elimu kwa weusi kwa ngazi zote kwanza. Leo hii kuna mamilioni ya watoto weusi hawana madawati wala viti vya kukalia mashuleni. Badala ya kuanza kuimarisha kizazi kijacho ili kiweze kushindana na hao weupe miaka ijayo wanazalisha mabilionea wachache halafu wanaacha lundo la weusi wakiangaika pasipo kazi wala elimu nzuri. Ukisikiliza mijadala yao utagundua kazi bado ipo.

Sunday, October 23, 2005

Dawa za ARVs husababisha magonjwa ya moyo

Kuna habari hii hapa inayosema kwamba dawa za kurefusha maisha husababisha magonjwa ya moyo. Tafadhali isome. wakati fulani kwenye blogu yangu ya kiingereza niliandika kuhusu hili jambo nikijenga hoja kwamba wale walioshtaki kampuni iliyokuwa ikitengeneza dawa za kutuliza maumivu ziitwazo VIOXX na baada ya kuzitumia mgonjwa magonjwa ya moyo hawakuwa wajinga na inawezekana kabisa kwamba kampuni hizi zinazotengeneza ARVs baadaye zikashtakiwa. Jamaa mmoja kanijia juu kishenzi. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba dawa hizi zina madahara makubwa sana katika mwili.

Thursday, October 20, 2005

KILA NCHI INATOA ELIMU KWA KISWAHILI

Nimekutana na maoni ya mzalendo mmoja kuhusu matumizi ya lugha ya kiswahili nikaona nishirikiane nanyi kupata anachosema: maoni yake nayaweka hapa chini:
KILA NCHI INATOA ELIMU KWA KISWAHILI
Mzee Nimejifunza yafuatayo na siyo vibaya tukichangia:
(1) Kule Mbeya, Bukoba, Moshi, Iringa na sehemu nyingi zenye baridi watu wanakunywa zaidi CHAI ya kahawa. Wakati sehemu za joto joto kama Dar hawana chaguo maalumu, hata CHAI ya siturungi, milo, cocoa,zote zinanywewa bila mpangilio wowote.
(2) Yule NYERERE wa Msumbiji aliyekuwa akiitwa SamoraMasheli alikufa kwa ajali ya ndege na wala siyo gari.Na NYERERE wa Libya, Gadafi huenda akawa ndiyekiongozi wa Afrika aliyekaa madarakani kwa muda mrefu. Somali wao hawana NYERERE bado, hii ni kwa ajili yamachafuko ya kivita.
(3) Kila nchi duniani hutumia lugha ya KISWAHILI kuunganisha jamii zao za makabila mbalimbali na kufundisha katika ngazi na nyanja zote za elimu. Mfano, Uganda, Malawi, Zambia, n.k., wao hutumia KISWAHILI cha Kiingereza. Gabon, Congo, Senegal, n.k.wao hutumia KISWAHILI cha Kifaransa; England, Wales,Marekani na Scotland hutumia KISWAHILI cha Kiingereza;Misri, Libya, Tunisia, n.k. wao ni KISWAHILI chaKiarabu; Uchina nasikia ni KISWAHILI kinachoitwa Mandarin; Arjentina, Kolombia, Chile, n.k. niKISWAHILI cha Kiispania, Urusi ni Kirusi, Ureno naBrazili na Angola ni Kireno, n.k. n.k.?
(4) Nchi yetu Tanzania ambayo KISWAHILI chake ni Kiswahili, ndiyo nchi pekee duniani ambayo imetumia KISWAHILI kuunganisha watu wake wa makabila mbalimbali halafu maajabu imekataa kutumia KISWAHILI hicho hichokatika kutoa na kupokea elimu mashuleni na vyuoni mwake !!!!!!!!!!!!. Hii inamaanisha kuwa kinachofundishwa mashuleni kwetu siyo elimu bali mahudhurio ya semina ndefu ndefu tulizozibatiza majina; Form IV, IV na madigirii.Nadhani vyeti vyake sahihi vingeitwa VYETI VYAMAHUDHURIO YA SEMINA YA FORM IV, n.k. na siyo vyeti vya ELIMU. Neno elimu ni pana na kubwa. Hivyo lisitumike pasipostahili. Vinginevyo ni sawa na kudai kuendesha kilimo cha minazi wakati shamba zima umepandikiza makuti mabichi!! Na misingi ya kukataa kutoa elimu kwa KISWAHILI ndiyo chanzo cha umaskikini wetu pamoja na kuwa matajiri wenye raslimali lukuki:watu takribani milioni 40, ardhi yote yenye rutuba,maji hadi kiama - yawe chumvi au baridi, hali ya hewa murua - hakuna vimbunga-matetemeko ya ardhi-baridi na joto zinazoua, madini kila aina nchi nzima, mbuga za wanyama duniani hakuna na lugha ya KISWAHILI iliyo pevu. Nchi zote duniani zinapotoa elimu kwa KISWAHILI chake,siyo wapumbavu, hivyo na sisi tuanze leo. Anayedai lugha haijakuwa bado, mwambie akupangia lugha ya kwanza hadi ya mwisho kama ataweza, hawezi, kwani hakuna kitu kama lugha changa. Anayesema tutafsiri kwanza vitabu kutoka lugha za kigeni - muulize mbona tunatumia maneno kama motokaa, oksijeni, pasipoti,kompyuta, redio na wenzetu nao wanatumia maneno yetu kama panga, shamba, safari, kimeharibika nini?. Anayedai hatutatambulika duniani - kwanza, waulize duniani kuna nchi ngapi zisizotumia hiyo lugha ya kigeni tunayoikumbatia - na wanatambulika zaidi yetu??pili wafahamishe kiswahili kinasambaa kama moto wa mbugani. Wasikilize Wakongo, Waburundi na Rwanda,Wakenya, Wamsumbiji, n.k. wanavyokiongea. Tatu waombe wasikilize redio Ujerumani, Peking, Sauti ya Amerika,BBC, n.k. Mwisho waelimishe kuwa wanapodai kuwa lugha haijakuwa, hatutatambulika, n.k huwa wanamaanisha,tena bila kujitambua wala aibu, kuwa wao ni wanyonge,dhaifu, wasiojiamini, wasioweza kujiendesha wenyewe,watumwa - haswa haswa huko vichwani mwao na wasiotakakuelimika.
Kwaheri,
Kiswahili chema,

Wednesday, October 19, 2005

Paper ya Prof. Othman

Profesa Haroub Othman wa Chuo Kikuu cha DSM alikuwa msemaji Mkuu kwenye Mhadhara wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ulioandaliwa na chuo hiki hapa tarehe 14/10/2005. Mada aliyotoa ilikuwa: Nyerere an Intellectual in Power. Isome kwa kubonyeza hapa

Tuesday, October 18, 2005

Misaada ya Nje jamani!!

Katika soma soma yangu nimekutana na sentensi ifuatayo: "At one point in Tanzania, the total for government wages and salaries (which are taxed) was $100 million, while the salary bill for technical assistants supplied under aid programs (and not taxed) was $200 million". Yaani mishahara inayotokana na misaada ambayo hailipiwi kodi kwa wakati huo ilikuwa mara mbili ya ile serikali. Tunapoteza kodi kiasi gani?

Monday, October 17, 2005

Makala ya kumkukumbuka Mwalimu

Niliandika makala kumkumbuka Mwalimu J. K. Nyerere ambayo ilitoka kwenye gazeti la Rai la tarehe 13/10/2005. Nakuwekea hapa uisome

Parched Earth

Padre Karugendo amemwandikia barua ya pongezi Mwandishi wa Kitabu cha Parched Earth mama Elieshi Lema. Ukisoma barua hiyo unaweza kupata mawili matatu yaliyomo kwenye kitabu hicho ambacho ni kizuri na muhimu mno. Unaweza kuisoma hapa. Kumbuka makala zake nyingine zipo kwenye kona yake ndani ya Blogu hii

Maajabu haya!!

Jamaa wa Kanisa la Ephata wameamua kwenda Israel kuombea uchaguzi mkuu na pia mahusiano mazuri kati ya Israel na Tanzania. Wakati huo huo Huyo kiongozi wao anawambia watanzania wengine waombee uchaguzi. Hivi, kwa nini wasingeombea wote nyumbani mpaka waende Israel? Kama anaona Israel ni mahali patakatifu ambapo sala zao zitakubalika zaidi, kwa nini sasa awaambie watanzania wengine wanaosalia nje ya Israel waendelee kuomba? Ndesanjo atalieleza vizuri hili. Halafu anataka uhusiano na Israel uwe mzuri, sababu zilizofanya uwe mbaya ni zipi? Je sababu hizo sasa si za msingi tena? Israel inaheshimu haki za Wapalestina? Soma habari hiyo hapa.

Sunday, October 16, 2005

Makala Mpya ya Padre karugendo

Kuna makala mpya aliyoandika Padre karugendo kuhusu kumbukumbu ya Askofu Mwoleka lakini ina ujumbe mzito wa "NDOA NYOYO". Isome hapa

Thursday, October 13, 2005

Chavez kawashitukia wamisionari

Rais wa Venenzuela Hugo Chavez ambaye ni adui mkubwa wa Marekani ameshtukia wahubiri toka Marekani na ameamua atawatimua sasa. Chavez ambaye Marekani inashinikiza kuondolewa kwake madarakani anahisi wahubiri hao ni wale wale wapiga propaganda za adui wake. Soma hapa ujionee mwenyewe.

Monday, October 10, 2005

Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Tarehe 14/10/2005, itakuwa imetimia miaka sita tangu Mwalimu Nyerere atangulie mbele ya haki. Katika kumuenzi na kumkukumbuka mzee wetu huyu, Chuo Kikuu cha Cape Town kwa ushirikiano na Jumuiya ya Wanafunzi wa Afrika mashariki wanaosoma Chuo hiki wamendaa mhadhara Maalum wa kumbukumbu kutafakari mchango wake kama kiongozi, mwanafalsafa, mwanazuoni na mpigania uhuru na haki za wanyonge katika bara la afrika na duniani kote. Mgeni Rasmi katika tukio hili atakuwa Prof. Haroub Othman wa chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam. Katika tukio hilo tunatarajia tutakuwa na wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali hapa Afrika ya Kusini na wawakilishi toka balozi mbalimbali. Huu ni mhadhara wa kwanza kuandaliwa na chuo hiki na ni nia yetu kufanya tukio hili liwe la kila mwaka. Nitazidi kuwafahamisha zaidi juu ya tukio hili.

Friday, October 07, 2005

Kichaka alitumwa na Mungu

Msemaji wa George Kichaka anakana kwamba rais wake aliwahi kusema kwamba alitumwa na Mungu kuivamia Iraq na Afrighanistan kama inavyodaiwa na mwakilishi wa mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati toka Palestina Bwana Nabil Shaath. Kukana ndio kawaida ya wasemaji wote wa serikali duniani. Cha kukumbuka ni kwamba vita hizi zote huombewa kwanza na wahubiri maarufu kama vile Bill Graham. Huyu ndiye Mungu wa Kichaka anayetaka kwenda kuua wairaq. Soma habari hiyo hapa

Tuesday, October 04, 2005

Ugunduzi mpya huwa mgumu kukubalika

Jana nilielezea washindi wa tuzo ya Nobeli katika Utibabu walivyogundua kwamba vidonda vya tumbo kwa asilimia kubwa husababishwa na bakteria na matibabu yake ni rahisi yaani kutumia "antibiotics" tuu. Hawa jamaa walianza utafiti wao miaka 20 iliyopita. Walivyotangaza mara ya kwanza walichekwa sana na kuonekana ni watu wanaotaka kuleta mzaa katika sayansi. Leo ukweli umedhihirika lakini baada ya gharama kubwa ya maisha ya watu pamoja na dawa za kutibu vidonda hivyo zinazouzwa na kampuni za mabepari. Hili si tukio la kwanza; miaka mingi iliyopita ugonjwa unaoitwa "Scurvy" ulikuwa ukiwasumbua sana watu. Akajitokeza mwanasayansi mmoja akasema watu wasihangaike; tatizo la ugonjwa huo ni ukosefu wa vitamini C. Alichekwa vibaya sana. lakini baadaye ikadhihirika kwamba ugunduzi wake ni ukweli mtupu. Sasa hivi kuna mtaalam mmoja anayeitwa Dr. Mathias Rath; anapambana na mambo mawili makubwa. Kwanza anasema magonjwa ya moyo husababishwa na upungufu wa vitamini C. Anauliza kwa nini wanyama hawapati magonjwa ya moyo lakini sisi binadamu tunayapata? Jibu ni kwamba miili ya wanyama inazalisha vitamini C ambayo ni muhimu katika kuzuia matatizo ya moyo wakati miili ya binadamu haina uwezo huo. Kwa maneno mengine tunahitaji vitamini C za kutosha toka kwenye vyanzo vingine. Jambo la pili analopambana nalo ni matumizi ya vitamini na virutubisho katika kupambana na UKIMWI. Katika mapambano haya anakumbana na upinzani wa kutisha. Upinzani uliogeukia majukwaani badala ya maabara. kampuni za dawa hazitaki kusikia dawa mbadala kabisa. Wanataka kuendelea kuuza dawa zao.
Nimalizie kwa kutoa nukuu hii: "New Truths go through three stages. First they are ridiculed, second they are violently opposed and then finally, they are accepted as being self-evident". Arthur Schopenhauer

Monday, October 03, 2005

Makala nyingine za Padre Karugendo

Niliahidi kutundika makala nyingine za Padre Karugendo. Leo nazitundika kutimiza hiyo ahadi. Anza na hii inayosema "baada ya uchaguzi" kwa kutwanga hapa, halafu kuna hizi nyingine mbili nazo kuhusu uchaguzi pia. Zisome hapa na hapa. Soma nyingine anayochambua mawazo ya Kadinari Pengo kuhusu mchakato wa watakatifu kwa kubofya hapa. Mwisho kuna makala anayojadili kitabu kinachoitwa "Parched Earth" kilichoandikwa na Elieshi Lema. Kabla sijakuelekeza kwa kuisoma makala hiyo nizungumzie kidogo kitabu hicho. Hiki kwa mawazo yangu ningemshauri kila kijana akisome. Kila mzazi pia akisome. Ukikisoma utaona hali halisi ya maisha ambapo wazazi tunaacha vijana wetu wakielea bila maelekezo na mafundisho ya kutosha kuhusu maisha. Kitafute ukisome. Hutajuta kukisoma sana sana ukishasoma utataka na mwenzio akisome. Sasa uisome makala ya Padre Karugendo kuhusu kitabu hicho hapa

Bakteria na vidonda vya tumbo

Tofauti na ilivyozoeleka na kuaminika siku zote kwamba vidonda vya tumbo husababishwa kwa kiwango kikubwa na mifumo ya maisha na mfadhaiko(stress), sasa wataalam wamegundua kumbe zaidi ya asilimia zaidi ya asilimia 80 husababishwa na bacteria waitwao "Helicobacter pylori". Wanasayansi wawili toka Australia Barry J. Marshall na J. Robin Warren wamepata tuzo ya Nobel kwa ugunduzi huu. Soma mwenyewe habarii hiyo hapa. Wiki hii pia washindi wengine wa tuzo za Nobeli wa Amani, Kemia, Fizikia watatangazwa. Jumatatu ya tarehe 10/10 ndio atatangazwa mshindi wa nishani hiyo katika uchumi, huku tarehe kamili kwa mshindi katika fasihi ikiwa haijatolewa rasmi. Unaweza kusoma zaidi habari za tuzo za Nobeli hapa

Monday, September 26, 2005

Makala za Padre Karugendo tena

Naweka makala nyingine tano katika kona ya Padre Karugendo. Moja inahusu maslahi ya Taifa. Isome hapa. Soma pia hii hapa inayosema sera tofauti lakini lengo ni lile lile. Halafu kuna nyingine mbili zinazohusu utakatifu wa Mwalimu Nyerere. Zisome Hapa na Hapa. Kwa leo ya mwisho inasema Kanisa si upinzani. Unaweza ukaisoma hapa. Nitaweka makala nyingine siku za karibuni.

Sunday, September 25, 2005

Mamilioni wanaishi Kwa umasikini wa kupindukia Marekani

Wamarekani zaidi ya milioni 37 wanaishi kwa umasikini mkubwa. Hii ni kama asilimia kumi ya wamarekani wote na ni kubwa kuliko idadi ya watanzania wote. Soma mwenyewe habari hiyo HAPA

Friday, September 23, 2005

Ya Zimbabwe kutokea Africa ya Kusini

Licha ya staili ya Bob Mugabe kukamata mashamba ya Wazungu na kuyagawa kwa wazalendo kulaaniwa vikali na baadhi ya nchi, Afrika ya Kusini inataka kujifunza mbinu toka kwa Bob. Soma habari hiyo hapa

Thursday, September 22, 2005

Elimu na Kujifunza

Tarehe 25/08/2005 Chuo Kikuu cha Western Cape kiliandaa mhadhara wa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Hili ni tukio la kila mwaka kukumbuka mchango wa Mwalimu katika Elimu. Mwaka huu mzungumzaji alikuwa Dr. Rosa Maria Torres Waziri wa Zamani wa Elimu Nchini Ecuador. Mama huyu alitofautisha kati ya kupata elimu na kujifunza. Baadhi ya mambo aliyosisitiza ni pamoja na: kumaliza mtaala si sawa na kujifunza, kujifunza hakuanzii darasani, kutojua kusoma na kuandika hakumaanishi ujinga, kujifunza si kusoma vitabu tuu, Elimu si kuongeza idadi ya wanafunzi pamoja na mengine mengi. Huu ulikuwa mhadhara mzuri na wa kufurahisha.

Jamani Ujambazi!!

Ujambazi umepamba tena moto. Nasikia polisi wametangaza msako kabambe. Kama kawaida utakuwa wa siku mbili tatu halafu watakaa tena mpaka vitendo vya ujambazi vizidi tena kupindukia. Sijuhi kwa nini hilo zoezi kabambe lisiwe la kudumu. Mwaka ule walivyouawa polisi ndio kampeni kabambe ilipamba moto wakakamatwa majambazi kibao. Baada ya hapo wakakaa tena mpaka sasa ndio mpango kabambe unatangazwa tena. Sijuhi utadumu kwa muda gani tena. Lakini kwa vile mapolisi wamejeruhiwa hivi majuzi tunaweza kushuhudia tena majambazi yakikamatwa na kuadabishwa kwa nguvu ya soda.
Jambo lingine ambalo linahitaji kuangaliwa kwa makini ni huu mfumo wetu wa fedha taslimu kila mara. Hii inatokana na mfumo duni wa kifedha. Kwa mfano mfanyabiashara kukaa na milioni zaidi ya mia moja kwenye duka la fedha za kigeni. Inatia shaka kama kweli ni fedha ambazo zimefanyiwa biashara jana yake. Kama ni hivyo basi ni biashara kabambe kabisa. Kama sivyo basi kuna watu wanakaa na fedha bila kuziweka benki na hilo linatia mashaka kwa sababu aidha mfumo wa benki ni mbaya au wafanyabiashara wanakwepa mambo fulani. "Cash Economy" ni mfumo mbaya na hatari sana. Fedha taslimu zinashawishi sana majambazi. Mfano wa yale yaliyotokea Dodoma nayo ni matokeo ya mfumo wa taslimu. Mtu kuchukua shilingi milioni nane kwenda kufanya manunuzi au kulipa chochote ni hatari. Simlaumu yeyote. tatizo ni mfumo wetu. Kila kitu kinahitaji taslimu. Wakati umefika kuanza kuharakisha mabadiliko ya hali hii la sivyo huu uporaji wa fedha taslimu utaendelea na kukua kwa kasi ya ajabu.

Monday, September 19, 2005

Makala ya Kuruwiji

Naweka makala nyingine ya Padre Karugendo inayoitwa Kuruwiji. Ni makala ya kuvutia mno. Isome hapa. Soma hii nyingine hapa inayoitwa wanawake na uongozi

Filamu Mpya ya Kiswahili kuhusu UKIMWI

Nimepata taarifa kwamba Filamu mpya ya Kiswahili iliyotengenezwa Marekani iitwayo TUSAMEHE kuhusu UKIMWI inatarajia kutoka hivi karibuni. Itatoka rasmi mwezi ujayo huko Washinton D.C. na baadaye itaonekana nchi zote za Afrika Mashariki. Cha kufurahisha zaidi ni kwamba kati ya waliocheza sinema hiyo watu Saba ni wazungumzaji wa Kiswahili -watano toka Tanzania na wawili toka Kenya. Cha muhimu ni kwamba kilichowaunganisha wote hawa ni lugha ya Kiswahili. Kampuni iliyoandaa filamu hii pia imekwishatoa filamu nyingine iitwayo Bongoland ambayo inaendelea kuuzwa sehemu mbalimbali duniani.
Nadhani Filamu hii imekuja katika wakati muafaka kwa sababu mbili kubwa; kwanza tatizo la UKIMWI ambalo linazidi kukua na athari zake kuwa mbaya kila ukicha, na pili matumizi ya lugha tamu ya Kiswahili. Uwe tayari kwa filamu hiyo ambayo nataraji itakuwa nzuri na ya manufaa kwetu. Unaweza kusoma zaidi kuhusu Filamu hiyo HAPA

Friday, September 16, 2005

Makala nyingine za Padre Karugendo

Katika kona ya Padre Karugendo nimeweka makala nyingine Tano. Moja inaitwa kichwa cha Yohana Mbatizaji, nyingine Mvuvi, nyingine mbili zinahusu uchaguzi mkuu na ya mwisho inamhusu mtoto wa Afrika. Pitia uzisome.

Tuesday, September 13, 2005

Makala za Padre Karugendo

Kuanzia sasa nitakuwa naweka makala za Padre Karugendo katika blogu hii. Makala zake nyingine nyingi pia zipo na zitaendelea kuwepo kwenye blogu ya Ndesanjo. Kwa leo anza kusoma hii hapa anoyouliza Saida Kalori anagombea Jimbo gani? Halafu isome hii nyingine kutoka Tanganyika kwenda Tanzania hapa. Nitaweka kona yake kabisa ambayo msomaji anaweza kusoma makala zake wakati wowote.

Vitabu

Kuna vitabu viwili nitamshauri kila mtu avisome. Mimi nimevisoma vyote, na uzuri vinavutia kusoma na si virefu sana. Cha kwanza kinaitwa Pambazuko Gizani; kimeandikwa na Kalumuna Mboneko. Usithubutu kukikosa. Kimeandikwa kama riwaya lakini ukikisoma utajionea mwenyewe ukweli wa mambo yanayoelezewa humo ndani. Kwa maoni yangu ni kitabu cha kusomwa na kila mtu. Cha pili ni Rai ya Jenerali; kimeandikwa na Jenerali Ulimwengu. Huu ni mkusanyiko wa makala zake alizokuwa akiandika kwenye gazeti la Rai kuanzia 1993 hadi 1995. Makala hizi japo ni za miaka ya nyuma bado ni mbichi utadhani zimeandikwa leo. Tafuta ukisome. Hutajuata kukisoma. Bei zake nadhani ni za kawaida. Pambazuko Gizani ni shilingi 3,000 na Rai ya Jenerali ni 5,000.

Watanzania tuna mawazo mazuri!!

Niko kwenye Basi nasafiri toka Moshi kwenda Dar. Tukikaribia Dar mjadala unaanza kuhusu uchaguzi. Ndani ya basi kuna mama mmoja mbaye niligundua baadaye sana kuwa ni diwani wa CCM huko Moshi. Mama anaanza kusomesha vijana umuhimu wa kuipigia kura CCM. Madai yake ni kwamba CCM imewalea hao vijana, pili CCM imeleta amani na tatu kwa hali ilivyo CCM imeshashinda. Vijana wale walikuwa na hasira sana kwa maneno ya yule mama wakipinga madai yake hayo. Sikupenda kuingilia mjadala ule kabisa lakini mwishoni nilishindwa kuvumilia. Sikutaka kujadili madai mawili ya CCM kuleta amani na kuwalea na kuwasomesha watanzania kwa sababu naelewa jinsi tunavyochanganya haya mambo. Mtu unaposomeshwa kwa fedha za umma watu wanafikiri nini sijuhi. Umma ndio umekulipia, ni umma umekusomesha. Serikali ipo pale kama wakala tuu. Kama huu umma haukulipa kodi serikali haitakuwepo na ni wajibu wake kuutumikia umma wote. Ikishindwa kuutumikia kuna njia za kuiondoa hiyo serikali. La CCM kuleta amani nililijadili katika makala yangu ya utamaduni wa amani(makala hii ipo kwenye kona yangu ya makala ndani ya hii blogu.
Nilianza kubisha pale huyu mama aliposema CCM imeshashinda. Mimi kama mchumi nilifikiria jinsi gharama za uchaguzi zilivyo kubwa na jinsi ambavyo umasikini umetapakaa nchini. Watu bado wanakufa kwa kipindupindu Dar es Salaam! Kwa nini sasa tutumie mabilioni kupiga kura wakati mshindi ameshajulikana? Nilimtupia huyo mama swali hili. Kabla hajajibu kuna bwana mwingine akadakia. " Wewe kama si mjumbe wa NEC hukumchagua Kikwete, lakini sisi tunajua Kikwete ndiye rais, upigaji wa kura ni formality tuu". Nikamuliza kwa nini Tanzania tusianze haka kautaratibu kazuri ambapo kila chama kikishamteua mgombea wake tunaangalia tuu wingi wa washabiki wanaompokea na yule atakayepokelewa na watu wengi ndiye awe rais tuokoe mabilioni ya kupiga kura? Jamaa akasema hapana. Ni lazima kupiga kura. " Si unaona hata mataifa makubwa kama Marekani ni lazima wapige kura?"Aliendelea yule bwana. Nikamwambia kwa nini sisi kama watanzania tusibuni utaratibu wetu ambapo mshindi atajulikana tuu kwa kutazama idadi ya wapokeaji baada ya kutangazwa na chama chake? Baada ya hapo nchi nyingine zinaweza kuiga toka kwetu. Isitoshe tuna uzoefu. Tutamuomba tuu Spika aliyemaliza muda wake atusaidie kwa uzoefu wake wa pale bungeni anapouliza: wanaokubali waseme ndiyooooo..... wasiohafiki waseme siyooooo......- Waliofiki wameshinda na kipengele hiki kimepita. Uzoefu huu utakuwa chanzo kizuri cha kutusaidia tuokoe mabilioni ya fedha za uchaguzi na kusaidia angalau uchimbaji wa visima.

Kimya

Jamani nimekuwa kimya kwa muda mrefu sasa. Nilibanwa na shughuli kibao. Nilikwenda pia Nyumbani kuwaona ndugu jamaa na marafiki. Nyumbani sasa ni kampeni mtindo mmoja, watu kujieleza kwa wananchi, mlungula kutembezwa pale inapobidi, kila mgombea kumtoa mwenzake kasoro na mambo mengine ya namna hiyo. Barabara za Dar zimezidi kuwa finyu, magari ni mengi kuliko uwezo wa barabara. Barabara ya Shekilango iliyojengwa miaka michache iliyopita inatisha. Imebomoka yote. Sinza yote sasa inafanana. Zile barabara za vichochoroni hazina tofauti na barabara kuu ya Shekilango. Cha kusikitisha ni kwamba uwezo wa hii barabara ya Shekilango ni kupitisha magari yasiyozidi tani kumi kama sikosei. Wapi? yanapita mpaka ya tani 30. Ukiongezea na ukweli kwamba hakuna mifereji ya kupitisha maji basi mvua inavyonyesha inazoa kila kitu. Barabara hoi.

Thursday, August 18, 2005

Simba wazidi kuua watu

Kuna hii habari hapa inayoonyesha jinsi ambavyo idadi ya watu wanaouawa na simba imekuwa ikiongezeka Tanzania. Kuna maeneo mengine watu huamini kabisa kwamba hawa si simba wa kawaida. Huwa wanatumwa kula watu fulani fulani. Kwa maeneo kama hayo hawa huitwa simba watu.

Wednesday, August 17, 2005

Taifa Moja Nchi Mbili


Niliposoma takwimu za umiliki mali na mapato kati ya weupe na weusi Afrika ya Kusini nilishindwa kuamini. Katika takwimu hizo mwandishi alisema kwamba, kama ukiigawa Afrika ya Kusini kama nchi mbili tofauti; moja ikiwa ya wazungu ambao ni asilimia 14 na nyingine ikiwa ya weusi asilimia iliyobaki na ukitumia kigezo cha shirika la maendeleo la umoja wa mataifa –UNDP cha maendeleo ya watu (Human Development Index) ambapo nchi hupangwa kuanzia ya juu kabisa mpaka ya mwisho basi sura itakuwa hivi:
Taifa la wazungu asilimia 14 wanaomiliki asilimia 88 ya mali binafsi (Private Property) litashika namba ya 24 likiwa hatua moja chini ya Uhispania
Taifa la weusi ambao zaidi ya nusu wanaishi kwa kipato cha dola moja kwa siku, na asilimia 40 ya watoto wakiwa wamedumaa kwa utapiamlo litashika namba ya 123 likiwa juu ya Congo hatua moja. Hii inaonyesha ni jinsi gani pengo la walio nacho na wasio nacho lilivyo kubwa.
Nilianza kwa kusema sikuamini hizo takwimu kwa sababu ya picha ya mwanzo niliyokuwa nayo ya sehemu za katikati ya miji ambapo kuna barabara nzuri, nyumba nzuri, mahoteli makubwa, magari ya kifahari na vinginevyo. Sasa nimeamini. Nilishiriki katika utafiti wa maeneo mbalimbali ya Cape Town siku za karibuni tukiwa tunatafiti shule za Msingi. Acha utani. Maeneo wanayoishi weusi ndani ya hili jiji zuri yanatisha. Vijumba vingi ni vya mbao na mabati kote. Msongamano wa ajabu. Shule zao utaziona ziko hoi kabisa. Ukilinganisha na hizo za wazungu utazimia. Za wazungu zimesheneza acha utani. Kila kitu kipo darasani. Wanafunzi utaona tofauti zao za kuelewa mambo kabisa. Si kwamba weusi ni wajinga ila mazingira yanawafanya wasiweze kuwa kama wenzao. Tembea uone. Hapa ni mjini bado sijaenda huko vijijini nijionee.
Gazeti moja hapa siku za karibuni limetoa takwimu za kusikitisha. Inasemekana kwamba kwa sasa wanafunzi 3.6 milioni hawana viti vya kukalia na wengine milioni 4.2 hawana madawati yanayofaa kuandikia (hakuna mweupe hapa). Lakini ukiona maisha ya mijini huwezi kuamini kabisa. Kwa mtaji huu si kwamba kuna watu tofauti tuu katika nchi hii, bali pia hizi ni dunia mbili tofauti kabisa.

Ni nini maana ya kustaafu ?

Hili neno kustaafu linanipa shida sana. Nilidhani maana ya kustaafu ni kwamba uwezo wako wa kutoa mchango katika uzalishaji unakuwa umeanza kupungua na ndiyo maana ukifikia umri fulani ni lazima ustaafu. Kwa Tanzania umri wa kustaafu ni miaka 60. Umri huu uliongezwa miaka michache ya nyuma. Kabla ya hapo ilikuwa 55. Na umri huu hauwekwi tuu kwa maana ya kuwekwa kuna vigezo vinatumika na pengine utafiti unafanyika kabisa kutafuta umri muafaka wa kustaafu. Nadhani ukishastaafu sasa unatakiwa kufanya shughuli ambazo haziumizi sana kichwa na mwili wako, shughuli ambazo kwa kweli hazihitaji kukimbia kimbia. Ukimona mtu anastaafu halafu eti anachukua jembe kwenda kufungua shamba ujue huyo hawezi kuzalisha chochote. Utalima wakati wa uzeeni?

Kama ninachofikiria ni sahihi basi inaelekea bungeni ni mahali pa kupumzikia. Ni mahali ambapo hapahitajiki sana kutumia akili nyingi wala nguvu nyingi kwa sababu watu wengi wanaoijiingiza kwenye ubunge ni wazee waliokwishastaafu. Kwa maana nyingine mchango wao sehemu za kazi walipokuwa wakifanyia ulishapungua. Sasa unampeleka bungeni akawakilishe wananchi wa jimbo lake, akatunge sheria, akaishauri serikali nakadhalika. Hivi kutatokea chochote huko bungeni? Mimi nadhani hapa kuna kasoro kubwa mno. Kuna wale watakaosema kwamba busara za wazee zinatakiwa. Ndiyo zinatakiwa lakini si lazima iwe bungeni wana sehemu nyingine wanazoweza kupenyeza hizo busara. Pili nani alisema kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya busara na uzee? Kuna kuchanganya mambo hapa. Kuna tofauti kubwa kati ya busara na kuona mambo kwa miaka mingi. Labda Kiswahili changu ni kibovu nashindwa kuelewa kama kuona mambo kwa miaka mingi ndiyo busara. Kuna vijana wadogo wenye busara kuliko wazee wa miaka 80!. Na kama hujawahi kuwa na busara udogoni mwako huwezi kuwa nayo uzeeni hata utambike.

Mimi nadhani sasa wakati umefika kwamba ukishafikia umri wa kustaafu uache zile kazi nzito na zenye kuhitaji msuli hasa msuli wa akili. Labda tukubaliane kwamba kwenye siasa hakuna kazi za kutumia nguvu na akili nyingi ndio maana ukishastaafu unaweza kujimwaga na kuanza kwenda kukaa kwenye vikao Dodoma huku usingizi ukikuandama bila kutoa mchango wa maana katika miswada inayowasilishwa. Mawaziri wazee nao huu uwe mwisho wao. Labda pia iwe uwaziri nao ni kazi ya mteremko isiyohitaji nguvu na matumizi ya akili.

Thursday, August 04, 2005

Uajua hili?

Mnamo mwaka wa 1960, Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikuwa na hali nzuri kwa zaidi ya asilimia 50 ikilinganishwa na Taiwan, lakini kufikia mwaka 2000, kibao kilikuwa kimegeuka kabisa kwa Taiwan kuwa tajiri mara 17 ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Tukiweka tarakimu ili ieleweke kirahisi ni kwamba; mwaka 1960 kipato cha wastani kwa mwananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kilikuwa Dola za Marekani 2,180 wakati cha Taiwan kilikuwa Dola 1430, mwaka wa 2000 kipato cha kila Mtaiwani kilipanda na kufikia dola 18,700 wakati cha Mwanaafrika ya kati kilishuka na kufikia dola 1,120. Hali si tofauti sana ukilinganisha kwa mfano Malaysia na Ghana ambazo zote zilianza kwa kipato kinacholingana mwaka 1960 na zote zikiwa zinategemea sana kilimo, kadhalika unaweza ukalinganisha Nigeria na Indonesia zote zikiwa wazalishaji wa mafuta. Nitajaribu kuandika kwa lugha rahisi sbabu za maajabu haya. Kwa vyovyote unaweza kwa sasa ukachukulia tuu kwamba Afrika tuna kile ambacho tunatumia kujifariji na kuhalalisha uzembe "bahati mbaya" wakati wenzetu wana kile ambacho huitwa "bahati nzuri." Au tuite mkosi kwa Afrika? Sijuhi. Ngoja nitafute muda nichambue sababu ambazo zimekuwa zikitolewa kwa pengo hili.

Monday, August 01, 2005

Wanablogu wanafanya uandishi wa habari je ni waandishi wa habari?

Soma habari hii hapa uone umuhimu wa wanablogu

Blair na aondoke

Soma habari hii inayosema kwamba Tony Blair hafai tena kuendelea kuwa Waziri Mkuu kufuatia kitendo chake cha kusababisha mji wa London ushambuliwe kwa utitiri wa mabomu na sasa kutaka kunyang'anya wananchi baadhi ya haki zao na kuminya uhuru wao kutokana na sheria mpya za ugaidi.

Tutamkumbuka Daktari Garang

Daktari John Garang, makamu wa rais wa Sudan kwa wiki tatu tuu na kiongozi wa Sudan ya Kusini kwa miaka lukuki emefariki wakati ambapo dunia ilikuwa na matumain makubwa sana kwake hasa baada ya kusaini makubaliano ya amani na serikali ya Khartom. Soma habari hii hapa. Garang, Daktari mchumi aliyewahi kusoma Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam miaka ya nyuma na kupata shahada yake ya udaktari wa falsafa katika chuo hiki hapa alijitolea kupigania haki za wasudani kusini ambao walikuwa wakitengwa na mfumo wa utawala wa Khartom. Kifo chake kitakuwa pigo kubwa kabisa hasa ikitiliwa maanani mkataba wa amani wa hivi karibuni. Alale pema Daktari Garang.

Friday, July 22, 2005

Mambo ya blogu

Leo Ethan alitoa shule kuhusu "Community Blogging". Lilikuwa somo la nguvu sana. Washiriki walikuwa na furaha na wengi wamehamasika kuanzisha blogu zao na kuanzisha jamii yao ya mtandao wa blogu. Mimi nilizungumzia kidogo kuhusu blogu za Kiswahili; tunaandika nini, ni nani wanaandika nakadhalika. Wengi walifurahia jinsi ambavyo watanzania wanachipukia katika ulimwengu huu wa blogu na jinsi ambavyo wengi wetu tunavyojadili mambo yahusiyo nchi yetu, na ulimwengu kwa jumla kinyume na baadhi ya wanablogu wa nchi nyingine ambao huzungumzia mambo yao binafsi, familia na rafiki zao. Changamoto kubwa waliyotupa ni je ni nani anasoma tunayoaandika? Tutahakikishaje kwamba mawazo yetu yanasomwa na watu wengi zaidi? Hili ni jambo la msingi na inabidi wanablogu wote tubunge bongo kuhakikisha tunasomwa na watu wengi zaidi hasa wale ambao hawana "internet". Tujadiliane kwa hili kurahisha ufikishaji wa ujumbe kwa jamii. Lazima nikiri kwamba Ethan ni mtu muungwana, mpenda mijadala na mhamasishaji mzuri anayeweza kukufanya ukawa na blogu hata kama ulikuwa huna mpango wa kuwa nayo. Anaijua Tanzania kiasi pia, ameniambia ameshakuwa Dar mara kadhaa na ametembelea Zanzibar na Mikumi. Tuongeze bidii sauti zetu zitasikika.

Thursday, July 21, 2005

Nimekutana na Ethan Zuckerman

Leo jioni nimekutana na Ethan Zuckerman Tumejadili mambo kadhaa likiwepo jambo muhimu la wanablogu wa Tanzania. Jambo moja analosema ni kwamba watanzania wengi wenye kublogu ni waandishi na wamejikita sana kwenye mijadala ya kisiasa. Si kwamba ni vibaya. Jingine ni kwamba watu wengine mitaani hawako kwenye hii taaluma ya kutumia blogu. Hili la pili lina maelezo- miundombinu hafifu; si rahisi kwa watu wengi kutumia blogu kutoa mawazo yao kwa vile teknolojia bado ni ya hali ya chini. Jingine la msingi ni kwamba je ni watu wangapi wanaosoma mawazo yetu tunayoandika kwenye blogu? Kama wasomaji ni wachache ni namna gani basi tunahakikisha kwamba mawazo yetu yanafikia jamii kupitia magazeti na vyombo vingine? Hili ni jambo la kufikiria kabisa wanablogu wote watanzania. Mambo tunayoandika kwenye blogu yanawafikia wanajamii? Kwa mfano wanasiasa kweli wanasoma blogu? Kama hawasomi tutawafikishiaje ujumbe? Kaniuliza pia jambo lingine ambalo sikuwa na jibu lake. Hili waandishi mnaweza kulijibu. Ni kweli kwamba mnayoaandika kwenye blogu hamyaandiki kwenye vyombo vya habari mnavyofanyia kazi? Kwa kuwa siandiki magazetini sikuwa na jibu. Labda msaidie hapo.
Kesho atatoa mhadhara hapa chuoni nitahudhuria na kutoa mchango wangu kuhusu blogu za kiswahili.

Saturday, July 16, 2005

Ugaidi

Kwa nini hawa watu wanaoitwa magaidi watoke Misri, Saudi Arabia, Pakistan na nchi nyingine zenye uhusiano mzuri na Marekani na Uingereza? Kwa nini hawatoki nchi kama Iran au Iraq(kabla ya kuvamiwa)? Hili jambo limekuwa likinitatiza mno lakini naanza sasa kupata Mwanga. Huu urafiki wa baadhi ya nchi za kiarabu na nchi za magharibi hauungwi mkono na watu, ni urafiki wa viongozi hivyo wanajaribu kuonyesha hisia zao kwa njia hizi ambazo nchi za magharibi zinaita ugaidi. Lakini kuvamia Iraq na kuua hovyo si ugaid hata kidogo, ni ukombozi. Kabla ya kuvamiwa Iraq kulikuwa hakuna kitu kama watoa maisha mhanga. Naam, sasa wamezalishwa wa kutosha. Kulikuwa hakuna ushahidi wowote wa Alkaida na Iraq. Naam sasa wana tawi kabisa. Kwa vile wanataka Iraq iwe na uhusiano na nchi za magharibi sasa wananchi hawataki wanaonyesha kwa vitendo kama vya kujitolea mhanga, hali ambayo haikuwepo siku za nyuma.
Kwa wale wasikilizaji wa BBC nadhani mmesikai mjadala alioendesha Tido Mhando katika kipindi cha wiki hii- Jumamosi, tarehe 16/07/2005, mmoja wa washiriki wa mjadala ameongea jambo la msingi sana. Kwamba ni waafrika wangapi wanakufa kwa kuchinjwa, wanakufaa kwa njaa, magonjwa yanayotibika nakadhalika kila leo? Hakuna tofauti kati ya mweupe na mweusi katika vifo. Lakini wakifa weupe nakuambia ni kama wao wana haki zaidi. Hawastahili kufa. Mabomu ya London yaliyoua watu 54 hadi sasa yameonyesha hili. Viongozi mbalimbali wanatia saini vitabu vya maombolezo. Inatakiwa sasa kila asubuhi baadhi ya viongozi wakiamka asubuhi jambo la kwanza liwe ni kutia saini vitabu vya maombolezo kwa makumi ya watu wao waliohujumiwa maisha yao kwa Malaria, Kipindupindu, Ajali nakadhalika. Wasisahau pia kutia saini vitabu vya maombolezo kwa wananchi wa Iraq wanaouwa kila siku bila hatia.

Wednesday, July 13, 2005

Wanahabari ni muhimu kusoma hii

Hii tovuti ya John Pilger ni nzuri sana hasa kwa wana habari. Ipitie hapa halafu soma hii habari hapa

Unmfahamu George Galloway?

Huyu ni mwakilishi katika "House of Commons" Uingereza, anawakilisha eneo ambalo watu wake wengi walikufa katika milipuko iliyogharimu maisha ya waingereza wasiopungua 50 karibuni. Huyu bwana ameamua kusema ukweli. Anasema haya ni matokeo ya chuki ambayo imeongezeka dhidi ya Uingereza na Marekani kutokana na sera zao mbovu hasa huko Iraq, Afrighanistan, Mambo yanayotokea Guantanamo bay, yaliyotokea katika gereza la Abu Ghraib huko Iraq na mengineyo. Pamoja na kulaani hiki kitendo cha kulipuliwa waingereza kwa nguvu zote, bado anahoji mantiki ya kutoona wale wanaouwawa Iraq kila siku kama binadamu wengine. Anasema kuna watu wanaofikiri kwamba damu ya Wairaq waliouwawa Falujah wakati mji unateketezwa na wanajeshi wa ushirika ikiwemo Uingereza haina thamani kama waingereza waliouwa kwenye mashambulizi hayo. Tafadhali soma mawazo yake kama yalivyonukuliwa katika taarifa rasmi ya bunge (Hansard) Hapa

Tuesday, July 12, 2005

Kuna Demokrasia IMF na World Bank?

Kuna wataalam ambao wanahoji uhalali wa nchi kama Marekani kuwa na maamuzi makubwa katika vyombo vya fedha duniani yaani Benki ya Duniaa na Shirika la fedha ulimwenguni. Wanahoji pia uhalali wa nchi nyingine hasa changa kuwakilishwa na waziri wa fedha na gavana wa benki kuu tuu katika kutoa maamuzi makubwa ya nchi yao. Kwa wenye hoja kwamba nchi kubwa zina kura ya turufu kwa sababu ya mchango mkubwa, anatoa mfano wa Bill Gates kwamba yeye basi apatiwe kura kwa mfano laki moja kwa vile kipato chake kinaweza kuwa mara laki moja ya kipato cha mmarekani wa kawaida. Nisikumalizie uhondo, msome mwenyewe HAPA

Saturday, July 09, 2005

Mapadre na Familia

Soma habari hii ya mapadre wa Kanisa katoliki huko Marekani

Friday, July 08, 2005

Matatizo yameisha?

Mkutano wa wanyakua mali za waafrika umeisha. Nasikia sasa wamekubaliana kuongeza msaada kufikia Dola Bilioni Hamsini ($50). Kweli waafrika tuna matatizo mengi kweli. Baadhi yetu tulikuwa haturajii maajabu japo kuna watakaofikiri wamelamba dume. Hebu fikiria dola bilioni 50 kwa bara zima. Bara lina nchi 53 hivi zenye matatizo mengi na tofauti lakini nyingi ya nchi, matatizo yanafanana. Tukichukulia ukweli kwamba kuna nchi ambazo zina ahueni kama vile Mauritius, Nchi za Afrika ya kaskazini, Botswana, Afrika ya kusini, Namibia na nyingine chache, nchi nyingine ni hoi. Hata hizi si kwamba umasikini si wa kutisha, ni takwimu tuu ambazo zinaonyesha kwamba wana ahueni lakini kuna watu hoi ajabu na wengi. Sasa tukiziondoa hizo tuchukulie tunabaki na nchi kama 25 ambazo ni hoi zinazohitaji msaada huo. Ina maana kwamba kwa wastani kila nchi itapata Dola bilioni 2 hivi. Na haziji mara moja. Sidhani kama kuna maajabu yatakayotokea. Pili, huu utegemezi hautatutoa kwenye mtaro tuliopo.
Ninasikia huko Kenya watoto wamemkabidhi Balozi wa Uingereza sahihi kama 400,000 wakitaka nchi za kibepari zishughulikie matatizo ya watoto wa Afrika. Wanasema wanataka sahihi nyingine toka Uganda, Ethiopia na Tanzania ili zifike milioni moja. Watoto nao wameshakataa tamaa kwamba matatizo yao hayawezi kutatuliwa na nchi zao wanataka mabepari wayatatue. Sijuhi tunajengea watoto wetu kasumba gani. Kasumba ya kukosa imani na Serikali yao na kasumba ya utegemezi. Unafikiri hao watoto wanaweza kujua katika kukua kwao kwamba inawezekana kufanya chochote bila wazungu? Si ajabu watoto walivyowasilisha sahihi hizo kulikuwa na viongozi wa serikali, hata kama hawakuwepo huenda wamefurahishwa na jambo kama hilo, kwa sababu wanadhani mabepari wanaweza kuwasikiliza watoto na kupewa misaada ili yaingie tumboni mwao. Aibu hii!!!

Wednesday, July 06, 2005

Makala ya Misaada

Nimeandika mawazo yangu kuhusu misaada na mkutano wa G8. Unaweza kusoma hapa

Monday, July 04, 2005

Gadaffi aonya viongozi wenzake kuacha kuomba

Soma habari hii uone jinsi kiongozi wa Libya anavyowaonya viongozi wa Afrika kuacha kuomba kwa nchi tajiri. Nadhani waliozoea kutembeza bakuli wanamuona kama mwendawazimu fulani hivi.

Huenda Afrika ikagawanwa

Nahisi huo Mkutano wa G8 utakuja na mkakati wa kugawana maeneo Afrika. Kila mshirika atapewa vipande ambavyo ataambiwa avipe kipaumbele katika kutoa misaada. Kila nchi inaweza kukabidhiwa eneo Afrika kutokana na umahiri katika sekta fulani. Marekani nahisi itakuwa ni Equtorial Guinea, Cape Vedre, Chad sijuhi na ipi. Na nyingine zitachagua maeneo kutokana na uwezo wa kampuni zake kugecha rasilimali za Afrika. Ikitokea hivyo usishangae. Ndiyo Berlin Nyingine hiyo!!

Sunday, July 03, 2005

Angalia hii habari ya huyu Balozi wa Iraq

Habari hii hapa inaonyesha jinsi huyu balozi wa Iraq katika Umoja wa Mataifa alivyo mbinafsi. Analalamika kuuwa kwa binamu yake ambaye anadai hakuwa na hatia. Hivi ni maelfu mangapi ya wairaq wasio na hatia wanaouwa na jeshi la Marekani? Ameumwa sana na binamu yake anasahau kila mwiraq ambaye mtoto, mzazi au ndugu yeyote aliyeuwa ana machungu kama yake ila hawana pa kulalamikia kama yeye. Yeye kama mwakilishi ingebidi aongelee mfumo mzima wa utendaji wa jeshi la wavamizi wa marekani wanavyoua watu hovyo. Sasa kaona binamu yake ni binadamu zaidi kuliko wengine!

Saturday, July 02, 2005

Yanayotokea Malawi

Ukifuatilia mambo yanoyotokea nchi jirani ya Malawi tangu alipochaguliwa Bingu wa Muthalika utagundua mengi. Jambo la kwanza utakalogundua ni lile onyo alilowahi kutoa Hayati Mwalimu Nyerere: je unapotumia fedha lukuki kutaka urais utazilipaje? Kuna kiwanda cha kutengeneza pesa ikulu? Ndicho alichofanya Bakili Muluzi rais mstaafu. Alitafuta mamilioni ya Kwacha za Malawi kumnadi wa Muthalika. Baada ya kuchaguliwa akatakiwa aanze kuchota pesa kulipa madeni. Wacha utani, mchumi kakataa kata kata. Sasa wakaanza kumzushia visa wanataka sasa kumtosa kabisa. Wabunge wa UDF chama kilichompa urais kinataka sasa kulitumia bunge kumwadabisha. Malumbano yakawa makali mpaka Spika kapata kiharusi na sasa Marehemu.
Lingine ni kwamba huyu rais Muthalika ataandika historia. Nadhani atakuwa miongoni mwa watu wachache wenye uthubutu duniani. Uthubutu wa kukihama chama kilichompa madaraka na kuunda cha kwake. Si mchezo inahitaji roho ngumu hasa. Wamalawi wameshindwa cha kumfanyia kwa sababu katiba iko kimya iwapo rais ataamua kukihama chama. Nani angefikiria kwamba kuna mtu angethubutu kufanya hivyo? Huyu bwana atasaidia sasa nchi nyingi kuangalia katiba zao upya. Kuna jamaa wanaosema kwamba huyu bwana kafanya kitu ambacho hakijawahi kutokea nchi yoyote. Kama ni kweli basi yeye ni mwanzilishi. Kila kitu huwa na mwanzo kwani ni lazima ufanye mambo ambayo yameshafanyika tuu? Ni lazima kuwe na pa kuanzia. Nadhani atakumbukwa kwa hilo.
Mwisho, ni lazima ugundue kwamba unavyogombana na mtu na kusuluhishana ni wachache sana ambao husamehe kabisa. Muluzi na wa Muthalika walikuwa maadui wakubwa siku za nyuma. Inadaiwa kwamba ni Muluzi aliyemfanyia fitna wa Muthalika kuondolewa katika COMESA. Baadaye wakasuluhishana na Muluzi kumshika mkono kutaka wamalawi wamchague. Nadhani jamaa alikuwa akingojea pa kulipizia kisasi. Na sasa anafanyiza kweli!! Kuna somo tunaloweza kujifunza?

Thursday, June 30, 2005

Kiswahili lugha yetu

Kuna makala mbili za Padre Karugendo zilizopo kwenye blogu ya Ndesanjo kuhusu Kiswahili. Moja ya jambo aliloonya ni kwamba kama Tanzania italala na kufikiri kwamba ni bingwa wa kiswahili, basi kuna siku utasikia wakenya, waganda, wakongo waafrika ya kusini wakiwa ndio waalimu wakubwa wa kiswahili na wakawa wanatengeneza fedha kupitia lugha ambayo Tanzania inaweza kabisa kujisifu ndio gwiji wake. Mambo kama haya yameshatokea duniani si mageni. Wareno katika historia walikuwa wa mwanzo kabisa kufanya tafiti na kugundua mambo mengi lakini wakalala wakaanza kunywa mvinyo wakapitwa na nchi nyingine za ulaya. Sasa hivi Ureno ni kati ya nchi masikini barani ulaya. Mfano mwingine ni wa Malasia na Ghana katika kilimo cha Mawese, nchi hizi mbili zote zilipata uhuru mwaka 1957, Ghana ilikuwa mzalishaji mkuu wa mawese ambayo ni malighafi muhimu sana, Wamalei walikuwa wanakwenda Ghana kujifunza kilimo hicho, waghana walikuwa wakienda Malasia kuwafundisha namna ya uzalishaji wa zao hilo. Angalia leo tofauti iliyopo kati ya Malasia na Ghana. Malasia sasa hivi ni mzalishaji mkuu wa Mawese duniani, wakitumia taaluma ya kisasa. Ghana sasa wanajifunza toka Malasia. Mifano ni mingi. Tunajifunza?

Tuna matatizo gani?

Je unajua kwamba shirika la ndege la Afrika ya Kusini SAA ambalo lilichukua ATC linamilikiwa na Serikali? Mbona wao wanaweza mpaka wananunua mali za shirika la serikali nyingine? Yaani tunatoa mali yetu inayomilikiwa na serikali yetu kwa serikali ya nchi nyingine. Hamu sina.

Mambo ya UKIMWI yapamba moto

Jamani haya mambo ya UKIMWI yanakuwa sasa ni siasa. Kama mtakumbuka siku za nyuma niliandika jinsi Daktari anayetangaza matumizi ya vitamini kama njia ya kusaidi kupunguza madhara ya UKIMWI anavyobanwa. Nimeandika pia kwenya makala yangu ndefu iliyopo ndani ya blogu sasa. Basi siku za Karibuni Waziri wa Afya wa Afrika ya Kusini, Manto Tshabalala- Msimang alionana na huyo Dr. Rath (bingwa wa vitamini) na anaelekea anakubaliana na hoja kwamba vitamini kiasi fulani zina manufaa katika kumsaidia mhathirika. Baada ya hapo akatoa tamko kwamba wananchi wawe na uchaguzi wa dawa zilizopo, wale wanaoweza kupata ARVs waendelee nazo wale wa vitamini na dawa asilia waachwe wachague kwa sababu asilimia 80% ya wagonjwa wanaofika hospitali za serikali huwa wanatembelea waganga wa asili kwanza. Wabunge wa chama cha wazungu cha DA wamekuja juu, sasa wanataka kumshitaki katika baraza la maadili la watoa huduma za afya kwa kuwaambia wanachi wanaweza kuchagua dawa ambazo hazijathibitishwa kutibu kitaalam. Kuna mvutano usio wa kawaida kati ya watetea kampuni za dawa za magharibi na watetezi wa dawa asilia na vitamini. Huu ukasuku wa waafrika kufikiri kila kitu lazima kipitishwe na wazungu utatumaliza. Huyu Waziri ni ngangari sana na si mhumini mzuri sana wa nadharia za UKIMWI zilizoenezwa na nchi za magharibi ambazo kwanza hazina uthibitisho wa kitaalam. Rais Thabo Mbeki pia alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakihoji nadharia ya HIV-UKIMWI. Ukienda kwenye tovuti hii utakumbana na picha yake pamoja na mambo mengi yahusuyo UKIMWI

Tuesday, June 28, 2005

Makala mbili mpya

Nimeandika makala mbili mpya. Moja kuhusu Shirikisho la Afrika Mashariki na nyingine kuhusu utata juu ya UKIMWI. Zisome hapa na hapa. Makala nyingine mpya kuhusu misaada ya nje nitaibandika karibuni.

PSRC ibinafishwe

Hili dude linaloitwa PSRC limekuwa likilalamikiwa kweli kweli. Limekuwa likifanya mambo ambayo yanalalamikiwa mara kwa mara kama kuuza mashirika kwa bei poa, harufu za rushwa na mikataba ya ajabu ajabu. Hii tume iliteuliwa kurekebisha mashirika ya umma sasa inabidi nayo irekebishwe. Inaweza kubinafsishwa. Kubinafisha taasisi inayoshughulikia ubinafsishaji kama PSRC ni aina mojawapo ya ubinafsishaji pia. Unatangaza tenda halafu unapata kampuni binafsi itakayofanya ubinafsishaji, serikali inabakia na kazi ile ile ya kuweka kanuni na kusimamia sera na kuhakikisha ubinafsishaji unafanyika kwa manufaa ya wananchi. Hii ni njia mojawapo ya kuirekebisha PSRC.

Mchakato wa kuwapata wagombea urais

Nilidhani hii hoja sasa basi, lakini kuna watu wameniuliza naonaje mchakato mzima wa vyama vyote vya siasa kuwapata wagombea urais. Mimi sina ugomvi na mchakato mzima unaotumika najua hizo ni taratibu ambazo vyama vimejiwekea na kukubalika. Ugomvi wangu ni watu wanaoshiriki katika zoezi zima la kuwateua wagombea. Nina maana wajumbe wa Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu wa vyama. Je wajumbe hawa wanaofanya maamuzi mazito namna hii wana uelewa gani wa mambo. Hivi kwa mfano ni wangapi wana uelewa wa rais anayetakiwa katika kipindi hiki cha mageuzi mazito na ushenzi unaofanywa na mataifa makubwa kwa nchi changa? Ni wajumbe wangapi wanaoelewa hali halisi au ni wafuata mkumbo tuu? Hivi wajumbe hupatikana kwa vigezo gani? Ni ualiwatani wa vijiweni, uimbaji wa kutukuza vyama au kupandisha bendera za vyama kwenye magenge au biashara? Hawa wajumbe wanafanya maamuzi makubwa sana. Wanajadili taarifa za utekelezaji wa kazi za serikali, wanatoa maagizo kwa serikali, wanateua wagombea urais nakadhalika. Hivyo wajumbe hawa wanatakiwa wawe waelewa kweli kweli si ualiwatani. Ni lazima vigezo viwekwe kwa wanaogombea nafasi katika ngazi hizi za halmashauri kuu na mkutano mkuu kwa vyama vyote la sivyo tutaona maajabu.

Mambo ya Yakobo

Sikutaka kuandika chochote kuhusu sakata la Yakobo Zuma, Makamu wa zamani wa Rais wa Afrika ya Kusini kutimuliwa kwa madai ya rushwa, lakini wapi, wachokozi wametaka niseme lolote. Basi ninasema. Miezi mitatu iliyopita nilijikuta nabishana na jamaa wawili toka Zambia. Hawa jamaa nilisafiri nao kwa masaa kama 18 hivi, tuliongea mambo mengi likiwepo sakata la Rushwa lililokuwa likimkabili Yakobo. Jamaa mmoja kati ya hawa anadai ni mzoefu wa mambo ya Afrika ya Kusini akaniambia; unajua sakata la Yakobo na rushwa si la kweli? Ni uzushi mtupu, ni mambo ya siasa tuu. Nikamuuliza kivipi? Akaniambia ni mambo ya ukabila, Yakobo ni Mzulu, na watu wa kabila la Waxhosa ambalo wanatokea pia Mandela na Mbeki hawataki mzulu awe rais kabisa kwa hivyo wameamua kumzushia kashfa ili wamtose kwa kuwa umakamu wa rais ungempa nafasi nzuri ya kuwa rais. Akaendelea, hata wazungu hawataki wazulu kwa sababu wazulu si mchezo, ni watu wa shari na walipiza kisasi. Kwa hivyo Yakobo amekumbana na janga kama hilo. Uzulu umemponza. Nikamuuliza huyu jamaa, sasa kwa nini wamwache au wampe vyeo mpaka umakamu wa rais? Jamaa haishiwi na hoja. Akaniweka chini na kuniambia: unajua walimweka pale kukimaliza chama cha Inkatha Freedom cha Mongusuthu Buthelezi ambacho kilikuwa na nguvu kubwa miongoni mwa wazulu na sasa si unaona Inkatha hoi? Kamaliza kazi na sasa anatoswa.

Kwa kweli kama si mambo ya aibu waliyokumbwa nayo kina Chiluba basi huyu bwana angeniaminisha kwa sababu mimi kuna jambo moja nashindwa na nitashindwa kuelewa mpaka kesho. Hivi kwa nini kiongozi wa ngazi za juu kama rais, makamu wa rais au waziri mkuu wakumbwe na kashfa za kijinga za wizi au Rushwa? Ukiona kiongozi anakumbwa na kashfa kama hii basi ni mjinga. Hawa watu wanatunzwa kwa kodi za wananchi wakiwa madarakani, wakistaafu wanaendelea kutunzwa mpaka wafe. Si wao tuu mpaka na wake zao hata kama unao wawili watakutunzia mpaka wafe. Sasa kwa nini unaiba tena? Mimi narudia tena, binadamu ni kiumbe wa ajabu kuliko kingine chochote.

Sasa haya ya Yakobo tutangoja tuone kama kweli ni safi au ni mla rushwa tuu baada ya yeye mwenyewe kujitetetea mbele ya mahakama. Hata yeye mwenyewe amesema ni mambo ya siasa na si mla rushwa, tuongoje tuone kama tutamweka kwenye kundi la viongozi wajinga wa Afrika au la. Kutakuwa na kasheshe, huko kwao Durban washabiki wake wamekuja juu vibaya sana, kila waziri mkuu wa jimbo la Kwazulu Natal anapotaka kuwahutubia wananchi, washabiki wa Yakobo wanavuruga mkutano. Hawaambiwi chochote wakaelewa.

Imetokea Karibuni

Dunia hii ina vituko nakuambia. Nilipoambiwa habari hii ya kusikitisha na kufurahisha niligundua binadamu wana mambo si kidogo. Ilikuwa hivi: jamaa mmoja mweupe nina maana mzungu, alikuwa akisafiri toka mji mmoja uitwao Gobabis kuelekea Windhoek huko Namibia akifuatana na mbwa wake na mfanyakazi wa kiume. Kwa vile alikuwa na gari aina ya pick-up, aliamua kukaa na mbwa wake mbele na jamaa akakaa nyuma huku akitwangwa na upepo usio na mfano. Kuepuka kuchapwa sana na upepo ilibidi atizame upande gari linakotokea , kwa wale wazoefu wa kusafiri kwenye magari ya wazi wanajua hii ndiyo njia ya kupunguza kuchapwa na upepo. Jamaa akachochea gari lake, kabla ya kufika walipokuwa wakienda wakapata ajali mbaya, yule mzungu akafa palepale, mfanyakazi na mbwa wakapata majeraha madogo sana. Polisi walipofika kusaidia na kupima ajali wakawa wanamuuliza yule mfanyakazi: hebu tuambie ajali ilivyotokea, jamaa nadhani hakuwa na subira wala hakupepesa macho akawaambia polisi muulize huyo- huku akimnyoshea kidole mbwa. Akaendelea: mimi nilikuwa nikiangalia gari linapotokea kwa sababu ya upepo, marehemu na huyu mbwa ndio waliokuwa wakiangalia gari linapoelekea hivyo walijua kilichotokea. Kwa hivyo mbwa anaweza kuwaelezea vizuri zaidi. Nakuambia polisi hawakuwa na na hamu hata kidogo. Naambiwa mbwa pia alikuwa akilalama kumona tajiri yake akiwa amelala usingizi wa moja kwa moja.

Saturday, June 25, 2005

Kodi na mishahara ya Tanzania

Nashauri kila mtu apitie lile jedwali la mapendekezo ya Mramba katika kubadilisha viwango vya kodi ya mapato ya ajira. Kuna mambo mengi sana unayoweza kucheza nayo kwenye lile jedwali. Kwanza utagundua wafanyakazi wa Tanzania wanalipa kodi kubwa si mchezo. Angalia kwa mfano mtu mwenye mshahara wa shilingi 100,000 kwa mwezi, ina maana kwa miezi 12 atapata shilingi 1,200,00. Mtu huyu atalipa asilimia 18.5 ya mshahara huo kwa mwaka kama kodi. Ina maana atalipa kodi ya shilingi 222,000 kwa mwaka. Kodi yake ya mwaka inamlipa mfanyakazi wa kima cha chini kwa miezi inayokaribia mitatu. Hiki ni kiasi kikubwa cha pesa. Nadhani viwango vya kodi zetu kwa ujumla ni vikubwa kweli. Nadhani wafanyabiashara wadogo na wale wa kati wana nafuu kubwa kwa sababu viwango vyao vya kodi kutegemeana na mauzo kwa mwaka ni vidogo kulinganisha na hivi vya wafanyakazi.

Jambo la pili unaloweza kuona ni kwamba wale wafanyakazi wanaolipwa mshahara ambao tofauti yake na kima kinachotozwa kodi cha shilingi 80,000 ni ndogo wataumia sana. Mfano mfanyakazi anayepokea 90,000 akilipa kodi ya asilimia 18.5 atabakiwa na shilingi 73,500 pungufu ya kile cha kima cha chini, anayepokea 100,000 atapata shilingi 81,500 akishalipa asilimia 18.5 tofauti yake na kile kiwango kinachotozwa kodi ni shilingi 1,500 kwa mwezi. Haya mahesabu si mchezo.

Jambo jingine ninalotaka kuzungumzia ni jinsi Serikali inavyopoteza mamilioni kwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara midogo. Kwa hali ya kawaida, waajiri wengine, wawekezaji, mashirika ya kimataifa na kadhalika yanapoajiri yanaangalia mishahara inayolipwa na mwajiri mkubwa. Kwa maana ya Tanzania, Serikali ndiyo mwajiri mkubwa. Sasa kama mwajiri mkubwa analipa kiduchu na wao watalipa mishahara ambayo si mikubwa sana, hapa serikali inakosa mapato ambayo ingeyapata kupitia hawa waajiri wengine kama wangelipa mishahara mikubwa zaidi. Hili ni suala la kisera linalotakiwa maamuzi. Sikatai kwamba mishahara pia hulipwa kutokana na tija. Kinachotakiwa ni Serikali kuangalia hili upya na kufanya mahesabu ambayo yataleta uwiano mzuri na kuongeza pato kupitia kodi zitokanazo na ajira.

Kuna haya majigambo kwamba Serikali imekuwa ikiongeza mishahara kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita kutoka shilingi 17,500 kwa kima cha chini mwaka 1995 hadi shilingi 60,000 mwaka 2004 kwa mwezi. Hapa ukiangalia tofauti utadhani ni kitu kikubwa kweli kweli na mwanasiasa anatamka tarakimu hizi akiwa ameuma meno yake kwa msisitizo. Tuambie hizo 17,500 zilikuwa zinanunua bidhaa na huduma kiasi gani mwaka 1995 na kwa sasa hizo 60,000 zinanunua kiasi gani? Huo ndio ungekuwa unyambulifu wenye akili lakini tarakimu tuu hazina maana. Kwenye uchumi tunachoangalia ni mapato yananunua nini kwa kipindi kati ya sasa na baada ya muda fulani.

Kitabu cha kusoma

Jamani kuna hiki kitabu nilichokisoma mara mbili kinaitwa Secret Terrorists kilichoandikwa na Bill Hughes. Jamaa huyu amendika mengi sana yote yakihusu jinsi ambavyo Kanisa Katoliki kwa muda mrefu limekuwa likihujumu taifa la Marekani na Dunia kwa ujumla. Baadhi ya madai haya ni Pamoja na Njama za kumuua rais Andrew Jackson aliyechaguliwa kuwa rais mwaka 1828 jaribio lililoshindikana; kuuwa kwa rais William Hendry Harrison aliyechaguliwa kuwa rais mwaka 1841 rais Zachary Taylor aliyechaguliwa mwaka 1848, jaribio lingine la kumuua Rais James Buchanan kwa sumu lililoshindikana; kuuwa rais Abraham Lincoln na John F.Kennedy. Chanzo cha mauaji na majaribio haya kwa mujibu wa mwandishi ni kutokana na marais hawa kupingana na matakwa ya wanaojulikana kama Jesuits chini ya Kanisa Katoliki.

Madai mengine ya nguvu ni pamoja na kuzamishwa kwa meli ya TITANIC mwaka 1912 kwa lengo la kuwaua matajiri watatu maarufu duniani wakati huo Benjamin Guggenheim, Isador Strauss na John Jacob Astro walioonekana tishio katika kuzuia kuanzishwa benki kuu ya Marekani inayomilikiwa na matajiri wachache wa Jesuits.

Vita ya kwanza na pili ya Dunia pia anasema ilianzishwa kwa mkono wa kanisa hilo. Hitler na Mussolini inasemekana walikuwa wakiungwa mkono na Kanisa Katoliki. Matokeo mengine yanayozungumziwa kwenye kitabu hicho ni pamoja na maovu yaliyofanywa na Slobodan Milosevic katika kuwamaliza Wakristo wa Madhehebu ya Kiorthodox huko Serbia miaka ya 1990. Mwandishi anadai muuji si Milosevic bali ni Papa na Kanisa Katoliki hata kumshitaki bwana Milosevic ni uonevu tuu.

Jamaa anaendelea kutupasha kwamba matokeo ya Septemba 11 ni mtiririko huo huo hakuna cha Osama wala nini kama hakukuwa na Osama mwaka huo wa 2001 basi angeundwa Osama mwingine ili kulinda maovu ya hao majamaa.

Jamani yote tisa lililoniacha hoi ni hili dai kwamba: Vatican ilianzisha Uislamu kwa lengo la kuwaangamiza wakristo na wayahudi, kulinda wakatoliki na kuiteka Jerusalemu ili waikabidhi kwa Papa. Katika miaka michache ya mwanzo ya uislamu, waislamu walifanya hivyo lakini ilipofikia hatua ya majenerali wa kiislamu kuisalimisha Jerusalemu kwa papa waligundua kwamba walikuwa na uwezo wakakataa kuisalimisha. Hata vita ya ugaidi inayoendelea leo ni moja ya njia za kuwalipiza waislamu kwa kukataa wakati huo kuikabidhi Jerusalemu kwa Papa. Kwa hiyo vita ya mashariki ya kati itaendelea, watakufa watu kwa maelfu hadi hapo mpatanishi atakapotafutwa na mpatanishi huyo atakuwa papa na kwa vile vyombo vya habari vilivyothibiwa vitashawishi ulimwengu kwamba anayeweza kutatua tatizo la mashariki ya kati ni papa pekee, atafanya hivyo na ataiteka Jerusalem. Hapo misheni itakuwa imefanikiwa kwa sababu lengo limekuwa wakati wote huu ni kuitwaa Jerusalemu.

Nimedonoa tuu kijitabu hiki nakushauri ukisome. Kisome kwa makini nahisi kimeandikwa na msabato. Kwa wale wanaowaelewa wasabato haitakuwa ngumu kuelewa kwa nini ninasema hivyo. Binafsi nina maswali lukuki ya kumuuliza huyu mwandisi najaribu kuwasiliana naye ili anijibu maswali yangu. Nitawaeleza maendeleo ya mjadala wangu na huyu bwana. Mwenye habari ya ziada juu ya madai haya yaweke adharani watu wayaone na wayajadili.

Majadiliano ya Doha

Jumapili ya tarehe 12/6/2005, kulikuwa na majadiliano mazuri yaliyoendeshwa na mwandishi maarufu wa BBC Tim Sebastian huko Doha Qatar. Majadiliano yenyewe yalihusu kama Wanawake wa nchi za kiarabu wawe na usawa kamili. Kulikuwa na pande mbili zilizokuwa zikijadili pamoja na wachangiaji wengine wengi, upande mmoja ukiwa na waunga hoja mkono ukiwakilishwa na mwanamama mmoja ambaye ni mbunge wa kwanza mwanamke nchini Jordan na Bwana mwingine ambaye ni mtangazaji toka Kuwait. Wachangiaji wa upande huu walielekea kuifahamu barabara jamii ya kiarabu. Walionyesha jinsi watu wengi wanavyochanganya mila za asili za uhafidhina za kiarabu na Uislamu. Nilichojifunza toka kwao ni kwamba wanawawake wanavyochukuliwa katika nchi nyingi za kiarabu si ndivyo uislamu unavyotaka bali ni mila za kale za kiarabu.

Upande wa wa pili wa hoja uliwakilishwa pia na mwanamama na bwana mwingine ambao wote wamekulia nchi za magharibi. Hawa pamoja na kuonekana kutoilewa vema jamii kutokana na kuishi nje walionya kuhusu nchi za kiarabu kuiga demokrasia ya magharibi kichwa kichwa. Lingine lililojitokeza ni uelewa kuhusu usawa kwa wanawake. Watu wengine bado wanafikiria usawa ni hali ya mwanamke kubadilika na kuwa kama mwanaume. Ukizungumzia usawa wanasema basi wanawake wakiwa sawa na wanaume ule uanawake wao utapotea, wanafikiri usawa ni mwanamke sasa kuwa mwanaume. Kinachozungumziwa ni nafasi. Mwanamke apatiwe nafasi kama anazopatiwa mwanaume na tuone kama hataweza. Ni lazima tujue kuna tofauti za maumbile ambalo ni suala la kibiolojia tusiloweza kushindana nalo. Mjadala uliitimishwa kwa kura waliounga mkono hoja walipata asilimia 86 na waliopinga walipata asilimia 14.

Hoja ya kutoiga kila kitu toka magharibi ilinifurahisha mno kwa sababu hata kwetu sisi weusi na watanzania kipekee ni mabingwa wa kuiga mara nyingi mambo ya hovyo zaidi kuliko ya msingi. Wakati mmoja Ndesanjo aliandika makala ambapo aliuliza kwa nini kwa mfano tusiige mambo mazuri toka kwa wazungu kwa mfano kuheshimu muda na kutunza mazingira kuliko kuiga mambo ya hovyo kabisa? Huko tuendako kwa kasi hii ya kuiga ni lazima ukiwa na watoto wa jinsia yoyote ile utenge pesa za kusuka nywele na kununua hereni kwa wanao.

Monday, June 20, 2005

Jamani nani anatoa mgao wa saluti?

Nilitaka kukaa kimya bila kutoa maoni yangu kuhusu baadhi ya wabunge kutaka wapigiwe saluti. Mimi nauliza ni nani mtoa mgao wa saluti? Ni waziri? ni nani? Kwa nini asiwagawie tuu. Nadhani wabunge wamegundua kitu kwenye saluti. Ni lazima wakishapigiwa saluti wananchi wa majimbo yao watapata hali nzuri ya maisha, ni lazima uzalishaji wa chakula utaongezeka, ni lazima masoko ya bidhaa zao yatapatikana, ni lazima umasikini Tanzania utapungua kwa kasi ya ajabu. Nina mategemeo kwamba wakipewa mgao wa saluti malengo yanayoitwa ya milenia yanaweza yafikiwe kabla ya muda wake tukaweka historia. Sidhani kama mtu anaweza kudai saluti kama haimuongezei mwananchi hali nzuri ya maisha. Naomba mtoa mgao afikirie hili. Baada ya kufikiria kuwapa wabunge, na ili kasi ya maendeleo iongezeke kwa kishindo, basi na atoe mgao kwa madiwani wa kata zote nao wapewe saluti zao hawa wako karibu na wananchi zaidi kuliko wabunge. Baada ya hapo viongozi wa mitaa, vitongoji na vijiji wapewe mgao wao, asisahau balozi wa nyumba kumikumi. Nadhani hawa waote wakipewa mgao wa saluti basi mwaka kesho mwezi kama huu tutakuwa tumefikisha malengo ya milenia.
Ili kasi ya maendeleo iongezeke kwa kasi ya ajabu na Tanzania iwe nchi ya dunia ya kwanza kwa kwa kipindi kifupi, viongozi wote walio karibu na wananchi wakabidhiwe saluti zao. Viongozi wa dini wapewe. Dini zote. Maaskofu wote. Mapadre wote. Baba Paroko wote. Viongozi wote wa vigango. Wachungaji wote. Mashemasi wote na waingilisti wapewe mgao wao. Masheikh wote akianzia mkuu, wa mikoa wa wilaya na maimamu wote wakabidhiwe mgao wao. Viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali wapewe pia. Nadhani tukiongeza kasi ya mgao ndivyo na kasi ya maendeleo itakavyoongezeka. Tusibanie saluti la sivyo tutabaki kuwa masikini mpaka kiama.

Wednesday, June 08, 2005

Wabunge na Saluti

Kuna wakati nilionya kuhusu kutaka uheshimiwa kwa nguvu zote. Angalia sasa ile hoja ya saluti imerudi. Soma hapa.

Wanablogu wa Tanzania na Habari za Siasa

Nakumbuka siku za nyuma kidogo Msangi alitoa changamoto kujadili mapendekezo ya mwanazuoni mmoja aliyeonyesha wasiwasi wake kwamba wengi wa wanablogu Tanzania ni waandishi wa habari na pia hupendelea kuandika habari za siasa. Hili la la waandishi wengi kuwa pia wanablogu nitalijadili kwa kirefu wakati mwingine. Nitalihusisha na tabia ya kutafuta habari kwa watanzania. Kuhusu siasa ni kweli kwamba wengi hujadili habari za siasa. Kwa mtazamo wangu ni kwamba mfumo wa siasa wa nchi au siasa zilizopo ndizo hutoa picha kamili ya mwenendo mzima wa kila kitu. Kama siasa ni mbovu basi kutakuwa na teknolojia mbovu, kutakuwa na sera mbovu za elimu, elimu itakuwa duni, miundombinu duni. Kama mfumo wa siasa haueleweki hakuna kitakachoeleweka. Sera za uchumi hazitaeleweka. Kwa kifupi hakuna kitakachoeleweka au kufanikiwa kama kuna mfumo mbovu wa siasa. Wakati wa siku za nyuma tulikuwa tunasema ili tuendelee tunahitaji: watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Unaweza kuwa na watu, ardhi lakini ukakosa siasa safi. Kutakuwa hakuna maendeleo. Siasa safi na uongozi bora vinaendana sana kama una siasa mbovu utakuwa na viongozi wabovu. Huu ndio ukweli. Napenda kuamini kwamba wanablogu wengi wa Tanzania wamegundua hili, na wanajua kabisa siasa zilizopo ni mbovu na ndio maana leo utasikia mtu akisema ni lazima tukitaka tuendelee tusitegemee wafadhili, kesho mtu huyo huyo anasema hatuwezi kuendelea bila msaada wa wahisani. Huku ndiko kukosa mwelekeo wa siasa. Nadhani waandishi wanaona umuhimu wa kuwa na siasa safi kwanza halafu mengine yatakuja tuu. Najiandaa kumwandikia yule bwana mawazo yangu kwa kirefu. Mjadala uendelee.

Elimu ya Dini Tanzania

Hivi ule ufundishaji wa dini katika shule za sekondari umebadilishwa? Wakati tukiwa sekondari kulikuwa na utaratibu mbovu unaofundisha ukristo, uislamu, uprotestanti ukatoliki katika shule. Walikuwa wakija Mapadre, Wachungaji, masheik kufundisha dini. Wakija mnatenganishwa. Waislamu darasa lao, waprotestanti la kwao wakatoliki la kwao. Nilichukia mno utaratibu huu kwani ulikuwa haufundishi elimu ya dini bali dini. Matokeo yake mtu anafundishwa dini nyumbani, kanisani na misikitini na shuleni. Shule ingetakiwa itoe elimu ya dini. Tofauti ni kwamba shuleni watu wanatakiwa wafundishwe kufikiri, kuzielewa dini zote kuanzia za asili na za kuja na wasifundishwe na viongozi wa dini wahafidhina bali wafundishwe na watu wenye upeo mkubwa wa theolojia. Hii inawapa wanafunzi uwezo wa kuzielewa dini kwa undani na kuzijadili bila jazba hata baada ya kuhitimu shuleni. Mwenye uhakika kama mfumo huu umebadilishwa naomba aniambie kama bado tupige debe ubadilishwe.

Afrika na Mikakati ya kuisaidia

Kama kuna bara la majaribio basi ni Afrika. Katika kipindi cha miaka mitano tumesikia mambo kibao ya kusaidi umasikini Afrika; Mara HIPC, Mara Millenium Account Fund, Mara tume ya Blair, mara sijuhi Clinton Fund za UKIMWI mara Bush initiative. Huku kuna mikakati kibao kwa upande wa Afrika lakini yote pia inategeme wafadhili. Sijuhi haya majaribio yatazaa matunda. Sasa hivi Blair na Bush wanajadili pia kuhusu madeni na misada Afrika. Inasemekana watafikia makubaliano karibuni kuhusu kusamehewa madeni lakini kwa masharti fulani. Nakuapia kutakuwa hakuna jipya watakalokubaliana hii ni danganya toto tuu. Tutaambiwa madeni yatasamehewa baada ya masharti kibao kutimizwa. Kuna jipya katika hili? Wasichoonge ni kwamba hayo madeni tunayoambiwa yatafutwa yalitumikaje kwa faida ya walengwa wa Afrika. Utakuta asilimia 60 ya fedha zenyewe zilitafunwa na watu wao halafu tumeshalipa kama mara tatu ya tulivyopewa. Nakuambia kama kuna kufa ndiko huku.

Thursday, June 02, 2005

Kimya kingi

Nimekuwa kimya kwa muda mrefu sasa. Nilibanwa sana na bado nimebanwa. Nilikuwa nasubiri kwa hamu matokeo ya kura ya maoni kuhusu katiba ya umoja wa ulaya yaliyofanyika ufaransa na uholanzi. Matokeo yake nadhani mmeyasikia watu wamekataa. Niliandika makala kuhusu jumuiya ya afrika mashariki siku nyingi lakini sikuitundika kwa vile nilikuwa nangojea kura hizi. Nitaitundika baada ya kuweka machache kuhusu matokeo ya kura ya ufaransa na uholanzi.

Wednesday, May 18, 2005

Sakata la CITY water

Nakuambia mambo yameiva. Hawa jamaa wa city water nani kakuambia watakubali kirahisi? Wamesema wataenda mahakamani. Nakuhakikishia hii mambo itakuwa kama yale ya TTCL. Si mnakumbuka ilianza hivi hivi kama utani. Jamaa wakagoma kutoa pesa zilizobaki. Songombingo za kisheria zikaanza. Jamaa wakavimba mahakama zote mpaka ughaibuni wakaibuka washindi. Sasa hivi wanajimwaga bado. Nasikia wataongezewa tena mkataba. Nakuapia wadanganyika tutakoma kipindi hiki. Unajua kuna watu ukiwaambia kuna wazungu matapeli watakumaliza. Watakuambia hapana, mzungu hawezi kuwa tapeli, atakuwaje tapeli wakati wao ndio magwiji na wapiga debe wa utawala bora? Hapo ndio tunapodanganywa. Tusipojihadhari tutapigwa bao lingine.

Daktari azidi kubanwa

Yule Daktari mjerumani anayepinga matumizi ya dawa za makampuni ya kibeberu na kusisitiza matumizi ya vitamini amezuiwa na mahakama huko Berlin kuendelea kutangaza kwa kijerumani kwamba vitamini zake zina uwezo wa kutibu kansa la sivyo atatozwa faini ya EURO 250,000. Hatua hiyo inafuatia kugundulika kwamba kijana mmoja kwa jina la Dominik Feld mwenye umri wa miaka tisa alikufa baada ya kuanza kutumia vitamini za Dr. Rath na kusimamisha tiba ya kansa aliyokuwa akiendelea nayo. Mambo yanazidi kuwa moto. Mambo ya kufanyika maabara sasa yamegeuka ukumbi wa mabishano kama siasa. Nitazidi kuwafahamisha maendeleo ya mkasa huu.

Kumbukumbu ya Mwanaharakati Malcom X

Wiki hii huko New York kuna maonyesho ya shujaa Malcom X. Soma habari hiyo hapa

Monday, May 16, 2005

Umoja Wa mataifa wamkemea Daktari

Yule Daktari niliyewaambia anapinga dawa za kuongeza maisha kwa waathirika wa UKIMWI na badala yake kusisitiza vitamini amepigwa mkwara na umoja wa mataifa. Nimepata hii habari toka kwenye mlolongo fulani wa barua pepe sijuhi ilitoka kwenye chombo gani cha habari. Naiweka hapa ili muisome.

Makala Mpya

Nimeweka makala mpya inayoitwa kasi ya ahadi za ajira. Bonyeza hapa uisome. Makala nyingine zipo kwenye kona yangu ya makala.

Hivi Angola inauza wapi mafuta yake?

Afrika kweli kiboko. Mimi najiuliza ni wapi Angola inauza mafuta yake? Hii ni nchi ya SADC lakini sijuhi kama kuna nchi inayonunua mafuta toka Angola. Wengi wanaagiza uarabuni. Jumuiya kama SADC inafanya nini sijuhi kupunguza hali hii ya utegemezi wa kununua bidhaa zinazopatikana kwenye moja ya nchi za jumuiya toka nchi za mbali. Na usione ajabu Angola ikawa inaagiza mafuta toka nje kama inavyofanya Nigeria. Inauza Mafuta ghafi halafu inanunua yaliyosafishwa. Kweli safari ya Afrika bado ni ndefu!!

Saturday, May 14, 2005

Vita dhidi ya dawa za kurefusha maisha

Kuna malumbano makali Afrika ya Kusini baada ya kundi la wanaharakati wanaounga mkono matumizi ya dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa UKIMWI kupeleka kesi mahakamani kutaka Daktari wa Kijerumami Matthias Rath aache kupinga matumizi ya dawa hizo. Daktari huyu amekuwa mpinzani mkubwa wa ARV's kwa madai kwamba zina madhara makubwa sana kiafya. Badala yake anapendekeza lishe bora pamoja na matumizi ya vitamini muhimu kwa waathirika. Kesi ilipotajwa jana kulikuwa na makundi mawili, moja likimuunga mkono daktari huyu na lingine likimpinga. Nusura zipigwe nakuambia. Dr. Rath anasema kwamba madawa haya si chochote bali ni kuendeleza biashara ya makampuni makubwa ya dawa duniani. Unaweza kutembelea tovuti yake kwa kubonyeza hapa

City Water

Soma habari hii hapa uone jinsi hawa "wenzetu" wawekezaji wanavyofanya. Habari za hawa jamaa kwamba walikuwa hawana chochote zilisemwa siku nyingi sana lakini kama kawaida waliosema wakaanza kupigwa mabomu na viongozi. Wakaambiwa si wavumilivu. Wakaambiwa kampuni yenyewe ndio kwanza imeanza kazi lakini watanzania wanataka mabadiliko haraka sana. Wakaambiwa subirini. Sasa sijuhi wataombwa radhi wale waliokuwa wanasema ukweli kwamba hao jamaa hawataweza kufanya lolote au vipi? Wamesubiri na maneno yao yamethibitika. Wakati mwingine viongozi wajifunze kusikiliza pia sio kutoa maagizo na vitisho tuu kwa watu wenye mawazo na maoni tofauti.

Baba Moi Mjanja mwenzao

Nasikia kati ya mambo ambayo rais mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi ameyafanya ni pamoja na kujenga chuo kikuu katika shamba lake kubwa huko Turkana. Chuo hicho kwa mujibu wa taarifa nilizonazo kina wanafunzi karibia mia tatu. Hii kwa mtazamo wangu ni kitu kizuri zaidi kuliko wanavyofanya viongozi wengi wa Afrika kuweka fedha zao katika mabenki ya Uswisi au nchi nyingine za magharibi. Angalau zikiwekezwa nchini zinaweza kufaidisha wananchi.

Wednesday, May 11, 2005

Uwezo wa kuhoji

Watu wanapokuwa wamebanwa kisawasawa, wanakuwa wanafikiria tuu namna ya kupata chakula cha leo. Si kesho wala keshokutwa. Si Elimu wala chochote kingine. Ni chakula kwanza. Utafikiriaje chochote wakati njaa imefanya makao makuu kwenye tumbo lako? Hii ndiyo hali halisi inayowakabili watanzania wengi na hasa vijana. Hali ya ajira ni mbaya sana. Vijijini hakukaliki. Wakati mwingine tunawalaumu watanzania kwamba ni wavivu. Kama ukitaka kujua si wavivu kiasi cha kutisha, safiri kuanzia Tunduma mpaka Dar-es-Salaam, ona mazao yalivyopangwa barabarani kwa bei ya kutisha. Nina maana bei ndogo kabisa. Nenda Shoprite (kama Si Shopwrong) uone vitunguu na nyanya toka "bondeni" ambavyo vimekuzwa kimaajabu. Kwa ufupi ni kwamba mazingira ya vijijini hayavutii kukaa. Mimi nina imani kubwa sana hakuna kijana atakayekubali kuja kuhangaika siku nzima mjini akiuza shati moja kama angeweza kulima nyanya zake na zikamrudishia fedha zake. Kijana kama huyu anayefikiria chakula cha leo hawezi kuhoji mgombea anayemwambia atampatia ajira. Anachoangalia ni lini tarehe 30 oktoba itafika akapige kura ili mgombea apite na apate ajira. Kwamba itapatikanaje hataki kuhoji, hata nguvu za kuhoji hana. Angekuwa na uwezo angesogeza kalenda mbele ili Oktoba ifike mapema apate ajira yake. Kwake hajuhi hata kama mgombea ana mpango kabambe wa kuongeza ajira itamchukua muda mrefu kabla huo mpango kabambe haujafanikiwa. Kama ni kuanzisha viwanda itabidi vijengwe (Sitaki kuingia ndani sana hapa, naanzia tuu kwenye ujenzi), vikamilike vianze uzalishaji. Vyovyote vile ni lazima kutakuwa na maandalizi yatakayochukua muda mpaka ajira izalishwe. Ukweli huu ndio hao vijana watatakiwa waujue.

Tuesday, May 10, 2005

Ripoti ya kumaliza matatizo ya Afrika

Bonyeza hapa usome hii ripoti ambayo "itamaliza matatizo yote ya Afrika". Blair kaamua kuyamaliza ndugu zangu. Nasikia anatupenda kweli waafrika.

Mjadala wa Mama Kibaki

Wale ambao wanapenda kutoa maoni yao kuhusu mama Kibaki na hasira zake wanaweza kuyatoa hapa

Monday, May 09, 2005

Makala mbili

Nimeweka makala mbili nilizoandika. Moja inaitwa utamaduni wa amani. Isome kwa kubonyeza hapa na nyingine inaitwa habari za udaku. Isome hapa

Angalieni hawa Wabeligiji jamani.

Angalieni hawa Wabeligiji HAPA yasije yakatufika kwani na sisi huwa ni mabingwa wa kuiga.

Demokrasia na Mkumbokrasia

Hivi kweli wengi ndio Demokrasia? Nadhani kuna Demokrasia na Mkumbokrasia(Mobcracy). Kuna mtu leo ukimuuliza kwa nini anamshabikia mgombea fulani wa kiti cha urais hawezi kukupa sababu. Mwingine haelewi hata huyo anayemshabikia ana ajenda gani. Kuna msemo unazungumzwa sana sasa hivi- huyu ana mvuto. Muulize sasa mvuto kwa nini? Hapo ni heri umchape fimbo sita kuliko akupe jibu kwa sababu atakuwa hana. Kama wapiga kura wengi wanafuata mkumbo kutakuwa hakuna Demokrasia bali ni Mkumbokrasia.

Upofu wa Rangi

Kuna mjadala mzuri sana unaoendelea Afrika ya Kusini. Mjadala huu unauliza swali; je watu wa Afrika ya Kusini wanakuwa vipofu wa rangi tangu kukoma kwa utawala wa kibaguzi mwaka 1994? Upofu wa rangi hapa unatumika kuuliza swali ikiwa watu wamepunguza kubaguana kutokana na rangi zao. Mjadala ni mzuri sana. Wengine wanasema kuna maendeleo katika hilo, wengine wanasema hali bado si nzuri. Wanaosema mambo yamebadilika wanaangalia hoja kama vile weusi kupata kazi za ngazi ya juu, wengine wanasema yeyote anaruhusiwa kuwa mahali popote. Wanaosema mambo bado wanatoa hoja kama vile watu weupe kupinga kwa nguvu zote kitendo cha serikali kubadilisha majina ya baadhi ya miji au mitaa. Kilichovutia zaidi ni onyo lililotolewa kwamba katika hatua za kusaidia weusi, lazima wazungu wasianze kubaguliwa tena. Ukajaribu kurekebisha matatizo ya ubaguzi siku za nyuma ukazalisha ubaguzi mwingine. Hili ni muhimu pengine si kwa rangi tuu. Katika mazingira ya nchi nyingine ambapo ubaguzi wa rangi si wa msingi sana, kuna hatua za makusudi za kupunguza ubaguzi wa kijinsia kwa mfano. Pamoja na umuhimu huu hatua hizo zisizalishe tabaka jingine nyonge katika jamii- ni lazima kuwepo na mizania. Mwalimu Nyerere wakati fulani alisema kwamba jitihada za kupigana na ubaguzi wa rangi zilipofanikiwa ziliwasaidia si tuu weusi bali pia weupe waliokuwa wakiathiriwa na mfumo huo. Si weupe wote waliokuwa na hali nzuri chini ya mfumo wa kibaguzi.

Sunday, May 08, 2005

Sadaka na Rambirambi

Soma habari ya mchanganyiko wa sadaka na rambirambi hapa

Dawa za kulevya zinabwiwa mchana kweupe Dar

Soma habari hii ya kusikitisha hapa uone jinsi vijana wanavyoharibiwa na dawa za kulevya. Mtaalam Profesa Kilonzo anaona jamii nzima ina cha kufanya kwa hili; wazazi, vyombo vya sheria, vyombo vya dola na vijana wenyewe.

Saturday, May 07, 2005

Kupokea kwa kishindo

"Au kama wanaompokea wana kazi, basi kiongozi huyo ajue kuwa shughuli za uzalishaji katika taifa lenye matajiri asilimia moja na masikini asilimia 99 zimesimama". Hii ni nukuu toka kwa msomaji wa blogu hii kufuatia kale katabia nilikokemea cha viongozi kupokelewa kwa kishindo. Nakubaliana naye moja kwa moja sina ubishi na hili.

Msome Mzee Wa Kiraracha

"Bw. Mrema akasema ni rahisi Osama kupatikana, kuliko Kikwete kupenyeza mabadiliko katikati ya vigogo wa CCM. ?Ili Kikwete awe mnyama msafi, kwanza anatakiwa akaushe tope la CCM, kwa kukifumua Chama hicho na kukisuka upya. Kuondoa wachafu wote ambao wamekula tangu uhuru, hapo kidogo ataona mwanga, vinginevyo, atakuwa anajisumbua" . Msome zaidi hapa. Usisahau kwamba huyu pia ni mzee wa ruzuku.

Wapinzani Igeni kwa Howard

Bwana Michael Howard Kiongozi wa Chama cha Conservative huko Uingereza anaachia uongozi ili kumpisha mtu mwingine kuongoza chama hicho. Baada ya jitihada zake za kurudisha chama chake madarakani kushindwa kwa mara mbili mfululizo kaamua kujitoa nje licha ya safari hii kufanya vizuri ikilinganishwa na wakati wa uchaguzi uliopita. Wale wagombea urais wa maisha wa upande wa upinzani Tanzania anaowasema Macha nadhani wamemsikia. Tunatarajia watajifunza toka kwake. Soma habari hiyo hapa

Uchaguzi wa kihstoria

"Katibu wa Msikiti wa Mtambani, Sheikh Abdallah Ally alisema uchaguzi wa safari hii utakuwa ni wa kihistoria kwa sababu itakuwa ni mara ya kwanza kwa viongozi wa ngazi ya juu serikalini wote kuwa Waislamu. "Yaani Rais Mwislamu, Makamu wake Mwislamu na Rais wa Zanzibar Mwislamu. Katika awamu zilizopita ilikuwa haijawahi kutokea hivyo. Hii itafuta ile dhana kwamba Waislamu hawana elimu," alisema Sheikh Ally". Soma mawazo ya Sheikh huyu zaidi hapa

Friday, May 06, 2005

Wananchi na kuwapokea viongozi

Hivi tutaacha lini hii tabia ya kuwaambia watu waache kazi zao kwenda kupokea viongozi? Hii ni dalili mbaya lakini sijuhi kama inamwonyesha kiongozi kwamba kuna mzigo mkubwa unaomkabili. Sijuhi kama mtu mwenye shughuli yake ya maana ya kufanya ataicha na kwenda kukaa barabarani kumlaki kiongozi. Kiongozi anapaswa ajue kwamba akiona umati mkubwa sana aelewe wengi wao hawana shughuli ya kufanya. Badala ya kufurahi na kushangilia kwamba amepokelewa kwa kishindo ajue ana mzigo wa hawa ndugu- nina maana mzigo wa kuzalisha kazi za kufanya. Wengi wa wapokeaji hao bila shaka ni vijana (sina maana ya vijana wenye umri wamiaka 50 na kuendelea). Hili ni kundi ambalo limeathirika sana kwa kukosa shughuli ya kufanya. Kiongozi mwenye mtizamo mpana asifuraie kupokewa kwa kishindo, aione hiyo kama changamoto mbele yake. Aone kwamba watu wanaompokea, kumsikiliza na kumpamba siku nzima asilimia kubwa hawana cha kufanya. Wenye cha kufanya wako kwenye shughuli zao. Cha muhimu zaidi na zaidi ni kutowalazimisha watoto wadogo washiriki katika mapokezi kama hayo.

Thursday, May 05, 2005

Ujana na Urais

Kwa kweli kabla hujafa hujaumbika. Kijana anakuwa na miaka 55? Hiyo ni kali zaidi. Naambiwa mwenyekiti wa CCM katika hotuba yake ya mkutano mkuu wa kumtafuta mgombea alitoa wito kwamba ateuliwe mtu kijana. Angetoka wapi wakati hakuwepo kijana kwenye jopo hilo? Hata lile la watu 11 hakuwepo. Kuna watu wanaosema kwamba hotuba ya Mwenyekiti huyo imemsaidia mshindi. Wenye mtazamo huo wanakubali kwamba ni KIJANA. Kijana miaka 55? Hiyo ni definition mpya sana ya CCM. Lakini imekuwepo muda mrefu sana. Sasa hivi wastani wa muda wa kuishi kwa mtanzania ni kama miaka 46 sasa hapo ina maana kwamba hata umri wa wazee na vijana upangwe upya. Hata umri wa kustaafu kazini upunguzwe pengine uwe miaka 50. Umri wa kugombea urais kikatiba inabidi upunguzwe pia. Kila kitu kinabidi kirekebishwe kulingana na umri mpya wa kuishi kwa sababu hakuna matarajio kwamba siku za karibuni wastani huo utapanda.

Wednesday, May 04, 2005

Kutawala kwa zamu

Kuna wakati Macha alipendekeza njia za kumpata rais. Kati ya hizo ni kuwa na rais mwislamu na Mkristo kwa sababu watu wa dini hizi mbili wameshika bango sana. Nyingine ilikuwa ni Kumomba George Kichaka atusaidie kama anavyosaidia Iraq na Afrighanistan na nyingine ambazo hazitangazwi lakini ziko chini ya uangalizi wake. Mimi napendekeza utawala kwa zamu. Kwa vile rais anaweza kuongoza kwa miaka kumi basi ni rahisi sana hawa jamaa wote waliojitokeza kupitia CCM wakaongoza kwa zamu yaani mwaka mmoja mmoja watakachokubaliana tuu ni kuondoa "Outlier". Yule wa kumi na moja aondolewe kwa kigezo cha umri. Mwenye umri kubwa aombwe akapumzike kijijini kwake kwa amani, waliobaki watawale kwa mwaka mmoja mmoja. Hii itasaidia sana "kuimarisha mshikamno" wa chama twawala. Rais akichaguliwa ahakikishe anashawishi bunge kubadili katiba ili staili hii mpya ikubalike

Tuesday, May 03, 2005

Asilimia kumi, Rushwa na Sadaka

Umeshawahi kujiuliza uhusiano kati ya asilimia kumi, rushwa na sadaka? Swali hili linanitatiza sana kwani tunaambiwa Bwana Mungu wa Ibrahim, Yakobo na Isaka alisema tumtolee asilimia kumi ya pato letu. Upande mwingine tunaambiwa kwamba rushwa mara nyingi huwekwa katika kiwango cha asilimia kumi ya gharama halisi ya pato utakalopata. Kwenye mfumo wa rushwa,iIli kupata tenda tunaambiwa kwamba unahitajika uwape watoa tenda asilimia kumi. Kuna uhusiano wowote au ni hisia zangu tuu?
Sadaka mimi bado sijaweza kuielewa vizuri. Muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo anaitaji kweli visenti vyako? Kama anavihitaji basi asilimia kumi ni lazima iwe baada ya kutoa matumizi yako. Hivyo kama unapata laki moja, basi utoe kodi ya nyumba, chakula, usafiri, ada ya watoto, matibabu nakadhalika. Kitakachobaki toa asilimia kumi mpe muumba.

Ni kuongoza tuu?

Nimekuwa najiuliza swali hili kila mara. Hivi watu wanavyogombea uongozi nia yao huwa ni kuongoza tuu? Nilianza kujiuliza swali hili zamani sana. Sielekei sana kugundua sababu hasa ya hata mtu kwenda "kwa Babu" kutafuta uongozi. Hivi kuongoza tuu watu unakutolea macho hivyo? Nadhani sababu ni nyingi mno. Kuongoza ni kajisehemu kadogo sana ka sababu hizo. Sidhani kama utaenda kwa babu ili tuu uongoze watu. Watu wanapenda ujiko bwana. Kutambulika. Kuitwa mheshimiwa badala ya ndugu fulani. Kuna wakati bunge lilipoteza muda wa wapiga kura wao mwingi wakijadili kwamba sasa waitwe waheshimiwa na si ndugu au bwana au bi au bibi. Ni lazima watofautishwe na wengine. Sijuhi ni mpiga kura gani aliwatuma kwenda kujadili hayo mambo. Uheshimiwa unakuja tuu hata bila kuutungia kanuni. Timiza wajibu wako, fanya kazi kwa bidii. Toa mchango kwa jamii yako (si mchango wa harusi) mchango wa maendeleo- simanishi pesa hapa. Mawazo, kukusanya rasilimali watu zilizopo katika jamii, tambua uwezo wao, weka mawazo yao pamoja, buni mkakati wa maendeleo pamoja. Baada ya hapo utaona utaitwa mheshimiwa sana. Hutahitaji kwenda kujadili bungeni utambuliweje. Uchaguzi wa urais ndio huo. Watu nasikia wanachafuana vibaya sana. Wanapigana vikumbo. Wanapigania nafasi moja ambayo itakuja tena baada ya miaka kumi. Wanataka kuongoza watanzania. Je ni kuongoza tuu? Ni maslahi binafsi? ni kuitwa mheshimiwa, mtukufu mpendwa wetu rais........ Ni ving'ora vya kutishia wananchi wako na kusafirishwa kwa mwendo wa kasi kama vile unatorishwa au? Lazima tuwaulize hawa jamaa swali hili: Kwa nini unataka kuwa rais? Ukishapata jibu muulize kwa nini utumie sana nguvu, uchafu, matambiko na mambo mengine ya ajabu? Kuna la zaidi si kuongoza tuu.

KITABU CHA WAGENI